A God can be a mere theory, nothing more

Ivi mkuu ulitaka niseme biblia na quran zipo sahihi kwa pamoja? Nilichokiona mchanganyiko wa ukweli, uongo and many unreasonable teachings.

Kitabu cha Mungu kitasemaje uongo?

Ningeomba kwanza kujua japo kwa ufupi uliifanya vp hiyo research? maana mie nina mashaka kuwa huenda hukufanya research kabisa kutokana na hayo maswali uliyouliza.
 
Ningeomba kwanza kujua japo kwa ufupi uliifanya vp hiyo research? maana mie nina mashaka kuwa huenda hukufanya research kabisa kutokana na hayo maswali uliyouliza.

Nimeangalia namna tulivyopokea dini.
Nikajiuliza kwanini kila dini inajiona ipo sahihi kuliko nyengine.
Nikaangalia kwanini hasa mtu anakua mkiristo au muislamu.
Nikaangalia ukweli, uongo na contradictions za kwenye dini.
Nikajiuliza kwa nini manabii and/or mitume wote wametoka sehemu moja tu (far east)
Nikajiuliza kwanini udhaifu wa dini fulani uonekane na dini nyengine.

Nakushauri pitia post za mwanzo.
 

Oooh!!!! hapa jf ninao mtazamo huo, ila maisha yangu yana mtazamo mwingine. toa shaka kwa hilo.
 

Aisee! Mkuu unatumia kiungo gani kufiki?

Ivi ni kweli hujaelewa hapo au ndio umeshavaa jezi?
 
Simama mwenyewe ndugu. Unayaamini unayoyaandika kwamba ni zao la fikra pevu ?
Mimi imani yangu haitokani na woga hata chembe na wengi ndivyo walivyo

Kwanini wewe ni mkiristo na sio muislamu?
 

Na ndio maana umesema, baada ya kuona madhara ya hicho kitu unawakataza. Sasa kama umeshawakataza na bado wakatenda, madhara hayo yatawapata, na yakishawapata, kama yapo ndani ya utatuzi wako utatatua. Ndio maana Mungu alitangulia kuwaonya Adamu na Eva kwa kauli hii matunda ya miti yote mwaweza kula, walakini matunda ya mti wa katikati ya bustani msile, maana siku mtakayokula, hakika mtakufa. Hivyo Mungu alionya kwanza, na lakini hata baada ya wao kukaidi, bado aliahidi ukombozi kutoka kwenye kifo hicho kwa kumtuma mwanae afe kama mbadala.
 

Hahahahaaaa! watu mnatishwa sana! mwee!!

Ilipotokea dunia ni ngumu kuelezea kama wewe tu utakavyoshindwa kuniambia Mungu katokea wapi!!!!
 
We jamaa sifuri kabisa mukichwa " wanachokiamini Wakristo na waislam " sio sahihi ?
Umefanya utafiti kuhusu imani ukaja na fact ?

Hahahahaaaaa! wee jizonge tu. kumbe unaamini imani ni ububusa usio na fact sio?
 

Kwaiyo Mungu hakujua kwamba wangekula tunda? Au hakuwa na mbadala mwengine baada ya wao kula tunda? Kwanini sasa alimuacha shetani akawapotosha? Jee Mungu hakua na uwezo wa kumtokomeza shetani?
 
Hahahahaaaa! watu mnatishwa sana! mwee!!

Ilipotokea dunia ni ngumu kuelezea kama wewe tu utakavyoshindwa kuniambia Mungu katokea wapi!!!!

Mkuu jibu lake ni sawa na yale maswali ya kuku na yai ilianza nini
 
vitu vingi umeongea ukweli lakn wabongo kwa imani zao huwez kuwashawishi, hizi dini mbili ni mawazo yaliibuka hapo middle east watu waka copy na kupest na kutuletea huku. yaani mungu ambaye anaona dunia yoote awe na uvivu wa kupeleka imani mwenyewe brazil,afrika,china hadi watu waje wamsaidie tena wengine through vita?????
 
mkuu ninachofurahi ni kuwa angalau asilimia tisini ya maswali yako yanaufumbuzi kupitia neno lake ila kama ukiamua kujifunza kwa unyenyekevu.

Wewe sio wa kwanza hata paul wakati akiitwa sauli alikuwa anaua watumishi akidhani anafanya kazi ya Mungu kumbe alijichanganya.

Mfalme NEBUKADNEZA alikuwa na akili nyingi pengine kuliko mtu yeyote anayeishi duniani kwa sasa. Lakini wakati ulipofika pamoja na miungu yake yote. alikubali na kukili Hakuna kama Mungu wa Israel.

Ninachoomba ukweli huu uuelewe mapema kabla haujachelewa na moyo wako kuziba kabisa uwezekano wa kupokea ukweli.
natanguliza shukurani. kwa huo utangulizi wangu
 

Ila matumizi ya android na simu yameibukia kisarawe kwenu. Au uvumbuzi wa vitu Vingi mnavyovitumia waafrika vimetokea mzenga ndiyo sababu mnapata shida na hsbari za dini kutokea far east ?
 
Viumbe sisi pumzi zinatuongopea sana!Eeh mwenyezi nifanye niwe mmoja wa waja wako wema.aaamen
 
Maswali haya aliyouliza mtoa mada ni maswali mazuri. Wengine wanaweza kuona anakufuru. Naomba ni-declare interest kwamba mimi ni mtu wa imani.

Kuna makundi mawili ya watu.
1- Watu wanaomwamini Mungu kwa mkumbo: Hawa wao hawajawahi kukutana au kuzungumza na Mungu katika maisha yao. Ama ushirika wao na Mungu ni wa kubahatisha.
2- Watu wanaomwamini Mungu wanayemjua. Hawa wanaweza kuwa walianza kwa mkumbo, lakini baadaye walifika mahali pa wao kukutana na Mungu katika maisha yao. Hawa wanamjua Mungu wanayemwamini.

Maswali hayo ya mtoa mada nimeyapenda kwa sababu yanawa-challenge watu wa kundi la kwanza juu ya imani yao ya mkumbo.

Kwa mtu wa kundi la pili, hayampi shida. Mtu anakwambia Mungu hayupo, wakati wewe asubuhi tu Mungu huyo ametoka kuzungumza na wewe juu ya mipango aliyonayo katika maisha yako kwa mwaka ujao, inawezaje kukusumbua?
 
Dhana ya uwepo wa Mungu haihusishi jinsi wanadamu wanavyoabudu,bali inajumuisha makundi yote yenye uhai.
Tunaweza kusema sisi kama binadamu kuwa hakuna Mungu lakini viumbe hai kama miti na wadudu wakathibitisha uwepo wa Mungu pasipo shaka yeyote.
Uwepo au kutokuwepo kwa Mungu uanza na huishia pale kundi moja linapobadilika kwenda kundi jingine la uhai.
Hivyo ili tuweze kuelezea dhana hii ni lazima tuangalie namna gani makundi ya vitu vyenye uhai vinavyoishi na kupotea kuliko namna gani dini zinavyotumika na kundi moja tu hususa sisi wanadamu.
Mimi kama binadamu ninaamini kuwa chochote kile kilicho na uhai na kisicho kilichoumbwa na Mungu kinatimiriza uwepo wake na ili kitokee ni lazima kitu hicho kitoke kwenye hali moja kwenda kwenye nyingine (mfumo mmoja wa uhai kwenda mfumo mwingine).
Pia naamini kuwa kifo ndilo fumbo kubwa linalowasumbua wanadamu na yamkini ndicho kitu wanakiogopa kuliko hata yule aliyewaumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…