Hivi hata swala hana urafiki na binadamu!? Tunashindwaje kumfuga aisee!?
Kiasi wanyama wote walikuwa porini nasi wanadamu ndio tukaanza wafuga. Hivyo mwanadamu kwa miaka mingi amekuwa akifanya juhudi za kujaribu kuwafuga wanyama kadhaa, wapo waliofanikiwa na wapo alioshindwa kabisa. Hawa wanyama tunaowafuga leo [Farasi, Mbuzi, Ng'ombe, Kondoo na Nguruwe] walikuwa ni wanyama pori waliokuwa wakipatikana eneo la ulaya na asia, huku kwetu waliletwa in the course of human interaction.
Katika wanyama wote ambao wanadamu tumefanikiwa kuwafuga, ni wamekuwa na sifa zifuatazo [ikikosekana hata moja, ilimfanya mnyama huyo iwe ngumu kumfuga]
1. Chakula. Wanyama walao nyama ni ngumu sana kuwafuga. Mf Simba ana kula wastani wa kilo 6 kwa siku. Sasa imagine awe na watoto wake. Unatumia karibu ef 60,000 kwa siku kumlisha. Herbivorous ndio hasa wanaofugwa.
2. Kasi ya ukuaji. Wanyama wanaokuwa haraka ndio wamefugwa. Mf Tembo anahitaji miaka 15 ndio awe amekuwa, sasa hii ni hasara.
3. Namna ya uzalianaji. Wanyama wenye uwezo wa kujamiiana wakiwa wamefungwa ndio ambao wamefugika. Mf Duma hawezi kujamiiana akiwa amefungiwa sehemu mbele ya wanadamu. Pia mchakato wake wa kumpata jike, kukubaliwa na kurutibishwa yai huchukua siku kadhaa. Kinyume na wanyama kama ng'ombe au mbuzi.
4. Madhala kwa wanadamu. Mnyama anayeweza mdhuru mwanadamu, huyu imeshindikana kumfuga. Mfano Zebra ana tabia ya kung'ata na hatabiriki.
5. Hulka ya kupanick. Wapo wanyama ambao hawana hulka ya kupanick sana kwenye hatari na huhitaji binadamu mara nyingi ndio awanusuru. Mf Mbuzi, ndio maana Chatu huwala mbuzi kirahisi bandani.
Wengine wana hulka ya Kupanick na kuruka na kukimbia kwa haraka wanapokuwa hatarini. Mf Swala. Swala akisense hatari anaruka karibu futi 10 juu. Maana yake kwenye banda ni rahisi kujiumiza. Lakini pia akiwa anakimbia speed ambayo mwanadamu ni kazi sana kummudu. Mruko wa suala ni hadi futi 33. Hivyo suala ni ngumu sana kumdhibiti. Huna hakika kama nikianza mfuga leo, siku kadhaa mbele nitakuwa naye, sasa huwezi fanya investment isiyo na hakika.