Ni kweli kabisa, anapokea kila mtu pale kwake, vijana na wazee, wake kwa waume, anaowafindosha kazi mbali, anaowafundisha ufundi mbali, anaowafundisha ujasiriamali na kutafutia mitaji mbali, anaowapatia ukulima mbao. Ilimradi kwa Mzee Abdul ushindwe mwenyewe tu.
Nilivypasikia nilikuwa siamini ikabidi nimtumie whatsapp kwa namab ya mtu nijifanye kama mimi ni single mother mwenye mahitaji maalum. Alinijibi kwa ufupi tu, njoo huku kwetu tuone tutanyanyuana vipi, unaishi wapi sasa hivi? Nikamwambia nipo Manzese kwa rafiki yangu, akaniuliza "utaweza maisha ya kwetu huku nje ya mji"? Kama utaona taabu siku ya Jumamosi tutampa mtu namba zako atakutafuta anakuja huko mjini, aone jinsi ya kufanya. Mie mwenyewe nikaonaa enheeeee, nimebeep amepiga. Nikamtumia message nikamwambia, asihangaike kumtuma mtu nimeongea na mdogo wangu kaniambia nikaishi kwake. Yalkaishia hapo.
Siku nyingine nikamtafuta kama ni mtu atakae kusaidia sadaka zake, akanambia "hatupokei sadaka za samaki" njoo huku uone sadaka zako zinavyoweza kurudi tena kwako, njoo uwekeze kwenye mambo ya waja wema. Hatutaki sadaka bila kuifanya kuwa endelevu. Haapo nikamshangaa sana na bado naendelea kumdadisi, nimeanza kuipata picha, ana very simple but highly effective ideas za empowerment. Tena akanifahamisha kuwa hata wao hawatoi sadaka ya samaki, wanakupa nyavu ukavue ili nawe uendeleze wengine. Siwezi kuyaeleza mengi aliyonifahamisha, atakae kuyafahamu amwandikie whatsapp, kanoiruhusu niitangaze namba yake, Hana neno.
Allah amzidishie kila la kheri, yaani kwanza utapoongea nae tu, unatambua kuwa huyu mtu yupo serious na anachokifanya.
Abdul Ghafur, hongera sana kwa juhudi zako. Allah akupe umri mrefu uwe mfano mwema wa kuigwa hata na serikali.