1894 Loniel Walter Rothschild akivinjari London na punda milia

1894 Loniel Walter Rothschild akivinjari London na punda milia

Sio kweli, watu wanafuga (domesticate) Tembo, Chui, Cape Buffalo, Simba, Fisi nk, sembuse Zebra ambaye ni jamii ya Farasi, Mule na Punda??.

Huyo ni nyara ya serikali hiyo ndiyo sababu kubwa watu hawajishugulishi naye isitoshe Punda na Farasi na ng'ombe ni wengi na wanatosheleza mahitaji ya drafting, (draft animals).
Hii ni elimu mpya kabisa kwangu.

Hebu nifafanulie domestication ya simba imefanyikaje na Wapi?
 
Hii ni elimu mpya kabisa kwangu.

Hebu nifafanulie domestication ya simba imefanyikaje na Wapi?

Alas, Uarabuni na hata hapa Africa simba (w)amewahi kufugwa na Mzungu na mkewe kuna Video (nimesahau jina??! something Lisa the lion??), na huyo simba waka m release to the wild ili ajitegemee na ikashindikana na wakaamua kumchukua na kuendelea kuishi naye kama domestic pet hadi walipokuja Simba dume na kumchukua to the wild, ni historia ya kitambo iliyotokea hapa hapa Africa.

Simba Wanafugwa Uarabuni, hata Mike Tyson alikuwa kafuga Tiger.

Hakuna mnyama asiweza kuwa domesticated mbele ya Binadamu, Binadamu ni superior over all animals, kinachotakiwa ni kujua ni jinsi gani mnyama afundishwe ili awe tamed na hatimaye domesticated kwani kila mnyama anayo staili yake ya kufundishwa.
 
Labda useme wanamiliki 95% ya mining industry duniani, hapo kidogo tunaweza ku compromise.,
lakini sio (100-5)% ya utajiri wa dunia [emoji1787], ingalikuwa ni hivyo hao wangekuwa ni demigods.

Utajiri upo Mashariki ya kati from the "black gold"
Ila hawaumiliki...mmiliki ni usa na kampuni zake kacheki documentary ya six sisters ndio utajua hujui.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mtu wa kawaida ukimbiwa kuhusu familia ya Rothschild unaweza kuhisi labda ni watu wa kawaida tu. Lakini historia inatuambia vinginevyo kabisa. Kuna matukio makubwa wameyafanya hapa duniani ambayo hata tajiri wa kawaida kama Jeff Bezos asingeweza kuyafanya. Kuna mambo mengi sana wanasingiziwa (Exaggeration), japo ukweli ni kwamba hii ni moja ya familia yenye nguvu sana.

-Wao ndiyo waliokuwa wanawakopesha pesa ufalme wa Uingereza na kuwasaidia kufannya malipo ya wanajeshi kipindi chote cha miaka 20 ya vita vya Napoleon. Alitengeneza mfumo wa mawasiliano ambao ulikuwa unampa taarifa nyeti kabla hata ya wafalme ambazo alizitumia sana katika kufahamu mwelekeo wa soko la hisa na kuchanga karata zake vizuri.

-Wao ndiyo waliomsaidia Myahudi Mwenzao na Waziri Mkuu wa Uingereza Benjamin Disraeli kujenga mfereji wa Suez Canal. Lionel Rothschild ndiyo alitoa ule mkopo ili kuisaidia Uingereza ipambane na Ujerumani ya Bismarck ambayo ilikuwa imejipanga kushindana na Uingereza popote pale duniani. Inasemekana Disraeli alikuwa anaogopa kwamba wao walikuwa hawana hela nyingi sana, na endapo Bismarck angesikia basi angetumia mapesa ya Ujerumani kuhujumu ujenzi wa ule mfereji.

-Wao ndiyo wamiliki wakubwa wa ardhi ya Israeli/Palestine baada ya kuinunua kutoka kwa mabwanyenye wa Kituruki (Sursock Family) na machifu wa Lebanon. Pesa za malipo ambazo walipewa machifu wa kilebanoni ndiyo zilitumika kutengeneza Lebanon ambayo ilikuwa ndiyo mji uliondelea zaidi (The Metropolitan of the Levant) wakati huo kabla haijaharibika. Walinunua ardhi kubwa na kuwaambia wayahudi waanze kuishi, wazungu, waturuki na waarabu walilamba hizi pesa ndiyo maana mpaka leo wakubwa wa dunia hukosa ujasiri kupambana na wazayuni.

Mengi sana kuhusu historia ya hawa watu yameandikwa na msomi nguli, Prof Richard Roberts na siyo mtu wa mtaani tu ambaye anatengeneza nadharia kutoka vijiweni (Conspiracy Theory). Kitu kimoja ambacho huwa nashindwa kuwaelewa watu ni kwamba wengi tunaangalia utajiri wa watu kwa zile Networth ambazo zimeandikwa na Forbes, WELL AND GOOD.

Japo kilichotokea jana na juzi kwenye THE PANDORA PAPERS kinafanya tujifikirie mara mbilimbili. Kuna watu wana pesa nyingi sana na wamezificha kwenye visiwa sehemu nyingine duniani kwa kutumia majina mengine au shell companies. Kuna watu naangalia jana pesa walizokuwa nazo na wala sijawahi kuwaona Forbes.

Hebu fikiria wakina Rockerfeller, kampuni lao la Standard Oil ndiyo limezaa karibia kampuni zote kubwa za mafuta duniani na familia ina hisa karibia kwenye kila kampuni la mafuta. Exxon, Mobil, Chevron, BP, Amaco, Texaco you name it. Lakini huwezi kutajiwa sehemu pesa zao halisi ni kiasi gani.

NB: Siku zote kufahamu nguvu ya mtu angalia sana matendo yake kuliko maneno yake. Ukiangalia matendo ya familia kama The Rothschild na Rockefeller, jinsi ambavyo wamekuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa pamoja kufadhili miradi mikubwa bure kabisa (Wenyewe wanasema Philanthropy) nadhani unaweza kubakia mdomo wazi tu.

Mwaka jana tu hapa, tajiri George Soros kasema anatoa msaada wa Bilioni 1.5 (Kama trilioni mbili hivi za kitanzania) kujenga Chuo Kikuu ambacho kitadaihili wanafunzi wenye mlengo wa kiliberali ili kupambana na Populism na Dictatorship ambao vimekuwa vikitumiwa na wanasiasa kama Narendra Modi, Xi-Jinping, Vladmir Putin na Donald Trump.

Just think, Soros yeye ni moja ya waratibu kabisa wa The Colour Revolutions na anafadhili vyama vingi na taasisi za kibinadamu (NGO's) Ulaya kote. Lakini pesa zake ni kidogo kuliko hata Mark Zuckerberg, Elon Musk au Jeff Bezos. Aidha hawa matajiri wanasingiziwa au kuna kitu hatukifahamu......
 
Alas, Uarabuni na hata hapa Africa simba (w)amewahi kufugwa na Mzungu na mkewe kuna Video (nimesahau jina??! something Lisa the lion??), na huyo simba waka m release to the wild ili ajitegemee na ikashindikana na wakaamua kumchukua na kuendelea kuishi naye kama domestic pet hadi walipokuja Simba dume na kumchukua to the wild, ni historia ya kitambo iliyotokea hapa hapa Africa.

Simba Wanafugwa Uarabuni, hata Mike Tyson alikuwa kafuga Tiger.

Hakuna mnyama asiweza kuwa domesticated mbele ya Binadamu, Binadamu ni superior over all animals, kinachotakiwa ni kujua ni jinsi gani mnyama afundishwe ili awe tamed na hatimaye domesticated kwani kila mnyama anayo staili yake ya kufundishwa.
Hata cases unazotoa ni chache mno, hii ni jibu kuwa upo walakini kwenye ufugaji wao.

