View attachment 2762707View attachment 2762709
Huyu alikulia hood mitaa iliyojaa msoto, uhalifu na umasikini, vitu livyoimba kuhusu shida ni mambo yaliyokuwa sehem ya maisha yake kwa muda mrefu.
2pac aliweza kufanya kazi kibao kudai haki, kuelimisha jamii, kutoa postive motivation, n.k. pia alipenda sana kusoma vitabu,
Changes ilikuwa kazi ya kiharakati kutetea haki za mtu mweusi, kukemea ubaguzi na kuhamasisha umoja wa watu weusi.
Dear mama ilitoa fundisho kuwa mama ni mama tu hata akiwa na mapungufu yake (mama yake alikuwa teja)
Only God can judge me alitoa ujumbe maridhawa kwamba ni Mungu pekee wa kumhukumu kikamilifu,
Brenda got a baby ilikemea mimba za utotoni.
Keep ya head high ni bonge la postive inspiration kujua thamani yako.
Wonder why they call you bitch ilitoa darasa kwa dada zetu tabia za kujiepusha ili wasijishushe thamani.
hizo ni chache tu.........
View attachment 2762702
View attachment 2762708
Ukija kwa Notorious Big, kwanza kabisa anadanganya kwamba aliishi maisha magumu wakati kiuhalisia hakulelewa maisha ya kitajiri ila sio haba aliishi maisha walau ya kati, mama yake alikuwa na kazi ya ualimu, Big alisomeshwa shule private, aliishi mitaa yenye hadhi ya wastan hakukulia hood, n.k. hali yake ilimpa wepesi hata wa kujuana na watoto wa kishua kina pdiddy, mama yake alikuwa anachukia sana kamlea vizuri ila yeye anadanganya kakulia kwenye shida
Big nyimbo kibao anaimba kubrag (kujisifia), bata, kudanganya aliishi maisha magumu, kusifia kuuza madawa kama njia sahihi ya kuhaso, n.k.
Huwa wanasema kazi zake za juicy na sky is the limit zina ujumbe, huo ujumbe ni upi ?
Juicy kaweka wazi mafanikio aliyopata kwenye mziki yamempa mkwanja wa kufanya umalaya na kupiga pamba kali, sioni cha kuelimisha hapo zaidi ya kujitamba.
Sky is the limit humo kaendeleza uongo wake kwamba alikulia maisha ya kimasikini, kasifia kwamba kuuza madawa ya kulevya kuna mkwanja kiasi aliamua kuacha shule ili ajifunze kuyauza, n.k.