"Leo ni siku muhimu sana na kwakweli Mwanza mmefunika, nimesikia Uwanja umejaa na kule nje kumejaa na Viwanja vya Furahisha vimekuwa, haijawahi kutokea hongereni sana”-JPM
“Nilipotembelea Gereza la Butimba niliumia sana kukuta Wafungwa kule wengine kesi zao za kubambikiwa na najua hii iko Nchi nzima, mwingine amefungwa kisa tu aligombana kidogo na Mpenzi wake au Mshikaji wake”-JPM
“Natangaza kuwasamehe Wafungwa wengi leo wapatao 5533 ni mara ya kwanza kwa msamaha mkubwa kama huu kutokea, najua Watu watashangaa lakini nimeamua kutumia Siku hii ya Uhuru kusamehe maana sifurahi kuongoza Nchi yenye Watu wengi Magerezani”- JPM
“Msamaha huu nilioutoa kwa Wafungwa 5533 utawahusisha Wafungwa waliofungwa kati ya kipindi cha siku moja hadi mwaka mmoja, na wale Wafungwa waliofungwa Miaka mingi kama 30, 20 au 10 na wamebakiza muda mfupi kumaliza” -JPM
Miaka58YaUhuru
Mungu mpe maisha marefu sana huyu rais wetu,