2010 BMW 320i vs Mercedes Benz C Class

2010 BMW 320i vs Mercedes Benz C Class

C Class ni entry level Mercedes Benz Sedan. E class ndio full executive Sedan. Cha ajabu Wajapan wanakimbizwa mpaka na C Class! Hapo ndio utajua kuna Wajapan na Germany machines 😂🙌🏿
Wanachanganya kweli.. C class ni kama Premio tuu..
E class ni mid size..
Full size ni S Class.. Hiyo ndio Mercedes yenyewe..
Hata kwenye production.. S Class ndio ilikuwepo mwanzo kabla hawajaleta E na C class..!
 
Kuna mmoja kasema hakuna benz ( it means S Class included) inaifikia Crown kwa comfortability nikawa shocked
 
Najua, nilichomaanisha ni kwamba kununua Bimmer au Mercedes ambayo karibia kila kitu kimeshachoka itakuchukuwa gharama kubwa sana mpaka kuja kuiweka sawa na kuenjoy Bimmer ambapo hiyo gharama ni bora utafute gari za kawaida ( ambazo hazing majina) lkn mpya kidogo ambapo utaitumia kwa muda mrefu zaidi, kununua Mercedes au Bimmer iliyokwishachoka ni kupoteza hela na siyo clever kwani aidha utaipaki kwa kushindwa kuirepair au itakubidi utafute gari nyingine ya pembeni kama toyota ya kutumia kila siku, sasa ukijumlisha hizo stress zote ni bora ujinyime ununue gari ( siyo brand name lkn nzuri) ya miaka max 5 lkn utaishi nayo bila ya stress, …

Gari ya 2010 bado mpya sana na unaponunua gari used ya japan unaangalia milage imetembea umbali gani most zinakua chini ya 100k KMs hiyo bado mbichi sana kwa bongo gari hadi ichoke iwe umetembea KM zaidi ya 2M , crown zanyewe nyingi ni za 2004 hadi 2007 ist ni za 2003 na bado inauzwa 14M hiyo Gari ya 2010 ni mali mpya sana na mbichi na unakuta bei ina range 16- 20M
 
Bro number’s don’t lie

Go for Mercie

Good Fuel economy,performance ni ya kawaida kiukweli japo ina top 260km/hr labda usichukue hizi cc1780

Comfotability inategemea una compare na gari ipi lkn haiifiki kwa gari kama crown.

All in all you buy mercides you buy pride
Kila utapoonekana wanajua una pesa[emoji28]

Maintenance ni expensive kiasi

Hizi C200 kompressor hazina magonjwa mengi ndo maana hutasikia kelele humu za wamiliki wa Benz

Ni gari reliable sana na ngumu mno.umeme kiasi

ONYO:kama hukai mjini kene barabara na mafundi wa uhakika achana nayo mkuu
Kadhalika tupambanie kuondoa matuta njiani na kuweka speed cameras kuyalinda magari
 
Gari ya 2010 bado mpya sana na unaponunua gari used ya japan unaangalia milage imetembea umbali gani most zinakua chini ya 100k KMs hiyo bado mbichi sana kwa bongo gari hadi ichoke iwe umetembea KM zaidi ya 2M , crown zanyewe nyingi ni za 2004 hadi 2007 ist ni za 2003 na bado inauzwa 14M hiyo Gari ya 2010 ni mali mpya sana na mbichi na unakuta bei ina range 16- 20M

Siyo kweli gari ya miaka 10 itembee km 100 000 tu tena in a developed country? Kama zipo ni chache sana na zitanunuliwa na Wajapani wenyewe kwani wanazihitaji pia, hizo zinazokuja Bongo zimeshachezewa tayari na km siyo za kweli, kwani BMW ya km laki moja tu haiwezi kuuzwa milioni 14.

Hata wewe unaweza kupiga hesabu ya kinadharia tu kwa Bongo, tuseme unaishi Mbezi beach unafanya kazi mjini posta kwenda kazini na kurudi nyumbani ni km 20*2=40/siku *siku 240/ mwaka = 9600 km * 10 miaka= 96 000 km/ miaka 10.

Sasa hiyo ni kwamba unaitumia gari kwenda kazini na kurudi basi, na j’tatu - Ijumaa, weekend inapaki na sijaweka safari za mikoani, na utumie gari hivyo kwa miaka 10 ndiyo uweze kupata hiyo km 100 000 unayoiongelea, unafikiri wangapi wanafwata hivyo? Tena huko kulikoendelea na ma highway yao gari zinatembea sana, huo ni mfano tu!
 
Nimeongelea comfortability tu sio prestige wala durability,mjapani yuko vizuri kwenye comfortability amini usiamini,ukipanda VX V 8 lile la samia ni kama uko peponi,hakuna gari ya mzungu inaifikia kwa comfortability
Haha.

Hiyo ya Samia si ipo moja nchi nzima.

Ushapanda gari zote za mzungu duniani mpaka ujue zilivyo kulinganisha na ya huyo mama samia?
 
Kuna mmoja kasema hakuna benz ( it means S Class included) inaifikia Crown kwa comfortability nikawa shocked
Huko kwa serikali ya CCM huwezi kuta Crown kwenye list ya state cars.

Its either VXR, S Class, 7 Series sometimes Nissan Patrol.

Nakuhakikishia hakuna serikali duniani yenye Toyota Crown kama state cars au wanazoendea kuwachukua marais wenzao.
 
Kuna jamaa alisema Crown ndio gari inayotumika na mfalme wa Japan 😀. Nikajiuliza kwa safety features zipi?
 
Japan gari ya Waziri mkuu ni crown
Acha uongo mzee ni Toyota Century. Soma hapa chini kidogo uelimike

In 2008, the Japanese government changed the official car to the Lexus LS. In addition to having the same level of luxury and safety as the Toyota Century, the new Lexus LS had lower fuel consumptions and lower CO2 emissions.[4]

In 2020, the Japanese government picked the newest version Toyota Century as the Prime Minister's Official Car instead of the new Lexus LS.[4][3]
 
Kwa mwaka 2010 BMW ya kuchukua ni 323i au 335i(kama ana pesa ya wese na anataka kunyanyasa watu barabarani).

The rest atakuja kulalamikia watu humu ndani.

323i ya 2010 ina Cc2500 ikiwa na engine ya N52B25 wakati 335i ya 2010 ina Cc3000 N55 with twin scroll turbo...

The rest ndio zina engine kama N43, N45, N53, N54 ambazo zote ni engine za majaribio na zilifeli...
Mimi naona watu wanaongea tu mimi na bmw 2010 cc 2000 ya 320I ? Nimenunua 2020 zaid ya kumwaga oil ,kubadili brake pad aijawai nisumbua nilinunua ikiwa na km 38000 mpaka sasa nakaribia 80000 na ndio gari yangu kwa kilakitu na before nilikuwa na crown but ilinisumbua sana kwenye ac ilikuwa inauwa compresa but for bmw series sijawai juta

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom