750k(take home) ni mshahara unaweza kumfanya mtu aishi kidogo bila wasi hapa Bongo?

750k(take home) ni mshahara unaweza kumfanya mtu aishi kidogo bila wasi hapa Bongo?

Una familia kubwa?
Unatumia kilevi?
Una michepuko?
Familia ninayo ndogo sana mkuu.
Kilevi umegusa penyewe na nimekaa nikatafakari chanya na hasi zake hivi juzi tu nimeapa situmii tena maana hawa marafiki ndo wananiponza. Nakunywa sana kiasi kwamba naamka asubuhi najikuta nimekata mpaka laki jana yake kwenye pombe!

Achana na hiyo take home lakini Kuna stahiki nyingine pia mwajiri hunipatia kwa mwezi, lakini pamoja na hayo yote kuna magumashi mengine pia huwa nayafanya yananiingizia takribani 200-300K per week huko ofisini lakini maisha nayoishi ni yale yale ya miaka yote, no Positive changes!

Nashkuru leo ni siku ya 3 sijagusa pombe, move nzuri katika kuacha kabisa maana siku ikipita sijanywa labda nina dozi.

Michepuko ipo lakini siithamini kama pombe na marafiki wa pombe!
 
Familia ninayo ndogo sana mkuu.
Kilevi umegusa penyewe na nimekaa nikatafakari chanya na hasi zake hivi juzi tu nimeapa situmii tena maana hawa marafiki ndo wananiponza. Nakunywa sana kiasi kwamba naamka asubuhi najikuta nimekata mpaka laki jana yake kwenye pombe! Achana na hiyo take home lakini Kuna stahiki nyingine pia mwajiri hunipatia kwa mwezi, lakini pamoja na hayo yote kuna magumashi mengine pia huwa nayafanya yananiingizia takribani 200-300K per week huko ofisini lakini maisha nayoishi ni yale yale ya miaka yote, no Positive changes!

Nashkuru leo ni siku ya 3 sijagusa pombe, move nzuri katika kuacha kabisa maana siku ikipita sijanywa labda nina dozi.

Michepuko ipo lakini siithamini kama pombe na marafiki wa pombe!
DAH mungu Akufanyie wepesi kaka uweze kupata nguvu ya kuicha kabisa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwa shida na mifumo ya kipumbavu ya serikali tuliyonayo unaweza kujibana bana ikakusaidia hiyo pesa. Usijiachie sana.

Hapo utalipa kodi, utanunua chakula na utaweza kusave kupata pesa ya mtaji kwaajiri ya biashara ndogo ambayo itasaidia kuongeza kipato.
 
Hiyo ni basic salary ya mwalimu wa digrii[emoji2]
Hapo hajakatwa kodi, bima, nssf nk
Siyo mwalimu sema mtumishi wa umma. Salary scale haitengenezwi kwa ajili ya walimu tu ni watumishi wote. Acheni chuki zenye laana kwa walimu waliowafikisha hapo mlipo. Kumdharau mwalimu ni sawa na kumdharau mzazi wako. Mi nitakuwa wa mwisho kumdhihaki mwalimu kamwe sintamdharau. Mtu unatoka kwenu Mwanza unaenda kusoma Tanga miaka 4 muda wote mikononi mwa walimu kipindi chetu hakuna hata simu barua mara ipotee njiani, kufika kwenyewe mwezi au zaidi. A-level Arusha toka Mawnza hiyo hiyo wazazi hawana wanalojua unatunzwa, unafundishwa na walimu. Leo una kakazi kako pengine kana mshahara zaidi ya mwalimu unaanza kumtukana, kumdhihaki. Mna laana shenzi nyie!
 
Wakuu nilikuwa nauliza tu kama 750k ni takehome inayoweza kumfanya mtu aishi kidogo standard life.

Maana isikute nadharau kumbe naweza kufanya kitu.
Halafu we usijifanye babukubwa eti 750K inatosha? Hapo ulipo unapata hata 100K kwa mwezi? Vitoto vya kitanzania ni vipumbavu hakuna mfano, mifukara tu anauliza utafikiri ana alternatives wakati maskini flani amejibanza kwa ndugu au rafiki tu. Acheni show off fake.
 
Back
Top Bottom