09 Dec, 2019: Maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika. Wafungwa 5,533 wapata msamaha wa Rais. Mbowe ataka maridhiano ya Kitaifa

09 Dec, 2019: Maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika. Wafungwa 5,533 wapata msamaha wa Rais. Mbowe ataka maridhiano ya Kitaifa

Pale nadhani Hakutaka kumaanisha Kuwa Mungu ni yeye
Ule msamaha wa wafungwa ni msamaha wa rais, aliyetoa msamaha kwa wafungwa hao ni rais Magufuli. Kitendo cha kusema huu msamaha sio wake ni msamaha uliotolewa na Mungu, by canotation yeye ni mungu!. Alipaswa aseme msamaha huu ni Mungu ndie ameniwezesha mimi rais Magufuli niwasamehe nyinyi hivyo ni Mungu amenitumia mimi kuwasamehe. Msamaha wa wafungwa ni msamaha wa rais na sio msamaha wa Mungu!.
P
 
Jambo jema Sana Leo wapinzani kuhudhulia hakika nafikili hiyo ndo Maana halisi ya kula na kipofu.

Na hiyo isiishie hapo waende mbali zaidi wawapo na mikutano ambayo sio ya Siri ya chama Basi wawaalike hao hao viongozi wa kitaifa na maafisa usalama wa nchi,wakuu wa polisi Kama itifaki inaruhusu,wakuu wa mikoa,madc n k.

Hiyo itawaongezea uaminifu kwamba lengo Lao sio baya Bali ni katika kulisongesha gurudumu la maendeleo ya taifa tofauti na imani potofu za watu wachache wenye mitazamo hasi kuhusu upinzani.

Lazima wabadilike na wabadilike aina ya siasa wanazofanya ili ziwe na tija kwa wananchi na nchi kwa ujumla kuliko Sasa ambapo zimejikita zaidi kiharakati ukili ganisha na chama kinacholenga kushika dola.

Mi nafikili kiongozi mkuu wa upinzani ni mtu mzito Sana hivyo alipaswa apewe heshima ya namna yake Kama viongozi wengine wa kitaifa Kama busara zaidi zingetumika.

Wakae chini watafakari upya wapi waliteleza kwa sababu chama kimeporomoka kwa kasi ya ajabu,wanachama wamehamia chama tawala hiyo inaonyesha namna gani wamepoteza Imani na chama tofauti na walichotegemea kipindi wanajiunga.
'Na hiyo isiishie hapo waende mbali zaidi wawapo na mikutano ambayo sio ya Siri ya chama Basi wawaalike hao hao viongozi wa kitaifa na maafisa usalama wa nchi,wakuu wa polisi Kama itifaki inaruhusu,wakuu wa mikoa,madc n k.'

Mbona NEC ya CCM ikikaa hua hatuwaoni hao wakuu wa usalama wakihudhuria?
 
... apumzike kwa amani Yonathan Netanyahu komandoo aliyewaokoa zaidi ya mateka 90 wa kiisrael pale Entebe 1976 utekaji uliosimamiwa na Nduli Idd Amin mwenyewe! Huyo ndiye komandoo wengine maigizo ya kusherehesha hafla tu.
 
Inaelekea hata wewe ni mchawi. Unawezaje kuangalia tv na ku conclude kwamba hawa ni wachawi? Hayo mavazi ni jadi, ni mavazi wanayovaa wapiganaji wa kijadi waendapo vitani. Hizo ni mbinu za kumtisha adui.
Au umezaliwa miaka ya tisini nini. Ndio maana tunawafundisha hayo mjue. Ulitaka waje na suti kama mchungaji wako kanisani???
 
Kuwa upinzani sio dhambi Eti kanyoshwa mbowe ajanyoshwa ni kawa muelewa tu hiyo kauli ya kunyoshwa ni yakichochezi.
 
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amewasamehe wafungwa wapatao 5,533.

Ametoa msamaha huu sasa hivi kwenye sherehe za Uhuru zinazokaribia kumalizika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Msamaha huo utawahusu wafungwa waliobakiza muda wa chini ya mwaka mmoja kuishi gerezani.
 
Rais Magufuli atoa msamaha wa kihitoria wa wafungwa 5,33!.
Huu ni msamaha mkubwa kabisa kuwahi kutokea katika historia ya Tanzania tangu tupate uhuru.

Kiukweli rais Magufuli atabarikiwa sana. Hata kama rais Magufuli ana makosa yake madogo madogo ya kibinaadamu,
Ila alipomalizia ameharibu kusema msamaha huu umetolewa na Mungu ambapo sasa connotation yeye ni mungu!.
P
Soma Warumi 13
Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu. 2 Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu. 3 Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu. 4 Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu. 5 Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri.
6 Kwa sababu hiyo hiyo mnalipa kodi, kwa maana watawala ni watumishi wa Mungu ambao hutumia muda wao wote kutawala. 7 Wal ipeni wote haki zao; mtu wakodi mlipe kodi; na mtoza ushuru mli pe ushuru; astahilie kunyenyekewa, mnyenyekee; astahiliye hesh ima, mheshimu.
 
Naangalia maadhimisho ya sherehe ya miaka 58 ya Uhuru, Kuna kikundi cha sungusungu kwa kweli wamevaa kichawi kabisa na matendo yao hata hayaeleweki.
Bila shaka hawa ndio wale elfu moja waliosema watamroga mtu yeyote atakayetaka kushindana na Magufuli.
vijana soft soft mnakwama wapi?
 
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amewasamehe wafungwa wapatao 5,533.

Ametoa msamaha huu sasa hivi kwenye sherehe za Uhuru zinazokaribia kumalizika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Msamaha huo utawahusu wafungwa waliobakiza muda wa chini ya mwaka mmoja kuishi gerezani.
Naona mipango ya kuongeza idadi ya kura inafanyika.
 
Naona wapinzani akili inaanza kuwaingia na ule moyo wa kupinga pinga kila kitu umeanza kuwatoka.

Kwa hili nawapongeza sana . kitendo cha Mbowe kuhudhuria sherehe za Leo ni hakika akili imemrudia.

Magufuli ana uwezo kumfunza mpinzani wake kwa vitendo.

Najua wapo wapuuzi wachavhe watapinga lkn hamkatazwi pingine tu lakini ukweli Mbowe amenyooshwa.
Akili yako ya matope wewe, huna ulijualo, kazi yako kulamba makalio ya wakubwa wenu ndani ya chama cha mauaji
 
Ujumbe wa Amani, Umoja na Mshikamano umetawala kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 58 ya uhuru wa Tanzania zilizofanyika jijini Mwanza.

Kwa kuonesha kuwa Tanzania ni taifa pekee lenye amani, Rais Magufuli amewaita viongozi wa vyama pinzani watoe neno ambapo nao wakasisitiza umuhimu wa amani
 
Back
Top Bottom