Huyo Tiger wa Tyson aliachana naye kwa sababu alijeruhi mtu—ndio sababu kubwa kwanini ufugaji wa simba ni mgumu. Nachosema ni kuwa, watu wamejaribu na wanaendelea kujaribu lakini ni ngumu sana kufuga baadhi ya wanyama.
 
Hata mbwa wanajeruhi watu pia, je ufugaji wa mbwa ni mgumu??!!, suala la ufugaji wa wanyama ni necessity, mtu afuge Simba kwa ajili gani?? au Fisi, Chui nk??.---- sababu hiyo ndio inayo hold.

Necessity ndiyo inayo determine ufugaji, lakini kila mnyama ANAWEZA KUFUGWA NA AKAFUNDISHWA na binadamu, and that's what makes human being superior over other animals, panya anakuwa tamed na domosticated in its level and be used in land demining, angalia mradi wa SUA, apopo.
 
Mbwa sio sawa na Simba. Mbwa anaattack adui au akiwa na maradhi ya akili. Lakini Simba ana attack yeyote bila kujali adui wala aliyemfuga (ili apate chakula).

Ufugaji ni selection ambayo imechukua maelfu ya miaka hadi kufikia leo simba hafugwi na Mbwa anafugwa.

Wale wanyama watano wanaofugwa wote hawakuwa huku Afrika, lakini je huku afrika hawakujaribu kuwafuga? Walijaribu kama walivyojaribu kumfuga zebra lakini ilishindikana.

Hii necessity unayoizungumzia hapa ni kwenye modern world. Mf, Farasi wamefika Afrika miaka ya 1600, kabla ya hapo hawakuwa na option ya zebra na farasi, it was only zebra ambaye walishindwa kumfuga.
 
Mbwa sio sawa na Simba. Mbwa anaattack adui au akiwa na maradhi ya akili. Lakini Simba ana attack yeyote bila kujali adui wala aliyemfuga (ili apate chakula).

Ufugaji ni selection ambayo imechukua maelfu ya miaka hadi kufikia leo simba hafugwi na Mbwa anafugwa.

Wale wanyama watano wanaofugwa wote hawakuwa huku Afrika, lakini je huku afrika hawakujaribu kuwafuga? Walijaribu kama walivyojaribu kumfuga zebra lakini ilishindikana.

Umesoma vizuri hicho ulicholeta??

Imeandikwa; "While attempts at demostication have failed some individuals have had SUCCESS training and EVEN hybridizing ZEBRAS!"

Hicho ndicho ninachosema, kwamba inawezekana ku domesticate Zebra isipokuwa taming yake lazima iwe tofauti na taming ya wanyama wengine, lackal of taming knowlegde for Zebra should not be taken as a failure that Zebras can not be domesticated, na huyo ndugu kaongezea kuwa Zebra imewezekana kuwa trained.

Mwanadamu ni Superior over other animals na kila animal anayo aina yake ya mafundisho.

Sasa usiseme kwamba Zebra hawezi kuwa domesticated sema watu hawana elimu ya kumfanya Zebra awe domestic animal. Suala ni ELIMU tu.
 
Hao ndio 666 Freemason,wao na rockefeller
Mdukuzi,
Nimekutana na mtu moja anaitwa Albert Rothschild katika Nyaraka za Sykes miaka mingi iliyopita.

Kuna makala niliandika kuhusu Rothschild na Freemason.

Makala hiyo chanzo chake ni kijana aliyekuwa akiniandikia sana kwa hili na lile.

Hapo chini nataka nimweleze Albert Rothschild kwa faida ya rafiki yangu Nyaluchi na kwa faida ya wasomaji kama nilivyokutananae katika kumbukumbu za Sykes.

Ally Sykes anamweleza Rothschild na hii ilikuwa mara tu baada ya Azimio la Arusha na yeye kwa kushindwa kufuata masharti ya kiongozi kutofanya biashara na kuwa na nyumba za kupangisha, Ally Sykes ilibidi aachishwe kazi serikalini kwa barua aliyoandikiwa na Bhoke Munanka.

Msikilize Ally Sykes:

‘’Nilikuwa tayari nimeshaingia katika aina nyingine za biashara.
Nilikuwa nawakilisha makampuni kadhaa ya kuuza madawa na vipuli kutoka Ulaya na Marekani.

Biashara hii mpya ikanifanya niwe nasafiri sana kwenda Ulaya na Marekani.
Katika hali kama hii nilipata marafiki wengi wenye nguvu na maadui pia wenye uwezo kama huo.

Katika marafiki zangu wenye nguvu alikuwa Albert Rothschild, mtu maarufu katika dunia ya mabenki.

Ngoja nieleze kisa kifupi ambacho Rothschild na mimi tulikutananacho kinachowahusu maofisa wa serikali ya Tanzania.

Rothschild alikuwa Myahudi na akiishi Paris.
Nilimfahamu Rothschild Nairobi kupitia Peter Colmore.

Tukawa marafiki na mwenzangu katika biashara.
Nilimtia Rothschild hima aje Tanzania kuangalia uwezekano wa kufungua biashara.

Ilikuwa siku moja wakati yuko Madagascar ndipo akanipigia simu kunifahamisha kuwa anakuja Dar es Salaam na nimpokee.

Mimi sikuwa nafahamu, kumbe Oscar Kambona, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje pia alikuwapo uwanja wa ndege kaja kumpokea Rothschild kama mgeni wa serikali.

Rothschild alikuwa ametua na ndege yake binafsi akiwa na wasaidizi wake.

Alipitishwa haraka sehemu ya VIP lakini Kambona alipigwa na butwaa pale Rothschild alipomwambia kuwa asingependa gari la serikali lililokuja kumchukua bali ataingia katika gari yangu na kufuatana na mimi mjini.

Hii ilikuwa kinyume cha itifaki lakini hakukubali akashikilia kupanda gari yangu.
Rothschild akapanda gari yangu akawa na mimi na mke wangu.

Nikafanya mazungumzo ya biashara na yeye kabla hajakutana na maofisa wa serikali ya Tanzania.

Haya yaliwaudhi sana watu fulani ndani ya serikali.

Mimi sikuona kosa lolote kwani sote tulikuwa tunahangaika katika kujenga nchi yetu na kumfanya mwekezaji ajihisi yuko katika mikono ya watu wema wa kuweza kutegemewa.

Kitu ambacho mimi sikuwa nakifahamu kwa wakati ule ni kuwa nilikuwa nachunguzwa na vyombo vya usalama.''

Nimeishi na watu waliokuwa karibu sana na mimi ambao ikisemwa ni Freemason lakini tofauti na nyakati hizi siku zilizopita Freemason watu wakiiogopa na kuhisi ni taasisi moja yenye usiri mkubwa wa kutisha.

Miaka hii karibuni hofu hii haipo tena na mkubwa wa Freemason hapa Tanzania, marehemu Andy Chande amekuwa akiandikwa kwenye magazeti na sura yake ikionyeshwa katika televisheni akieleza shughuli za taasisi hiyo tofauti na miaka iliyopita.
 
Mdukuzi,
Nimekutana na mtu moja anaitwa Albert Rothschild katika Nyaraka za Sykes miaka mingi iliyopita.

Kuna makala niliandika kuhusu Rothschild na Freemason.

Makala hiyo chanzo chake ni kijana aliyekuwa akiniandikia sana kwa hili na lile.

Hapo chini nataka nimweleze Albert Rothschild kwa faida ya rafiki yangu Nyaluchi na kwa faida ya wasomaji kama nilivyokutananae katika kumbukumbu za Sykes.

