TANZIA 10 wafariki baada ya lori la Polisi kugongana na kirikuu Kilimanjaro

TANZIA 10 wafariki baada ya lori la Polisi kugongana na kirikuu Kilimanjaro

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
#BREAKINGNEWS: Watu 10 wamefariki dunia na mwingine mmoja kujeruhiwa baada ya Lori la Polisi kugongana na gari dogo la mizigo (KIRIKUU), katika eneo la Datch Conner, Siha mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa Wilaya ya Siha Christopher Timbuka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, huku akibainisha kuwa katika ajali hiyo waliofariki wanawake ni 6 na Wanaume 4, majeruhi wapo katika hospitali ya Siha na Maiti imehifadhiwa hospitali ya Kibon'oto, ambapo taratibu za kutambua waliofariki zinafanyika.

#itvdigital

FB_IMG_1692362875932.jpg
 
Pole kwa wafiwa,Kwenye Kirikuu walikuwa wangapi na wangapi wamekufa?na kwenye Lori la polisi pia walikuwa wangapi na wangapi wamekufa?
Inavoonekana waliokufa watakuwa wa kwenye kirikuu tu maana hawajasema kama lori lilipinduka, kwa kuangalia height ya Lori bila kuanguka abiria hawawezi pata madhara (assumption)
 
Watu 10 wamefariki dunia na mwingine mmoja kujeruhiwa baada ya Lori la Polisi kugongana na gari dogo la mizigo (KIRIKUU), katika eneo la Datch Conner, Siha mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa Wilaya ya Siha Christopher Timbuka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, huku akibainisha kuwa katika ajali hiyo waliofariki wanawake ni 6 na Wanaume 4, majeruhi wapo katika hospitali ya Siha na Maiti imehifadhiwa hospitali ya Kibon'oto, ambapo taratibu za kutambua waliofariki zinafanyika.
 
Watu 10 wamefariki dunia kufuatia ajali ya gari aina ya Toyota (Kirikuu) iliyogongana na gari la polisi Layland Ashok wakiwemo wafanyabiashara tisa (9) na askari polisi mmoja wa Chuo cha Polisi Moshi.

Gari hizo ziligongana uso kwa uso kufuatia gari hiyo ya mizigo kupasuka gurudumu la mbele. Ajali hiyo imetokea eneo la Dachikona, katika kijiji cha Wiri, Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa Wilaya Siha, Christopher Timbuka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea leo, Agosti 18 majira ya Mchana na miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Siha.

"Idadi ya waliopoteza maisha imeongezeka na kufukia watu 10 na amepatikana majeruhi mmoja ambaye hali yake inaendelea vizuri."
 
Back
Top Bottom