2022 Haya ndio makabila yanaongoza kwa maendeleo

2022 Haya ndio makabila yanaongoza kwa maendeleo

Hakuna kabila la wahindi ama waarabu, wao wana makabila yao ya huko walikotoka ndio maana hawamo kwenye list, tunaweza kuwaita jamii ya waarabu ama wahindi.

Uzi huu ni kwajili ya makabila yenye asili ya hapa kwetu

Watu wana maduka kariakoo kwanini wasilete makontena ? Labda ulikuwa bandari ya kigoma huko 😂
Unaumwa wew ndo maana nikamwambia kwamba izo jamii mbona hujataja makabila yao? Unakurupuka tu! Kuwa 🤓 kama ndo uwezo wako umefikia hapo basi tunajua jamii za waarabu ,wahindi na wachina ndo wanaingiza containers nyingi nyie wachuuzi ndo mmebaki kuwa middle men ..Kaa kwa kutulia😂😂😂😂Ushamba unakusumbua ..bandari pale TZDL
 
Endeleeni kukaririshana upumbavu miaka yote kuja kushtuka nyote mtakuwa watumwa wawasukuma kwa uzumbukuku wenu.
Hapo Mwanza kwenyewe wanao run huo mji ni Wakurya, Wasukuma wapo porini na mang'ombe yao tu na kuzaliana kama panya
 
Hapo Mwanza kwenyewe wanao run huo mji ni Wakurya, Wasukuma wapo porini na mang'ombe yao tu na kuzaliana kama panya
Ila watu mnadharau sana aese! Yaani ukienda Libeti pale ukahesabu maduka ya wakurya na wasukuma utasema wakurya ni wengi? Hata gorofa nyingi hapo mwanza ni za wasukuma Mipa,Nyerere roadplaza,mongo,rock beach, kishimba apartment bugando hill,Ekakriff,Holmand,pigeon,The farmshotel, Isamilo hotel, mata wa capri point vijana wa Geita wachimba dhahabu wamejenga mahekalu huko n! Majengo yanayimilikiwa na wakurya hapo mwanza kama ni mengi ukilinganisha na wasukuma!
Tatizo nyingi vikabila vidogo mnainfiriolity complex na wasukuma hawanaga kelele! Yaani wakurya wanawilaya moja tu ambayo haina hadhi hata nusu ya kahama ndo wawazidi wasukuma!?
Mna chuki sana nyie! Vijana wa kisukuma wanapesa sana ukienda stendi buzuruga ukiangalia wamiliki wengi wa mabasi ni wasukuma fikoshi,isamilo,sabuni,batco,malangwa,coaster za kwenda Geita ,kahama shinyanga ,misungwi asilimia kubwa ni za wasukuma! Chuki ndo inawasumbua pia hata ukiangalia kwa hali tu ya kawaida wasukuma wa bariadi wanyantuzu utawalinganishaje na wakurya hata kiutafutaji?
Sema wakurya wanawatu wao identity kama Gachuma na kitana wazee wa zamani!
Lakini akina kishimba, Njiwa pori wote hao ni matajiri wakubwa ila hawana kelele!
 
Yule inasemekana ni mtu wa kigoma mama yake msukuma ila kakulia Geita na anafedha nyingi sana!
Ndo mwekezaji mzawa wa mgodi wa Nyanzaga!

Duuu kumbe Nyanzaga ni ya Baraka? Basi akina gachuma sio ligi zake tena ashawaacha
 
Ukweli wasukuma wako mbali kwanza ukumbuke peke yao wako kama mikoa mitano ukiacha mikoa mingine walitosambaa sasa ukiweka kwa asilimia jamaa wanautajiri mzuri tu na nadhani ni kabila ambao ukiacha mifugo wanamiliki ardhi kubwa anzia moro, lindi, mtwara wanamiliki ardhi kubwa sana
 
Gac
Duuu kumbe Nyanzaga ni ya Baraka? Basi akina gachuma sio ligi zake tena ashawaacha
Gachuma hata kishimba tu hamfii! Kwanza Mwanza hotel mpangaji tu! Ukitaka kujua shughuli za kishimba kwenye industry ya real estate nenda dodoma! Hapo mwanza pia kaanza kuwekeza apartment!
Ila sema wasukuma hawana showoff!
 
Ukweli wasukuma wako mbali kwanza ukumbuke peke yao wako kama mikoa mitano ukiacha mikoa mingine walitosambaa sasa ukiweka kwa asilimia jamaa wanautajiri mzuri tu na nadhani ni kabila ambao ukiacha mifugo wanamiliki ardhi kubwa anzia moro, lindi, mtwara wanamiliki ardhi kubwa sana
Nikwambie ukitaka kujau hawa mabwana hawana kelele nenda CRDB kahama ukaone magunia ya fedha yanaingia bank!
Lakini wenzangu na mimi akiotea milioni kumi kila mtu atajua!
Mtu yeyote mtafutaji nchi hii hawezi kusema msukuma hana hela!
Wateja wa bidhaa za hao matajiri wa hapo mwanza majority ni wasukuma halafu mtu anakuja kusema hawana hela!
Flight nyingi za ndege tanzania zinahusisha jiji Mwanza ambapo watu wa simiyu,shinganga,geita na musoma hushukia hapo je katika hao wengi ni akina nani?
 
Nikwambie ukitaka kujau hawa mabwana hawana kelele nenda CRDB kahama ukaone magunia ya fedha yanaingia bank!
Lamini wenzangu na mimi akiotea milioni kumi kila mtu atajua!
Mtu yeyote mtafutaji nchi hii hawezi kusema msukuma hana hela!
Wateja wa bidhaa za hao matajiri wa hapo mwanza majority ni wasukuma halafu mtu anakuja kusema hawana hela!
Flight nyingi za ndege tanzania zinahusisha jiji Mwanza ambapo watu wa simiyu,shinganga,geita na musoma hushukia hapo je katika hao wengi ni akina nani?

Msukuma anahukumiwa kwa lafudhi tu lakini ni mtu ambae anapambana na alipomsukuma hata njaa inakimbia kabisa kabisa
 
Zingatio 1: Simo katika kabila lolote kwenye hii orodha, sina mgongano wa kimaslahi wa kunifanya kupendelea ama kuchukia makabila niliyotaja.

zingatio 2: kuwa ndani ya haya makabila haimaanishi watu wote wa kabila hilo wafanikiwa, hata idadi ya wenye mafanikio makubwa ndani ya haya makabila bado ni ndogo, usibweteke kujidanganya umefanikiwa kisa umo ndani ya haya makabila, Tafuta chako!!

Muhimu 3: kama kabila halipo haimaanishi halina watu waliofanikiwa, kuna watu wa makabila ambayo hayamo humu wana mafanikio makubwa kuzidi watu kibao wa makabila yaliyowekwa hapa.

Muhimu 4: hakuna muhuri wa kudumu wa umasikini ama maendeleo kwenye haya makabila, kuna kupanda na kushuka, kuna makabila yalikuwa chini zamani ila kwa sasa yanakuja kwa spidi ya radi, mengine yameshuka.

1. Wachaga -

🎯Biashara
🎯Elimu
🎯Siasa
🎯Kubebana
🎯Kuendeleza kwao

Kibiashara kabila hili wapo katika nafasi nzuri, wamekuwa pioneers wakubwa katika kuanzisha na kuziendeleza biashara kibao, mifano ya biashara maarufu kuna kampuni ya ndege za Precision Airways, Hamidu city sehemu ya makazi yenye nyumba elf 2 za kisasa, hotel kali za Arusha / Dar, n.k. Icon kubwa katika kabila hili ni Marehemu Mzee Reginald Mengi, aliweza kuingia ndani ya orodha ya top 10 ya matajiri wa hapa nchini akiwa ni mtanzania pekee mwenye asili ya makabila ya hapa kwetu, kwenye elimu nako hakuwa nyuma, alikuwa muhasibu wa kwanza nchini kuthibitishwa na bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu za fedha (CPA), aliweza kutumikia sehemu mbali mbali zilizompa mishahara minono lakini aliamua kugeukia ujasiriamali uliompa utajiri mkubwa.

Kielimu wamejitosheleza, mkoa wanaotokea unaongoza kwa kuwa na shule nyingi tangu zamani hadi sasa, kupata elimu ni kitu rahisi, maofisini katika kila watumishi 10 imeshazoeleka kumkuta mchaga walau mmoja na hii idadi imepunguzwa sana, miaka ya nyuma maofisin kulijaa wachaga na makabila machache yasiyozidi matatu yaliyokuwa na wasomi hususan wahaya. sikuhizi hali ni tofauti, elimu imesambaa kwenye makabila mengi na mbaya zaidi wasomi ni wengi kuzidi ajira kiasi kwamba nafasi 1 inagombaniwa na watu 500, pia wizara ndio inasimamia zoezi la ajira sio kama zamani kila shirika / taasisi ilijisiamia kwenye kuajiri, bosi akiwa mchaga anarundika ndugu zake. Uzuri ni kwamba wachaga hawategemei ajira pekee, huwa kuna mlango mwengine wa kufanya biashara, inakuwa rahisi kwao kuanza biashara maana wana utamaduni wa kubebana kwa kuchangiana mitaji na kwavile kunakuwa na ndugu wanaofanya biashara huwa inakuwa rahisi kushikwa mkono kupewa ramani, ushauri na connections za biashara.

Kisiasa wapo active na sijaona wa kuwakaraibia, vyama vikuu vya upinzani vilivhowahi kuleta upinzani mkali kuanzia Tlp, Nccr na Chadema vimeanzia huko kwao, wamo pia kwenye chama kikuu cha ccm na influence yao ya political power si haba.

Kubebana na kusaidiana ni silaha kubwa sana katika maendeleo yao, mmoja akitoboa anasaidia wengine.

Hawasahau kuendeleza walikotoka, wanajenga na kuboresha makwao huko kwenye asili yao, hata ikitokea misiba au wakirudi kusalimia huwa hapati shida kwenye makazi. Kuna nyumba ya Marehemu mzee Mengi aliijenga kwao ni mfano wa mansion za kisasa.

kila mwisho wa mwaka kabila zima huwa wanarudi makwao kwa pamoja, ni utamaduni wa kipekee, kukutana huku husaidia ndugu waliotawanyika kukutana, ndugu kuchangiana mitaji, ndugu na majirani kujuliana hali, kupanga mikakati, kutambulisha watoto kwa ndugu, n.k. kurudi inakuwa rahisi maana makazi ya vijijini wanayaboresha.

mkoa wao ni wa pili kwa kiwango kidogo cha umasikini...

Niishie hapa maana ntaanza kuonekana nawapendelea lakini kila nilichoorodhesha hapa ni facts.


Wakinga -

🎯Biashara
🎯Kubebana

Kama ilivyo kwa wachaga, nao hawa kubebana na kusaidiana ni silaha kubwa sana katika maendeleo yao, idadi yao ni ndogo hawavuki milioni lakini wanabebana sana pengine kuzidi hata wachaga.

Hawa shabaha yao kuu ya mafanukio wameilenga sehemu moja kwenye biashara, kwenye elimu bado wanajikongoja lakini main focus wameweka kwenye biashara na kiukweli biashara zimebadili maisha yao.

Nchini China katika jiji la Ghuangzhou wakinga ndio watanzania waliojazana zaidi mpaka wana mitaa yao, ni jiji kubwa la kibiashara lenye viwanda vingi na kuna bandari kubwa ya kusafirisha mizigo, wakinga wa huko huwa wanashughulika na kutafuta bidhaa nzuri viwandani kisha wanasafirisha kwa meli ziwafikie ndugu zao wa huku, hata ikitokea kuna bidhaa kama kiatu kinauzwa sana hapa nchini basi kitasafirishwa kwa ndege kiwafikie ndugu zao wa huko wakipeleka kwa wachina watengeneze vingi na kuvisafirisha haraka vifike hapa kwetu wapige pesa, wana kampuni maarufu ya kusafirisha bidhaa kutoka China hadi hapa kwetu inaitwa Mapembelo Cargo, hilo neno Mapembelo ni salamu yao ya kilugha.

Silaha yao kubwa ni kuuza kwa bei ndogo, ndugu zao wa huko China wanahusika sana hapa kwa kupeana connection za machimbo ya huko China yenye bei za chini, kampuni ya kusfirisha bidhaa zao nayo inapunguza gharama, pia na wao hawanaga tamaa za faida kubwa nayo hii inasaidia sana gharama kuwa ndogo. hii mbinu ya kuuza kwa bei ndogo ndio iliwafanya hata wapemba na wachaga kupungua pale Kariakoo, ni ngumu kushindana na mtu anaeuza bidhaa hio hio au yenye ubora zaidi kwa bei chee, ni ngumu sana!


Mwamko wa biashara kwa wakinga wengi ulianza miaka ya 2000 lakini ndani ya muda mfupi maendeleo yao ni mithiri ya spidi ya radi.

Masoko waliyoteka ni soko la kuu la Kariakoo pamoja na mikoa ya nyanda za juu kusini. Kwa Dar wamejaa kwenye soko la Kariakoo ambalo ni soko mama na kubwa kuzidi yote nchini, wafanyabiashara wengi wenye maduka Dar, mikoani na wale wa nchi za Malawi, Zambia, Congo, Rwanda na Burundi wanajumua mizigo yao katika soko hili. Kariakoo si ajabu kwenye maduka 10 kuyakuta 6 yana wakinga, soko hili hapo zamani walijaa wachaga na wapemba hapa lakini kwa sasa hali ni tofauti, wakinga wamejazana na ndio wanaongoza kwa uwakilishi. Pia wanamiliki maghorofa mengi hapo Kariakoo.


Ukiachana na kariakoo, wameweza kuuteka kibiashara ukanda wa nyanda za juu kusini kwenye miji mikubwa ya mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma..

Wapemba -

🎯Biashara
🎯Kubebana

Hawa nao kubebana na kusaidiana ni silaha kubwa sana katika maendeleo yao, kwa mara nyingine tunaona jinsi umoja ulivyo na nguvu

Kwenye swala la elimu huko Pemba wapo chini sana ni mkoa unashika namba ya mwisho miaka nenda rudi lakini kwenye biashara wapo mbali sana, mafanikio waliyonayo ni kuzidi hata ya wasomi wengi wanaopokea mishahara mirefu, connection walizonazo na ndugu zao waliojazana nchi za nje nyingi zinawabeba pia.


Wahaya -

🎯Elimu

katika swala la akili za darasani ni kama walizidishiwa 😂, mkoani kwao mazingira ya elimu yapo chini lakini bado wanafaulu, ilifikia kipindi serikali iliongeza alama za ufaulu kwa mkoa wa kagera maana watu walikuwa wanafaulu kama vile wanakunywa maji.


elimu inawabeba na inawapa sifa za kuajiriwa sehemu nyingi,


maofisini katika kila watumishi 10 si ajabu utamkuta mhaya angalau mmoja na hii idadi imepunguzwa sana, miaka ya nyuma ilishazoeleka maofisin kujaa wahaya na makabila machache yaliyokuwa na wasomi kama wachaga. Sikuhizi uwanja umebadilika kwasababu elimu imesambaa kuna shule nyingi za serikali + private, tuisheni, upatikanaji rahisi wa vitabu, ufaulu umekuwa mkubwa, n.k. hali hii imefanya kuwe na wasomi kibao karibu kila kabila, maofisini hata wamasai wapo. pia kwa sasa wizara ndio inasimamia zoezi la ajira sio kama zamani bosi wa shirika unamkuta ni mhaya au mchaga anarundika wenzake. ubaya ni kwamba wahaya wengi hawana mlango wa pili (plan b), wana uwezo mkubwa darasani wa kuwafanya wapate sifa za kujirika (zamani ilikuwa ni uhakika wa ajira) lakini sasa nje yah apo kujiongeza hata kwenye biashara ni wazito.



Kubebana bado wapo kiwango cha chini, naweza kusema kubebana kupo sana makabila ya kibiashara kwenye kuchangiana mitaji lakini huku kwengine sio kivile.



Wasukuma -

🎯Elimu


Wasukuma ndio kabila lenye watu wengi kwenye hii nchi, wapo takribani milioni 12, idadi yao ni kubwa sana na ilibidi iwabebe lakini tatizo lao kubwa ni kwamba wana ushirikiano mdogo, laiti wasukuma wangekuwa na muungano hakuna kabila lingewafikia hata nusu ya maenddeleo yao.

any way kwa wasukuma bado idadi yao kubwa inawabeba, katika hii idadi kuna koo zimeelimika na kuliweka kabila kwenye ramani,


Pia hujishughulisha na shughuli za uchumbaji mdogo wa dhahabu na kilimo japo ni kiwango cha kawaida.



Kuzaliana kwa sana kumekuwa ni tatizo kubwa.
Wasukuma ni biashara na kubebana elimu
 
Wasukuma ni biashara na kubebana elimu
Tatizo la wasukuma ni ushirikina sana, wanavyohamia sehemu wana waganga wao kabisa wamebeba matunguri, pia maendeleo inakuwa changamoto kwasababu wanazaliana sana, mama moja watoto nane.. Kwenye biashara nako wananishangaza, kuna sehemu niliwahi kwenda wafanyabiashara huko geita wamefunga maduka kisa kuna mgeni kafungua duka wanashinikiza mgeni awape kreti moja lasivyo hawafungui maduka
 
Hapa mwamba kuna kitu hujakitaja! Ndicho kinawabeba sana!
Uchawi ?

Kama ni ndio basi kwanini hata waganga hali zao ni duni ? Kwanini makabila yanayosifika kwa uchawi hali zao ni duni ?

uchawi una vigogo wake hapa Tz na inajulikana wazi kabisa vinara wa hizi teknolojia wapo Gambooshi, Ukerewe, Bagamoyo, Pangani, Sumbawanga, Kigoma, Shinyanga, Lindi, Kwanini hawana maendeleo kama wanaweza kuroga biashara ziwape maendeleo ?
 
Hili swala naomba mlifute litakuja kuwakosti siku moja
 
Hakuna kabila la wahindi ama waarabu, wao wana makabila yao ya huko walikotoka ndio maana hawamo kwenye list, tunaweza kuwaita jamii ya waarabu ama wahindi.

Uzi huu ni kwajili ya makabila yenye asili ya hapa kwetu

Watu wana maduka kariakoo kwanini wasilete makontena ? Labda ulikuwa bandari ya kigoma huko [emoji23]
Mimi niko niliachia hapo ulipoanza kuwashusha wahaya na elimu zao...nikajua kabisa hauna kitu kichwani..

Hao wakinga na wapemba walivyo wachache ndo wakulinganisha na wahaya na wasukuma kweli...

Yes naweza kukubali kuwa wahaya hakuna wale matajiri extreme ( ingawa walikuwepo wakina Mfuruki aliyekuwa top ten ya matajiri na yule karamagi), lakini sidhani kuna kabila lenye middle class kama wahaya nchi hii...

Siku hiz mnawashusha kwa sababu ya mkoa wa kagera kuanguka kiuchumi na kuonekana maskini mbele ya serikali lakin reality maisha ya mtu mmoja huko kagera hasa uhayani na wale wahaya waliopo nje ya mkoa ni bora kuliko jamii nyingi nchi hii...

Yes wamekumbatia elimu na ajira hakuna...lakin ukifuatilia vzr sidhani kama kuna kabila lenye diaspora nchini kama wahaya...hawajaamua tu kuwekeza Bukoba...lakin hakuna kabila lenye watu wengi nje ya nchi ya kama wahaya...tena wameajiriwa huko nje kihalali kabisa...


Endelea kudhatau elimu na kuamini haiwasaidii wahaya....halafu unasema kagera mazingira ya elimu sio mazr[emoji23]...ungejua sasa kagera ina shule nyingi kuzidi Dar na soon itaipita kilimanjaro kwa shule za sekondari na ishaipita kilimanjaro kwa shule za msingi ( ina shule zaidi ya 1000 sasa)
 
Mimi niko niliachia hapo ulipoanza kuwashusha wahaya na elimu zao...nikajua kabisa hauna kitu kichwani..

Hao wakinga na wapemba walivyo wachache ndo wakulinganisha na wahaya na wasukuma kweli...

Yes naweza kukubali kuwa wahaya hakuna wale matajiri extreme ( ingawa walikuwepo wakina Mfuruki aliyekuwa top ten ya matajiri na yule karamagi), lakini sidhani kuna kabila lenye middle class kama wahaya nchi hii...

Siku hiz mnawashusha kwa sababu ya mkoa wa kagera kuanguka kiuchumi na kuonekana maskini mbele ya serikali lakin reality maisha ya mtu mmoja huko kagera hasa uhayani na wale wahaya waliopo nje ya mkoa ni bora kuliko jamii nyingi nchi hii...

Yes wamekumbatia elimu na ajira hakuna...lakin ukifuatilia vzr sidhani kama kuna kabila lenye diaspora nchini kama wahaya...hawajaamua tu kuwekeza Bukoba...lakin hakuna kabila lenye watu wengi nje ya nchi ya kama wahaya...tena wameajiriwa huko nje kihalali kabisa...


Endelea kudhatau elimu na kuamini haiwasaidii wahaya....halafu unasema kagera mazingira ya elimu sio mazr[emoji23]...ungejua sasa kagera ina shule nyingi kuzidi Dar na soon itaipita kilimanjaro kwa shule za sekondari na ishaipita kilimanjaro kwa shule za msingi ( ina shule zaidi ya 1000 sasa)
watu wanaotusua saizi ni wenye biashara zao, hizo ajira kwa sasa wasomi wapo kila kabila na wamo maofisini na wengine zaidi wanahitimu kila mwaka na wengi zaidi wanazikosa ajira.

wahaya walikuwa juu ila wanazidi kushuka kwasababu wanakumbatia sana elimu pekee wakidhani tupo kipindi cha Nyerere kwamba wao na makabila machache ndio walikuwa wasomi pekee wenye sifa za kujazana maofisini, zama zimebadika kwa sasa wasomi wapo wengi kama utitiri karibu kila kabila wenye sifa za kuajiriwa, maifisini demographics zimebadilika mno.

Wahaya wajifunze kwamba ajira hazina mmiliki kwa sasa, karibu makabila yote yanafaidi keki hii, hatupo enzi zile kila bosi wa shirika anaruhusiwa kuajiri anaishia kuweka ndugu zake, kwa sasa ajira zinasimamiwa na wizara ya utumishi, mambo yamebadilika sana.

pia tukija katika maendeleo ya kimkoa Kagera ipo nyuma sana, ripoti zinaonyesha wazi Kagera ndio mkoa unaoongozea kwa umaskini na ni mkoa wa mwisho kuchangia pato la taifa.
 
Hakuna kabila lenye watu milioni 12, Tanzania, unaposema wasukuma milioni 12 ni uongo, wapo milioni 4 hivi au 5.
 
Ni kipi nimedanganya hapa ?

1. Mkoa wanaotoka wachaga hauongozi kwa shule nyingi ?
2. Mengi hakuwa tajiri pekee list ya top 10 mwenye asili ya Tz?
3. Wachaga sio kabila pekee wanalorudi pamoja kila mwisho wa mwaka?
4. Wachaga sio kabila linaloongoza kwa kuendeleza makwao ?
Top ten matajili Tanzania alikuepo Ally Mafuruki wa Infotex na Mengi, sasa wote ni marehem, hakiwa mengi peke yake.
 
Back
Top Bottom