Abby Chams: Sijawahi kula miguu ya kuku wala firigisi, wala sijawahi kusikia sehemu inaitwa Mburahati

We kenge kuna elewa maana ya kupasikia na kupajua

Shule ulienda kusomea ujinga?
 
Shida ya wabongo wanaamini ili uwe mtanzania basi ni lazima upitie shida kama wao.

Niliwahi kuwa na Binti kwenye mahusiano ilikuwa full vichekesho akifika ghetto,ila baadae nikamzoea.

Nikisonga ugali alikuwa hajui jinsi ya kumega Wala kupamba kwenye mboga. Ikabidi niwe mwalimu nimfundishe jinsi ya kumega,kumpoozea na kufinyanga tonge.

Siku ya kwanza kuingia bafuni akakutana na kopo la kuogea akauliza hiki kikombe Huku kina kazi gani,nikamwambia hiki ni kwa ajili ya kujimwagia maji. Kwao full mvua unatachi tu na kubadilisha maji either yawe ya baridi au ya vuguvugu. Ana gym yake private thamani ya vilivyomo humo ndani ni mtaji wa Biashara wa mtu sinza.

Mwanzoni mwa mahusiano Kila mmoja alikuwa anamwona mwenzie kama anaigiza maisha. Mimi namshangaa na yeye ananishangaa na kunionea huruma, nikimsimulia maisha magumu ya zamani analia.

Huyu Aby chams anashambuliwa na wabongo sana mitandaoni. Sijui kwa nini tunahusudu umasikini kiasi hiki.
 
We msengerema semea nafsi yako
 
Watu wengi wanaona haiwezekani Mtanzania asiijue Mburahati.

Wakati wao wenyewe nikianza kuwauliza Mwembetogwa ni wapi, Mchafukoge ni wapi, Miburani ni wapi, wengi hawapajui.
 
Akishafikisha 30 mbwembwe zote zitaisha hizo.
 
Kula miguu ya kuku, utumbo wake, ama kichwa chake, nakubaliana naye kwa 100% lkn kwa firigisi. moyo, ama maini ya kuku hapo kapiga fix.


Mb'hati, Tandale, Senze,, Mabibo, Luhanga, ama Kigogo ni chimbo la wana wengi sana. Kujifanya hulifahamu ni kujitoa ufahamu.

Ukisema wana asili wa Masaki, Upanga, ama Posta hawalifahàmu vyema naweza kukubaliana na wewe. Lakini kama historia yako si ya Tanganyika School ya enzi hizo, unatuletea uchwara tu.
 
Umeiweka kitaalam sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…