1950 Machifu wa Kinyakyusa walienda Uingereza kudai uhuru!

Status
Not open for further replies.
Chifu mkuu Hangaya alisema pelekeni majina yenu ili msimikwe uchifu, kazi kwenu ajira ndiyo hizo mlizokuwa mkizilalamikia kuzikosa.
😕😕😕wakasimikwe tu waanze kudaiwa kodi uyu karl peter wa kike ana mbinu balaa
 
Sikusema WENELA ni mji, ndege ya kampuni hiyo ilikuwa ikienda Mbeya kuwachukua na kuwarudisha wachimba migodi.
 
Ni kweli , babu yangu alikuwa chief, na mpaka anafariki alipewa heshima zote na wananchi.
 
Mwaka 1948 watemi wa Kisukuma walienda Uingereza kudai uhuru wao wa nchi yao iliyokuwa nchi ya NYANZA wakiongozwa na mtemi Masanja,Kidaha na Ihangilo, ni vizuri nam nikakumbusha make Chui dume asije akasahau nasi tulikuwa wapambaji sio mapoyoyo
 
Wagogo watan zangu walikuwa na uongoz imara sana Chini ya MAZENGO, na uongozi wao ulikuwa sio wa mapigano lakin walikuwa imara Sana hata Chief Mkwawa alikuwa anawaheshimu na kuwaogopa Sana hadi wakapeana Wanawake wa kuoa.
 
Kumbe na Wanyakyusa walienda hadi UK?? Kweli kuna makabila yenye asiliya aggressiveness nasikia pia Cheif Marialle toka Kilimanjaro naye alienda UN. Swali langu tu la kijinga

1. Ni nani aliwagharamia safari hizi ukizingatia zilikuwa ni safari za kupingana na watawala wao
2. Education level yao ilikuwa ya kiwango gani kuwawezesha kuwasilisha mada yao in an understandable manner
3. Kwa nini hii safari ya hawa machifu wa Kinyakyusa haijazungumzwa sana kwenye vitabu vya historia ya nchi hii
 
Wagogo watan zangu walikuwa na uongoz imara sana Chini ya MAZENGO, na uongozi wao ulikuwa sio wa mapigano lakin walikuwa imara Sana hata Chief Mkwawa alikuwa anawaheshimu na kuwaogopa Sana hadi wakapeana Wanawake wa kuoa.
Hawa hawa kina matonya?
 
Mkuu historia wanasiasa huwa wanaifanya kuwa ni siasa ya kujitukuza wenyewe.
Hivi karibuni tu lilitoka agizo kwa Wizara ya Elimu, angizo ambalo limesitishwa, la ku rewrite history ili kuwa favour current politicians.
Unyakyusa watu walikuwa aggressive sana kudai haki yao.
Ni watu wachache wamesoma kuwa wanyakyusa walipigana na wajerumani in 1897.
Tena wanyakyusa waliungana na ndugu zao wakinga kupambana na wajerumani.
Kwa miaka mingi wanyakyusa na waking wamekuwa wakiishi karibu, ingawaje wakinga wanaoa unyakyusanai lakini wanyakyusa mara nyingi hawaoi wakinga(wanasema siyo wasafi sana, kutokana na kutokuwa na maji ya mito kwa wingi kule juu milimani.)

Wajerumani walishangaa kuwa style wanyakyusa/wakinga waliyopigana nyo ni kama ile ya wahehe, 1894, ingawaje walishindwa kutokana na kutokuwa na bunduki.

1. Nani aligharamia safari: wanyakyusa miaka hiyo , toka 1920-30 bado walikuwa na mali ningi sana, kuuza ng'ombe haikuwa shida
2. Education: kinachohitajika hapo ilikuwa tu communication, kujieleza na kueleweka, hata walipofika wakloni communication ilikuwepo
3. Kwa nini hii safari haijazungumzwa: nimetangulia kueleza hapo juu, na kuna mdau Huihui2 said: ameeleza vizuri mtandao wa safari za watu wa Nyanda za Juu kusini kusafiri Kusini mwa Arika.
Wenyewe wakiita Kujohni(Johannesburg).
Mjomba wangu amekaa sana Zimbabwe miaka hiyo na aliongelea sana miji ya Broken Hill na Wankie.
 
Mwaka 1948 watemi wa Kisukuma walienda Uingereza kudai uhuru wao wa nchi yao iliyokuwa nchi ya NYANZA wakiongozwa na mtemi Masanja,Kidaha na Ihangilo, ni vizuri nam nikakumbusha make Chui dume asije akasahau nasi tulikuwa wapambaji sio mapoyoyo
Mwaka uliofuata watemi wa Kigogo nao wakaenda kudai wakiongozwa na chief Le Mutuz...
 

Kumbe zamani miaka ya mwanzo kabisa ya karne ya ishirini (1900) watu walianza kwenda South Africa kitambo kabla ya zama za mabaharia wa enzi hizi miaka ya 1994 miaka ya South Africa chini ya Nelson Mandela ya wazamiaji na waruka senyenge.
source : big light worldwide

Shukrani Jamiiforums na wanaJF kwa kutuelimisha kupitia uzi huu wa utani aliotupia mwana JF mwenzetu masopakyindi
 
Lakini jamaa ni mkali amechukua picha mtandaoni akawabatiza na majina kabisa akawapa majina ya Kinyakyusa...
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…