09 Dec, 2019: Maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika. Wafungwa 5,533 wapata msamaha wa Rais. Mbowe ataka maridhiano ya Kitaifa

09 Dec, 2019: Maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika. Wafungwa 5,533 wapata msamaha wa Rais. Mbowe ataka maridhiano ya Kitaifa

... apumzike kwa amani Yonathan Netanyahu komandoo aliyewaokoa zaidi ya mateka 90 wa kiisrael pale Entebe 1976 utekaji uliosimamiwa na Nduli Idd Amin mwenyewe! Huyo ndiye komandoo wengine maigizo ya kusherehesha hafla tu.
[emoji3526]
 
Naona wapinzani akili inaanza kuwaingia na ule moyo wa kupinga pinga kila kitu umeanza kuwatoka.

Kwa hili nawapongeza sana . kitendo cha Mbowe kuhudhuria sherehe za Leo ni hakika akili imemrudia.

Magufuli ana uwezo kumfunza mpinzani wake kwa vitendo.

Najua wapo wapuuzi wachavhe watapinga lkn hamkatazwi pingine tu lakini ukweli Mbowe amenyooshwa.
Wanakesi ya mauaji hao ndio maana wanajipeleka peleka ili kupata huruma


USSR
 
Ni Kweli maana hata Sasa anashauriwa Na mama yako
 
Ni Kweli maana hata Sasa anashauriwa Na mama yako
 
Hpo lazima kna wengine watarudia uhalifu tu
Wengine hawakomagi

Ova
 
Ndugu zangu Watanzania, TUJUE SISI NI TAIFA, SISI NI WAMOJA KABLA YA VYAMA.
TUACHE KUJITENGA KTK MASUALA YA MSINGI AMBAYO AKILI YAKO AU YANGU INAJUA HATA LEO UKISHINDA NAFASI YA RAIS WA TANZANIA CHAMA CHAKO HAKIWEZI KUONDOA KITU HICHO.
MFANO WA MACHACHE HAYO NI BENDERA YETU, NEMBO YETU, WIMBO WA TAIFA, TAREHE ZOTE ZA UHURU ,MUUNGANO WETU ,JINA LA TAIFA ,ALAMA NYINGINE ZA TAIFA KAMA MWENGE nk.
NAMSHANGAA KAKA YANGU ZITTO KWA KUENDELEA KUSUSIA SHUGHULI RASMI ZA TAIFA.
NAAMINI KAMA KIONGOZI ANAJUA HAYA NA AKAJIFANYA HAJUA, MIMI HUWA NAREJEA MSEMO WA MWANAFALSAFA (ARISTOTLE ),alisema
"UNAWEZA KUWA NA AKILI NYINGI, LAKINI KAMA AKILI ZAKO HAZIENDANI NA WENZIO NA HAZIHESHIMU WENGINE NA HAZINA MSAADA KWA TAIFA BASI AKILI HIZO ZINAKUTOSHA WEWE MWENYEWE"
kwa maana na kwa mantiki hii yoyote anayedhani Siku ya UHURU NI YA KINA FULANI TU Kama Zitto BASI AKILI ZAKE ZINAMTOSHA YEYE PEKEE [emoji1334]

Hassan K. Almas,
KATIBU MKUU - NRA
(MWENYEKITI WA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA BORA -BARAZA LA TAIFA LA VYAMA VYA SIASA TANZANIA)
 
"Leo ni siku muhimu sana na kwakweli Mwanza mmefunika, nimesikia Uwanja umejaa na kule nje kumejaa na Viwanja vya Furahisha vimekuwa, haijawahi kutokea hongereni sana”-JPM


“Nilipotembelea Gereza la Butimba niliumia sana kukuta Wafungwa kule wengine kesi zao za kubambikiwa na najua hii iko Nchi nzima, mwingine amefungwa kisa tu aligombana kidogo na Mpenzi wake au Mshikaji wake”-JPM

“Natangaza kuwasamehe Wafungwa wengi leo wapatao 5533 ni mara ya kwanza kwa msamaha mkubwa kama huu kutokea, najua Watu watashangaa lakini nimeamua kutumia Siku hii ya Uhuru kusamehe maana sifurahi kuongoza Nchi yenye Watu wengi Magerezani”- JPM


“Msamaha huu nilioutoa kwa Wafungwa 5533 utawahusisha Wafungwa waliofungwa kati ya kipindi cha siku moja hadi mwaka mmoja, na wale Wafungwa waliofungwa Miaka mingi kama 30, 20 au 10 na wamebakiza muda mfupi kumaliza” -JPM
Miaka58YaUhuru
Mungu mpe maisha marefu sana huyu rais wetu,
 
Kwani kabla ya msamaha idadi ilikuwa ni wangapi?
 
Ukiona amani inasisitizwa ujue wale ni wanafiki na waoga, tena ni watu Wa mapambio tu hamna lolote!
 
Maridhiano na upendo awaambie wachaga wenzio ambao walikuwa wakiona makabila mengine Ngedere kauli hiyo akaitoe kilimanjaro
Acha ukabila wewe
Tabia ya watu wawili au wanne sio tabia ya watu wote tena kama hujui katika wale madiwani wa kwanza kabisa kuhama upinzani kwa lengo la kuunga juhudi ni kutoka huko huko kasikazini na kwenye jimbo la mbowe ni karibu madiwani wote waliondoka upinzani sababu ya JPM
 
Msimamo wa Zitto kususia hizo sherehe nauunga mkono. Sioni haja ya kushiriki sherehe na wahuni wowote wale kwa kisingizio chochote kile.
 
Miongoni mwa siku rais Magafuli ameonekana akiwa na furaha iliyopitiliza ni leo. Ameonekana mwenye furaha, raha, bashasha na mwenye hisia za Kitanzania yenye umoja. Kuwepo kwa viongozi wa upinzania hasa hasa Mbowe wa CHADEMA kumeleta relief kubwa sana ya kitaifa.
Kuna mambo kumbe huwa yanamnyima raha Magufuli likiwemo hili la mgawanyiko wa Waranzania kwa itikadi zao.
Sherehe za leo zimenoga sana kuliko za miaka mingine.

Na kuna haja sasa ya sherehe hizi kuwa zinafanyika mikoani kwani Mwanza ime prove hilo.
 
Back
Top Bottom