Tetesi: Abdallah Bulembo akalia kuti kavu kisa elimu yake

Bulembo hajaiingia pale kwa elimu yake,pale kaingia kwa kujua kulamba watu fulani,usisahau kibint chake kina miaka 21 tu tayari ni mbunge wa vijana hiyo kazi yake ya kumchekesha mfalme sio ndogo
Yupi kati ya hawa wawili?
 
Kwani kila kitu ni elimu? CCM imefika hatua ya kumtema kweli? nilifikiri huyu alikuwa mshauri muhimu wa mjomba wakati wa uchaguzi!!
 
Hivi huyu aliyemteua hivi karibuni kuwa mwenyekiti wa board Fulani mbali ya kuwa amejichokea anaelimu gani?
 
kabla ya kuropoka unazijua sifa za kugombea hiyo nafasi? ccm inaongozwa na katiba si matamko.
 
Jumuiya za Chana cha Mapinduzi, haziongizwi kwa kufuata hivyo uunavyohitaji wewe kuwa ni lazima iongozwe na mtu mwenye Elimu kubwa sana na yenye kutisha. Tulikuwa na Mheshimiwa Marehemu Rashudi Mfaume Kawawa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, huyu Bwana alifanya kazi kubwa sana kwa iliyokuwa Jumuiya ya Wafanyakazi na aliiongoza vizuri tu. Uongozi ni karama mbona hivi sasa tuna Maprofesa wanaojiuzuru nafasi zao kwa utashi wao na baadae kuja kuzidai kana kwamba wao ndiyo wenye uwezo huo pekee?
 
Huenda kuna ukweli na fyekeo hilo lipite mpaka ilipo mizizi maana kule ndo hapafai kabisa.
 
dunia imebadilika kwa kasi sana ,kawawa hakufika chuo kikuu lakini huwezi kumfananisha na villaza wa ...... alikuwa vizuri kichwani ndio maana akawa pm wa jk nyerere ,hata jpm ameligundua sasa we angalia shule za jumuiya ya wazazi zinapumulia mipira kila kitu sasa kinaongozwa na elimu mkuu
 
Mzee Bulembo kwani hizi sio zama za kujua kusema zama za sayansi Na teknolojia mkuu
 
siasa sio kazi ya taaluma ingawa kuna nafasi kama za ukatibu mkuu zinahitaji watendaji wenye uwezo zaidi ndio maana kuna chama ambacho mwenyekiti wake elimu yake haieleweki ingawa anaongoza mpaka maprofesa pia kuna wabunge darasa la saba kama lusinde na yule mbunge ambaye juzi juzi amevuliwa madaraka akikana elimu yake.Kama Bulembo angekuwa ameomba kazi ya kuajiliwa ni wazi angeondolewa sababu hakuwa na vigezo lakini kama elimu yake inamruhusu
 

Nakubalianà na wewe kwa kiasi fulani tu, mbona hawa wa sasa hivi hizo Elimu zao hata wenyewe haziwasaidii? Utakuta mtu ana Dgree ila hata kujielewa hajielewi hizo nafasi za uongozi akipewa si ndo anaharibu kabisa? Tukubaliane kuwa Elimu inahitajika hasa kwa kazi za Kitaalamu zaidi ila hizi za kuongozana hata wa Kidato cha Nne anatosha alimradi anajua kusima na kuandika kama alivyo yule ndugu yetu wa kile chama jirani, anaweza hata kuonyesha Cheti cha kidato cha Nne? Ila tunamuamini sana na kazi ya kutuongoza anaiweza juzi juzi katoa tamko na tumelikubali.
 
ni kujipa moyo tu kwa karne hii form four wa tanzania cheo cha juu kabisa ni mjumbe wa nyumba kumikumi tu hata kama ni mwenyekiti sio saizi yake
 
ni kujipa moyo tu kwa karne hii form four wa tanzania cheo cha juu kabisa ni mjumbe wa nyumba kumikumi tu hata kama ni mwenyekiti sio saizi yake

Mkuu wengi wenye hizo elimu kubwa kubwa wanatuangusha sana
Ukiangalia hasa Serikali iliyopita, mambo mengi yameharibika kwa hawa wenye Elimu kubwa ya Vyeti na hivi sasa wengine wanaachia ngazi baada ya kubainika vyeti vyao ni Feki, tumuache Mhe Bulembo apige kazi maana duuuh si unakumbuka alivyoambatana na Mkubwa kwenye kinyang'anyiro kilichopita? Bado anafaa kwa naandalizi ya 2020
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…