2013 kurudi nyuma ukipata division one watu wanakushangaa ila siku hizi ukiikosa watu wanakushangaa zaidi!

Uko sahihi mi ni mwalimu nayaona haya
 
Kama shule ina division 3 A level mwaka huu wao ni vilaza wa kutupwa.

🤣🤣🤣🚮🚮🚮. Miaka hii usipofaulu ww ni kilaza kabisa 😝😝😝
 
Pitia review Tena pole sana kama ulikuwa mmoja wa waliokuwa wanafeli kupata 30 wastani
 
Pitia review Tena pole sana kama ulikuwa mmoja wa waliokuwa wanafeli kupata 30 wastani
Sijakuelewa hoja yako, nimesema serikali imeshusha passmark za form two kutoka wastani wa 30 mpaka D mbili au C moja ,nikasema kwamba kwa madent wa sasa ingerudishwa ile average ya 30 wachache wangetoboa
 
Hata zamani mitihani ilikuwa rahisi sana sema mlikuwa wengi vilaza na mnasoma kwenye mazingira magumu sana imagine miaka Hiyo mtu anafeli kupata wastani wa 30 ili kivuka form two
Saizi wamerahisha zaidi mwanafunzi anatakiwa kupata division 4 ya 33 ili kwenda form 3. Hiyo ni sawa na D 2 tuu of which zamani ungepata lakini bila wastani wa 30 zisingekusaidia.

Nakubaliana na wote waliosema saizi teknolojia inasaidia sana wanafunzi kufaulu. Zamani ulikua unatumia energy kubwa sana kama hukuelewa darasani wakati siku hizi unaingia youtube na kukutana na maelezo ya kutosha.
 
Elimu ya siku hizi kanyaboya na watoto wamekuwa kanyaboya.

Sector zinawatendaji wasiojielewa. Dharau zimekithiri
 
Je hapo twaboresha au twaharibu elimu yetu?
 
Kina fulani walimpinga sana Ndalichako ila yale ndiyo yalikuwa matokeo sahihi kwa taifa letu, tatizo lilikuwa siasa wakaona wayaweke sawa.
Mzanzibar kaingia pale kwa sasa kila mtu anafaulu
 
Kwanza kupangilia kwa Division kwa Madarasa ya chini ya Form Four ni upumbavu.
Waweke Wastani kama mtu hafikishi akalime
 

Hahahahaa ni hatari sana ,zamani kweli ukipata Div I ,Kijiji kizima wanakujua na hata matokeo ya darasa la 7 ukifaulu ni Bonge la heshima....Shule zetu zamani Div I point 7(form iv) au Div I Point 3(Form vi) ilikuwa either hakuna au ni moja tu lakini sasa unashangaa eti darasa karibia wote wamepiga One ya 7 😀 😀 😀 😀.
 
Siku hizi watu watakushangaa Ukikosa one utaonekana kiazi ajabu ,ukipata division 2 hata ya 10 unaonekana umefeli.
Waliokua wanasahisha zamani sio wanasahisha sasa hivi alafu kuna Mambo yanabadirika it's all about timing kuna Mambo ulifundishwa 2013 kushuka chini sasa hivi utakuta hawafundishwi

Alafu mitihani majibu wanalishwa sasa hapo kufeli ufeli wewe tu tofauti na zamani watu walikua wanahaha kuzisaka possible paper za maswali na wanayafanya kabla wanapitia past papers sikuhizi wanerelax tu

Siku hizi imekua tofauti wanalishwa majibu ya mitihani km yalivyo kabla ya mitihani sasa ukifeli hapo wewe ni lofa kiwango cha SGR
 
Hilo mimi nakukatalia. Ukichukua mitihani ya zamani ukampa mwanafunzi wa Sasa, nakuhakikishia utalia. Mitihani ya huko nyuma ilikuwa balaa na ndiyo maan hata walimu waliokuwa wanapatikana ingawa walikuwa wa daraja la chini lakini walikuwa hatari na nusu ukilinga Isha na product ya walimu wa sasa wengi wao ni tia maji tia chumvi ( Ila heshima iende kwao wote). Fikiria wale wa walimu wa darasa la 7 waliotufundisha jinsi walikvyokuwa wanapiga kipindi balaa lakini leo ukichukua mwanafunzi aliemaliza la 7 ukimwambia afundishe Primary utalia kwa uchungu.
 
2013 ni zamani!? Aisee, kweli Jf ni Kokoro....tumetofautiana rika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…