2030 kuna uwezekano mkubwa Kafulila na Bashungwa wakapewa kijiti cha kuongoza nchi mama hatabiriki huko mbeleni

Probably Bashungwa japo hana mvuto Kisiasa ila kwenye kazi Yuko vizuri
 
TISS
 
2030 kwani 2025 Rais ameshapatikana?
 
bashungwa hicho kichwa cha Harvard University, anastahili, kwanza walau tuwe na Rais toka kanda ya uhayani, itafaa zaidi.
 
Punguzeni ramli
 
Wahaya na Waha mnapenda sana kukuza mambo!

Huyo Bashungwa mwenye domo zito ndo kawa muhimu kiasi hicho? Huyo Bashungwa ambaye Wizara zote alizopita zilimshinda!? Hapana

Halafu na wewe Kafulila mbona unapenda sana kujipigia promo? Kila siku kuja humu kujiandikia makala. Hufai
 
Mama Samia kwa jinsi navyomuona 2030 huenda akafanya kama ya jk 2015
Kama unadhani mgombea wa CCM 2025 lazima ni Rais Samia, kwanza soma hii Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! kisha Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke

Hakuna Rais wa Tanzania alipanga mrithi akafanikiwa!
Nyerere alimpanga Sokoine, akatwaliwa!, akampanga Dr. Salim, akapigwa zengwe, Mwinyi aliingia by defaults only!.

Mwinyi hakupanga mtu, Nyerere akamleta Ben!.

Ben akampanga Dr. Omar Ali Juma, watu wa kazi zao wakaingia kazini, akachomoka, JK akapeta.
JK alimpanga Eddo, system ikamgomea, JPM was just a default!. Mama anaendelea kujipanga huku hajui wataamua nini, ataendelea kuwapangua tuu lakini lililopangwa ndilo liwalo!.

Hao watu wako wawili uliowataja ni hakuna kitu hapo!, CCM wakifanya kosa hilo, litakuwa ni grave mistake, hoja za bandiko hili Uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, ndio mwanzo wa mwisho wa CCM! Wajinga karibu wote watakuwa wamemalizika!
P
 
Chapisho hili halikutoka kwa bahati mbaya .
 

Attachments

  • 5744975-8bcb85f1807b40dfe9b1bdf5a6eabbb0.jpg
    8 KB · Views: 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…