Sasa huyo aso kudai hela anaonekana mjinga Yani kuna vurugu na upotoshaji mkubwa kwenye hayo mahusiano hususa kwenye jamii yetu.
Fikiria hapo huyo unayempa hela na huyo usompa patakuwa na fair?!
Na huwa wanasema kabisa “ mwanamke usipoomba hela kwa Mwanaume wako jua Kuna mwanamke mwingine atamuomba na kumpa” kumbe ni kweli nimeamini kupitia hayo maandishi yako!
Tena unaandika kabisa huyo anaeomba hela mara kwa mara nampa tena huoni shida?
Maskini huyo mwanamke ndiye sasa anakuwa kama fala tu na kutumika bure!
Maana kama ingekuwa unampenda Kwa dhati ungekuwa naye peke yake na siyo kuwa na mwingine tena?!
Nimewaelewa wanawake wanavyosema usipomuomba Mwanaume wako hela ujue atakuwa na mwanamke mwingine ambae atakuwa anamuomba na kumpa kwa sana tu.
Kwa hiyo kumbe ni bora kuendelea kuwapelekesha kwa mwendokasi kwa kuomba hizo hela tu sasa manake hela ni hela ukiipata huwezi kosa cha kufanyia hata kula seafoods platter yako nzuriiii ya kutoka Kalambezi au kutumia vyovyote vile.