09 Dec, 2019: Maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika. Wafungwa 5,533 wapata msamaha wa Rais. Mbowe ataka maridhiano ya Kitaifa

09 Dec, 2019: Maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika. Wafungwa 5,533 wapata msamaha wa Rais. Mbowe ataka maridhiano ya Kitaifa

Unajua maana au definition ya ukoloni???!!! Au umejawa na chuki ambazo zinakufanya uropoke hovyo??
Chuki ni kweli ninayo, Ila kiwango Cha chuki Cha Mhe Magufuli ni kikubwa mno na siwezi kumzidi kiukweli!!
 
Dhana ya wewe ukisusa wengine wala huku maisha yakiendelea kama kawaida imeanza kuwaingia baadhi ya wanasiasa!

Ni sawa na mtoto ambaye kama hujamtimizia baadhi ya maombi yake hususa kula chakula ulichompikia akitegemea utambembeleza lakini ukimpuuza baadaye anaanza tena kukuomba chakula akidai ana njaa!

Niwapongeze wale wanasiasa ambao wamefanya self assessment na kugundua kuwa kususa kwao kwenye sherehe za kitaifa hakuna impact yoyote ya kisiasa kwa taifa na kwa sababu hiyo wameamua kubadili msimamo!
Mengi yamebadilika.Jiwe hajaahirisha sherehe kama miaka ile,sehemu ya sherehe pia siyo Dar es salaam kwa 'KI-MUNGU" cha kuchonga,na 'uchafuzi' umekaribia. Kila mmoja na hesabu zake .
 
Ni
Usinitafutie kesi kuwa Amiri Jeshi Mkuu wetu anamuogopa mtu fulani nikamponza bure huyo mtu!.

Angalia tarehe ya bandiko hili, halafu linganisha nini kilimtokea mtu huyu baada ya bandiko hili

Please!.
P
Mkuu nimekupata.asante kwa bandiko lako
 
Habari wadau! Tukutane hapa kujua yanayojiri leo mwanza kwenye mahadhimisho ya miaka ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika:

Update: Majeshi mbalimbali ya gwaride yanaingia uwanjani.
Updates: Waziri mkuu na rais wa Zanzibar wanaingia uwanjani pamoja na makamu wa rais

Leo nawaona wanajeshi toka China wakiwa jukwaa kuu.

​



09:15 Rais Magufuli ndio anaingia uwanjani

Tanganyika ilishakufa na jina likafutwa , hii sikukuu ni batili
 
Rais anazungumzia SGR
Kipande cha Dodoma Dar
Kipande cha Mwanza Isaka
Kipande Dar Moshi Arusha
Vipi Dodoma Isaka mbona hapatajwi?
 
Anasema tumenunua ndege 11 lakini nilosikia wanasema zipo 8
 
Wachangiaji mmekwenda wapi leo? Hamuonekani humu
 
Mila na Desturi zetu ziheshimiwe,.Sema hamna hata kapicha.
 
Wafungwa wa siku 1 mpaka mwaka mmoja wasamehewa

Na wale waliobakiza mwaka mmoja mpaka kumaliza kifungo chao

Wale wa kesi ya Chama pinzani wangefungwa leo wangetoka
 
Rais Magufuli atoa msamaha wa kihitoria wa wafungwa 5,533!.
Huu ni msamaha mkubwa kabisa kuwahi kutokea katika historia ya Tanzania tangu tupate uhuru.

Kiukweli rais Magufuli atabarikiwa sana. Hata kama rais Magufuli ana makosa yake madogo madogo ya kibinaadamu, japo alipomalizia ameharibu kusema msamaha huu umetolewa na Mungu, kwa vile msamaha huo ni msamaha wa rais na yeye ndie rais, ndiye aliyetia msamaha huo, hivyo kusema msamaha huo umetolewa na Mungu, connotations yake yeye ni mungu!, lakini kwa vile na mimi ni Msukuma na najua Kiswahili kinawatatiza sana Wasukuma, alimaanisha ni Mungu ndio amemuwezesha yeye kutoa msamaha huo hivyo wamshukuru Mungu kumuwezesha Magufuli kuwasamehe!.
P
 
Leo katika sherehe za uhuru , mwanza . Raisi JPM ametoa msamaha kwa wafungwa idadi kubwa ya zaidi ya 5533 . tumshukuru kwa msamaha huo na pia hongera kwa wafungwa waliopewa msamaha huo.
 
Back
Top Bottom