1950 Machifu wa Kinyakyusa walienda Uingereza kudai uhuru!

1950 Machifu wa Kinyakyusa walienda Uingereza kudai uhuru!

Status
Not open for further replies.
Napenda kijua waliwezaje kusafiri hadi kwa mabeberu huko kudai uhuru?

Kuna waliowafadhili au walikuwa wana wenye kujiweza kifedha sana?
Wanyakyusa uwezo wa fedha walikuwa nao kwani wanalima kahawa, chai, ndizi na walikuwa wanakwenda WENELA Afrka Kusini kuchimba dhahabu, wao suti hawakuzianza wakati wa Magufuli.
 
Walikuwa na uwezo, Chifu ana ng'ombe wengi, akiuza wachache tu pamoja na michango ya eneo lake, tosha kabisa.
Ebu subiri kwanza,kwahiyo machifu waliuza ng'ombe ili wakate ticket za kupanda mwewe wa chuma.Vipi kuhusu mchongo wa Visa na transit ilikuwa wapi na wapi? Na nani aliwapokea London? Je hakukuwa na wazamiaji?

Hii story imeshaanza kunivutia ujue
 
Naona Chifu Hangaya hapa kapata mchongo, muda sio mrefu atatinga Mbeya kwenda kusimikwa kuwa chifu wa wanyakyusa.

Yule mama anapenda msereremko, ni mama wa kimichongo, urais wa msereremko na uchifu wa kimichongo.

Hivi toka lini mila zetu za kitanzania zikawa na chifu mwanamke?
Toka lini mtu mmoja akawa chifu wa makabila mbali mbali?
 
Ebu subiri kwanza,kwahiyo machifu waliuza ng'ombe ili wakate ticket za kupanda mwewe wa chuma.Vipi kuhusu mchongo wa Visa na transit ilikuwa wapi na wapi? Na nani aliwapokea London? Je hakukuwa na wazamiaji?
Hii story imeshaanza kunivutia ujue
Zamani VISA haikuwepo kwa Tanganyika ulikuwa mkoa wa Uingereza, pia pesa ya Tanganyika ndiyo hiyohiyo ya Uingereza kwa thamani ileile, kwa kifupi Uingereza ilikuwa sawa na kwenda Kigamboni.
 
View attachment 2093301

Nawakumbusha 1950's Machifu wa Kinyakyusa Walienda Uingereza Kudai Uhuru wa Nchi yao ya REPUBLIC OF SOUTHERN Highlands walikaa Mbele ni Kutoka Kushoto Chief Mwangobola...
Hii nchi tunadanganywa sana kwenye historia. Tunaambiwa ni Nyerere na Marealle ndiyo walioenda Ulaya kudai Uhuru kumbe hata ndugu zetu hawa wa Nyanda za Juu Kusini walipambana kudai Uhuru hadi huko Ulaya...kwa nn hatufundishwi darasani haya mambo?
 
Ok,sasa mipaka ya Republic of Southern Highlands ilikuwaje? ni ile ya kikoloni au walikuwa na ramani yao?
 
Hii nchi tunafanganywa sana kwenye historia. Tunaambiwa ni Nyerere tu na Marealle waleanda Ulaya kudai Uhuru kumbe hata ndugu zetu hawa wa Nyanda za Juu Kusini walipambana kudai Uhuru hadi huko Ulaya...kwa nn hatufundishwi darasanj haya mambo?

Ufundishwe UKWELI ili uujue halafu sifa uzipunguze kwa Nyerere?? 🤣

Sio katiba tu inatakiwa iandikwe upya bali hata Historia yetu.
 
View attachment 2093301

Nawakumbusha 1950's Machifu wa Kinyakyusa Walienda Uingereza Kudai Uhuru wa Nchi yao ya REPUBLIC OF SOUTHERN Highlands walikaa Mbele ni Kutoka Kushoto Chief Mwangobola...
Kumbe hapo ndipo walipopata misamiati mipya ya Kinyakyusa kama vile 'injinga, ibaisko, isipuni n.k."

Safi sana.
 
Ok,sasa mipaka ya Republic of Southern Highlands ilikuwaje? ni ile ya kikoloni au walikuwa na ramani yao?
Nyanda za juu Kusini zina watu wenye utamaduni unsofanana.

Hivyobasi unakuta kwa mfano kabila la wanyakyusa lipo Tanganyika na Nyasaland hadi Zambia.

Hata kabila ka wanyiha Mbozi linaingia hadi Zambia.

Kabila la wandali(kimsingi wanyakyusa) waki Tanganyika, Nyasaland na Zambia(Northern Rhidesia).

Hivyo unaweza kuona eneo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom