Abdul mwana wa Rais Samia yuko nchini India kwenye msafara wa Rais

Abdul mwana wa Rais Samia yuko nchini India kwenye msafara wa Rais

Akihutubia katika chuo kimoja huko India JAWAHARLAL NEHRU UNIVERSITY, nchini India Rais amemsimamisha na kumtambulisha mwanae wa tatu Abdul kwenye mkutano huo.

Ikumbukwe kuwa mwana huyu alionekana akiwakilisha nchi kwenye mkutano mmoja na Rais wa nchi ya Uganda mh Yoweri Museveni na sasa kaandamana na ujumbe wa Rais nchini India.

Huyu mwana ana wadhifa gani ndani ya serikali ya Muungano wa Tanzania? Naamini haya ni maswali yasiyoepukika hasa kwa wanaolitakia mema Taifa hasa Kwa masuala ya utawala Bora na kulinda Rasilimali za Taifa .

View: https://youtu.be/fCKlJX19s6w?si=EKNnnJd2Gcag64N_

Salaam aleikhumu .

Kiongozi huandaliwa
 
Acheni mtoto pendwa Abdul adeke bhana.......hata nyinyi mlivyokuwa wadogo mlikuwa mkifuatafuata mama zenu nyuma kila mahala.
 
Hacheni Dula ale maisha nchi si ya mama yake na anko J.
 
Ukipata nafasi saidia ndugu kwanza halafu jirani. Hvi wewe muanzisha mada ni Mtanzania kweli? maana hii desturi yetu naona kama huijui
 
Utakufaa namichuki yako ya kijinga na kimasikini.Tangia lini katiba yetu ikapiga marufuku Rais kuwa na familia yake au mtoto wake akitaka kwenda naye mahali? Kwani Rais hana uwezo wa kumlipia mwanae Nauli? Pasukaaa kama umetumia.pambana na wewe upate nauli usafiri nje ya nchi
Ukunguni kumbe maana yake ni kutokuwa na akili sawasawa!
 
Alikuwa kwenye mahafali ya mama yake ambaye ametunukiwa PhD wajameniii mbona kawaida!
 
Yeye sio mwajiriwa wa serikali, anakwendaje kufanya nini na kwa gharama za nani!
Tutarajie "dipii wedi" nyingine
 
Akihutubia katika chuo kimoja huko India JAWAHARLAL NEHRU UNIVERSITY, nchini India Rais amemsimamisha na kumtambulisha mwanae wa tatu Abdul kwenye mkutano huo.

Ikumbukwe kuwa mwana huyu alionekana akiwakilisha nchi kwenye mkutano mmoja na Rais wa nchi ya Uganda mh Yoweri Museveni na sasa kaandamana na ujumbe wa Rais nchini India.

Huyu mwana ana wadhifa gani ndani ya serikali ya Muungano wa Tanzania? Naamini haya ni maswali yasiyoepukika hasa kwa wanaolitakia mema Taifa hasa Kwa masuala ya utawala Bora na kulinda Rasilimali za Taifa .

View: https://youtu.be/fCKlJX19s6w?si=EKNnnJd2Gcag64N_

Salaam aleikhumu .

Me nafikiri tungeanza kumjadili Obama kwanza maana alikua anaongoza kusafiri na watoto wake.

Acha wivu wewe. Sio dili.
 
Me nafikiri tungeanza kumjadili Obama kwanza maana alikua anaongoza kusafiri na watoto wake.

Acha wivu wewe. Sio dili.
Issue si kusafiri, issue ni kuunganisha familia na madili yanayogusa Taifa. Waafrica Wana laana
 
Back
Top Bottom