Abby Chams: Sijawahi kula miguu ya kuku wala firigisi, wala sijawahi kusikia sehemu inaitwa Mburahati

Hey ndugu mshabiki, naomba niseme kitu kimoja ninachokiona Mimi.

Huyo binti anaweza akawa hayuko sahihi kama ambavyo hao wanamshambulia hawako sahihi na hata nyie watetezi wake pia hamko sahihi kwenye utetezi wenu.

Kwanza kabisa akiwa kama msanii anapaswa kujua watu(watanzania) wanaofuatilia Muziki wake ni watu wa aina gani kwanzia uelewa mpaka zao za kimaisha zikoje na vitu ambavyo mara nyingi vinawafanya kuwa hypersensitive.

Ni jambo ambalo liko wazi hakuna kitu ambacho kinamfanya mtanzania hasa wa Hali ya chini kutoa sensitive reaction kama pale anapohisi unamkebehi kuhusu Hali yake ya kimaisha( naomba unielewe hapa), mtanzania ukiongelea habari za kutokula baadhi ya vyakula ambavyo yeye ndio chakula Chake Cha Kila siku anahisi kama umemdharau sana).

Sasa huyo Abby champis sijui Abby champs kwa aina ya majibu anayotoaga ni obvious lazima wabongo wampopoe maana majibu yake Yana create negative feelings, sio kwamba wako sahihi lakini ndivyo jinsi walivyo.

Kwahiyo Sasa kuliko kuanza kujustify sijui ametoka familia ya kishua mara ooh kakulia nchi za nje inapaswa nyie washauri wake mumfundishe namna nzuri ya kujibu maswali ya aina hiyo yaani ajue kuingea nini na kwa wakati gani...

Mimi binafsi huwa simlaumu kutokana na umri wake. Na pia suala la yeye kukulia ushuani sio sababu ya msingi ya hicho anachokifanya maana yeye sio msanii wa kwanza kutoka familia ya kishua.

Mbona Navy Kenzo wanaotoka familia za kishua lakini hatujawahi kuona wakipopolewa na wabongo kama anavyopopolewa huyu Binti??? Kwani wao hawajaishi nje?

Jibu ni kwamba Envy Kezno wanajua kuishi na mtaa wakati huo huyo binti yenu hajajua kuishi na jamii ya kitanzania kwa namna inavyopaswa, na mbaya zaidi career yake Bado changa sana.

Mfahamishe tu kuwa hao Wala miguu ya kuku na firigisi wanaotoka Mburahati na maeneo mengine yenye hadhi ya Mburahati ndio mashabiki wakubwa wa Muziki wa bongo flavor na wao ndio wanaweza kuamua kupush Muziki wake au kumu hold back, hivyo haepuke kuwakwaza kwa namna yoyote ile hata bila kukusudia na pia vile vile ajifunze kiundani kuhusu uhalisia wa maisha ya watanzania wengi yakoje.
 
Kweli wanatujazia server kwa nyuzi zisizo na kichwa wala miguu iwe anapajua au hapajui sisi inatuongezea nini au ina mchango gani kwa Taifa
Kiingereza chake ndio kipimo cha kuitwa mshua na celebrity. Huyu ameishia grade 10 Haven of Peace Academy.
 
imagine mkuu. pia sio kila kitu mtu lazima apende au atake kula. mfano utumbo mimi, uwe wa kuku sjui wa ng'ombe, hell NO[emoji55]

au sjui kisamvu sjui matembele yani siwezi,
sio kibaya but sipendi taste yake , na baadhi vingine, but miguu ya kuku nakula tena soup yake napenda.

so guys muacheni mwanangu msimuone anaringa but ni kweli
 
umemaliza mkuu, ni suala la huyo binti aelekezwe tu kitu gani cha kusema in public kwa hadhira yake ambao 99% ni watz. Management yake wawe proffesional, azingatie nini cha,kusema mbele ya media.

hao waandishi wanamuuliza maswalivya hivyo ili wapate content tu, but management iwe inawapa limitation ya maswali cas mashabiki watamchukia kwa kuona kama anawadharau.
 
Huyu ndo nani kwani??
 
Kawaida sana kwa watoto wa kishua, hata wa kwangu sio wa kishua lakini hawajawahi kula miguu ya kuku na kambi ya fisi hawajawahi kupasikia🤪.
Fiŕigisi wanazijua.
 
Hata mimi nikulia ushuani na nimefika mburahati, manzese ndani ndani mpaka uwanja fisi, buguruni zote, Tandika, Temeke yote, mbagala zote, mtoni zote na ni curiosity tu ya kuangalia maisha tofauti na mpaka leo nawashukuru sana wazazi kwa maisha niliyokulia na kwa kweli hizo sehemu nashukuru sikuishi huko na sio jambo la kujivunia kama unaishi huko ni hali ya umasikini inayotakiwa kupigwa vita na si kujivunia
 
Mtangazaji mjinga sana, mburahati kuna umaarufu gani Tanzania hadi pajulikane na kila mtu?
 
Another fool, unafikiri dar tu ndo kuna ushuani? Ushamba mzigo,
 
Mbona dogo ni wa kishua, kwani hutaki au?

Dogo hana uswahili kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…