Ntuzu
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 17,418
- 10,877
Yaleyale nlokwambia. Amri kumi za Mungu hajakataza kuoa mke zaidi ya mmoja. Amesema tu usizini. Lakini ndo kama nlivyosema, kuna vimjamaa vilijifanya vina ushkaji na Mungu ndo wakaleta hivi visheria vyao vipya kuongezea ukali wa maisha.
Tuseme tu ukweli.... Kama tutalazimika kufuata Amri kumi za Mungu, pamoja na viamri vingine vya nyongeza... Hakuna atakayeweza kwenda mbinguni. Kwanza viamri vingine vinapingana vyenyewe kwa vyenyewe mpaka mtu unajiuliza ufuate ipi?
Mi naamini njia bora na sahihi ya kwenda mbinguni, bila kujali imani sijui ya dini/dhehebu gani..... Ni kutenda wema! Yani ni kuwa na upendo tu baaasi. Vingine vyote ni mikwala tu.
Uzuri wetu wapiga ulabu huwa hatuna maneno na watu. Unapiga ulabu wako kwa upendo unarudi kitandani kwa amani...
Asprin na Mashaxizo
Nina swali moja kwenu!
Dhambi ni nini? Au dhambi ni kukosea nini?
Nawaomba mtoe majibu kwa mujibu Wa biblia!
Last edited by a moderator: