Hao hawamuwezi Kikwete hata dakika moja, Kikwete ni mtu mkimya sana sana ,na hatari ya mtu mkimya ni kubwa kuliko yule anaepiga makelele,maana mtu mkimya anakuwa alert kwa kila step anayochukua,japo ataonekana hajui au mtamuona zezeta lakini hesabu zake haziendi upande, anapanga ,anayajua, na kuelewa ni wakati gani anahitaji kuchukua hatua ili kuidhibiti hali.
Hivyo hao akina Rostam na wengine inakuwa kama wadudu waliokuwemo ndani ya sufuria kubwa ,hivyo Kikwete aliepo juu anawaona na kuwatazama movement zao na nani anataka kutoka kwenye sufuria atamuona tena kwa urahisi zaidi ,natumai umepata picha halisi ,hivyo Kikwete anayatazama haya yanayofanywa kwa upole kabisa akiamini watu watajirekebisha intime kabla hajaamua kuwarudisha ndani ya sufuria kwa yule anaekuja juu akiamua kutaka kutoka ndani ya sufuria ,kwa ufupi hawa watu wamewekwa ndani ya kona au uangalizi na kila hatua wanayofanya inadhibitiwa na kupimwa kwa kina na malengo yake,kiasi kwa walipo wanaonekana wamo katika kugombea ukubwa wao kwa wao,hivyo Kikwete analielewa hilo ,na wao kama ndugu lazima mkubwa amuheshimu mdogo ,sasa wanapotokea ndugu kupigana inabidi uwawache ili mmoja aweze kumuheshimu mwenziwe.
Kikwete ni Raisi ambae amekuwa mvumilivu sana kiasi kuwa uvumilivu wake unaonekana kuwa umepita mipaka ,lakini anaamini kuwa kila mtu atauona ukweli wa anayoyafanya na atajirekebisha hivyo tunaweza kumuweka katika kundi la watu wenye subira.Na ndivyo nimuonavyo mimi kwa upande wangu ,ni mtu ambae anaweza kukasirika mpaka akabadilika rangi lakini mwisho wake hurudisha hasira zake na kuwa katika uvumilivu na ndio tunavyokwenda nae he is a man of GOD & we can do nothing to force him to take action by our makelele.
Hata Mtume wetu Muhammad alikuwa mpole sana kuna sehemu alipigwa mawe na yakamtoa ngeu na damu,malaika alimshukia na kumwambia sema tuwafanye nini wale watu ,Mtume akawaombea dua tu na hakuwatakia waadhibiwe.
Hivyo wavumilivu ni watu wa aina hawawezi kabisa kufuata matakwa ya mtu mwengine katika kuchukua hatua.