TANZIA 10 wafariki baada ya lori la Polisi kugongana na kirikuu Kilimanjaro

TANZIA 10 wafariki baada ya lori la Polisi kugongana na kirikuu Kilimanjaro

Watu 10 wamefariki dunia kufuatia ajali ya gari aina ya Toyota (Kirikuu) iliyogongana na gari la polisi Layland Ashok wakiwemo wafanyabiashara tisa (9) na askari polisi mmoja wa Chuo cha Polisi Moshi.

Gari hizo ziligongana uso kwa uso kufuatia gari hiyo ya mizigo kupasuka gurudumu la mbele. Ajali hiyo imetokea eneo la Dachikona, katika kijiji cha Wiri, Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa Wilaya Siha, Christopher Timbuka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea leo, Agosti 18 majira ya Mchana na miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Siha.

"Idadi ya waliopoteza maisha imeongezeka na kufukia watu 10 na amepatikana majeruhi mmoja ambaye hali yake inaendelea vizuri."

Poleni ndugu , jamaa na marafiki.
 
Walikuwa wanafukuzana mmoja akawekewa bodi?
 
Una hakika ni tetesi hiyo?

Unajua hii Habari imeletwa na kuwa confirmed tangu jana?

Shida ni nini kwani, kuwa wa kwanza kuleta Habari au?
 
Back
Top Bottom