Ally Sykes anamweleza Rothschild na hii ilikuwa mara tu baada ya Azimio la Arusha na yeye kwa kushindwa kufuata masharti ya kiongozi kutofanya biashara na kuwa na nyumba za kupangisha, Ally Sykes ilibidi aachishwe kazi serikalini kwa barua aliyoandikiwa na Bhoke Munanka.

Msikilize Ally Sykes:

‘’Nilikuwa tayari nimeshaingia katika aina nyingine za biashara.
Nilikuwa nawakilisha makampuni kadhaa ya kuuza madawa na vipuli kutoka Ulaya na Marekani.

Biashara hii mpya ikanifanya niwe nasafiri sana kwenda Ulaya na Marekani.
Katika hali kama hii nilipata marafiki wengi wenye nguvu na maadui pia wenye uwezo kama huo.

Katika marafiki zangu wenye nguvu alikuwa Albert Rothschild, mtu maarufu katika dunia ya mabenki.

Ngoja nieleze kisa kifupi ambacho Rothschild na mimi tulikutananacho kinachowahusu maofisa wa serikali ya Tanzania.

Rothschild alikuwa Myahudi na akiishi Paris.
Nilimfahamu Rothschild Nairobi kupitia Peter Colmore.

Tukawa marafiki na mwenzangu katika biashara.
Nilimtia Rothschild hima aje Tanzania kuangalia uwezekano wa kufungua biashara.

Ilikuwa siku moja wakati yuko Madagascar ndipo akanipigia simu kunifahamisha kuwa anakuja Dar es Salaam na nimpokee.

Mimi sikuwa nafahamu, kumbe Oscar Kambona, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje pia alikuwapo uwanja wa ndege kaja kumpokea Rothschild kama mgeni wa serikali.

Rothschild alikuwa ametua na ndege yake binafsi akiwa na wasaidizi wake.

Alipitisshwa haraka sehemu ya VIP lakini Kambona alipigwa na butwaa pale Rothschild alipomwambia kuwa asingependa gari la serikali lililokuja kumchukua bali ataingia katika gari yangu na kufuatana na mimi mjini.

Hii ilikuwa kinyume cha itifaki lakini hakukubali akashikilia kupanda gari yangu.
Rothschild akapanda gari yangu akawa na mimi na mke wangu.

Nikafanya mazungumzo ya biashara na yeye kabla hajakutana na maofisa wa serikali ya Tanzania.
Haya yaliwaudhi sana watu fulani ndani ya serikali.

Mimi sikuona kosa lolote kwani sote tulikuwa tunahangaika katika kujenga nchi yetu na kumfanya mwekezaji ajihisi yuko katika mikono ya watu wema wa kuweza kutegemewa.

Kitu ambacho mimi sikuwa nakifahamu kwa wakati ule ni kuwa nilikuwa nachunguzwa na vyombo vya usalama.
Aisee kumbe aliwahi kuja Tanzania,hao kina Sykes ndio ilibidi wawe Rothschild wa Tanzania
 
Aisee kumbe aliwahi kuja Tanzania,hao kina Sykes ndio ilibidi wawe Rothschild wa Tanzania
Mdukuzi,
Shule niliyopata kwa Ally Sykes ni kubwa sana.
Nimejifunza mengi kutoka kwake.

Allah alimkirimu kupita kiasi.
Ally Sykes akiwatuma Wazungu apendavyo na wakimwita, ''Sir.''
 
Mdukuzi,
Shule niliyopata kwa Ally Sykes ni kubwa sana.
Nimejifunza mengi kutoka kwake.

Allah alimkirimu kupita kiasi.
Ally Sykes akiwatuma Wazungu apendavyo na wakimwita, ''Sir.''
Dah kweli alimkirimu
 
95% ya utajiri wa dunia???----- are you serious or kidding!!?[emoji33]---- kwa maana hiyo 5% iliyobaki ndio inamilikiwa na almost 7bn people??!!

Itakuwa kateleza kwenye hizo namba, nadhani ilitosha angesema wanamiliki sehemu kubwa ya utajiri wa dunia
 
Back
Top Bottom