Abdulrahman Kinana: CHADEMA wamelipwa ruzuku kiasi cha Billion 2.7

Nimemsikia Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Kinana akiwahutubia Wanaccm wenzake juu ya Maridhiano .Miongoni mwa Mambo aliyoyazungumzia ni Suala la RUZUKU ya CHADEMA .Kinana amesema Chadema Wamelipwa Tsh.BIL.2.7 lakini HAWAJATANGAZA
Najiuliza JE LINI CCM iliwatangazia WANACCM kuwa inapata RUZUKU kiasi gani?Binafsi naamini CCM inapata RUZUKU mara 10 YA RUZUKU ya CHADEMA lakini pamoja na RUZUKU kubwa bado CCM inatumua FEDHA za SERIKALI kuendesha Shughuli zake kwa mfano SHUGHULI za CHAMA magari karibu yote yanayokuwa kwenye Misafara ya VIONGOZI wake ni ya SERIKALI fuatilia ZIARA za Viongozi wa CCM kwa mfano hai ZIARA anazifanya MAKONDA una msafara wa Magari zaidi ya 30 na yote ni ya Serikali .CCM haiwezi kutangaza RUZUKU yake kwani nayo INAPIGWA badala ya KUNUNUA Magari wakayapaka Rangi ya Kijani ili tuyaone ktk MISAFARA ya MAKONDA
Tunakuomba KINANA tuambie CCM inapata RUZUKU kuasi gani na kazi ya RUZUKU ni nini?

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Abdul Rahman Omar Kina miaka hiyo mitatu chama chako kimelipwa ruzuku kiasi gani tuanzie hapo.
 
Wamelipwa billion zote hizo kwa nini wasianze ujenzi wa ofisi ya makao makuu badala ya kukodisha nyumba ya mbowe? Hakyanani hiki chama kimejaa nyumbu tupu!
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Abdulrahman Omari Kinana amedai Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kililipwa Tsh. Bilioni 2.7 ikiwa ni malipo ya ruzuku ya miaka mitatu kutoka Serikalini, mchakato ambao ulifanyika wakati wa mazungumzo ya maridhiano baina ya CCM na CHADEMA.

Amesema “Ruzuku inapitia katika Bajeti ya Serikali na ikishapita haipatikani tena lakini Rais (Samia Suluhu) akaagiza Serikali kutafuta utaratibu wa kuwalipa na wakasema mkitupa hizo hela itakuwa mwanzo mzuri wa kutambuana, wakalipwa lakini hawakuwahi kusema japo madai yao yalikuwa yamepitwa na wakati.”
Ulitaka wamwambie nani??
Kama majukumu yanaenda sawia na malipo hayo.

Unaacha kusema ya Chama chako unakalia umbea!!
 
04 February 2024

Abdulrahman Kinana kuhusu maridhiano , uchaguzi wa 2019 na 2020 CCM hatutaki kutoa kauli kuwa uchaguzi ulivurugwa. Bali tumekuja na sheria pia miswada kurekebisha ya 2019 na 2020

View: https://m.youtube.com/watch?v=-FxK8p4voBI

Makamu mwenyekiti wa CCM asema chama dola kongwe kina nguvu na madaraka tunayo lakini hatuwezi kutoka hadharani kukubali uchaguzi wa 2019 na 2020 ulichafuliwa na kuporwa.

Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana anaongeza kuwa hatuna rais mfalme na ndiyo maana ameamua kutoa nafasi mabadiliko ya sheria za uchaguzi wa madiwani, mabunge na rais, pili sheria za tume ya uchaguzi na tatu katiba

Makamu mwenyekiti Abdulrahman Kinana amekishutumu chama kikuu cha upinzani CHADEMA kwa sababu ilidai rais apunguziwe madaraka, Serikali tatu, maridhiano kushirikisha vyama vikubwa tu na vile vya mfukoni kuachwa pembeni...
 
😂😂 vigogo wa Tanzania hawajali nchi ni matumbo yao na familia tu
 
Aibu Sana Hii Ndani Ya CCM Mnavuruga Uchaguzi Leo Mnatamba Hadharani
 
Wale covid ndio tatizo maana wanakula wasichostahili acheni kutuona wajinga.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Abdulrahman Omari Kinana amedai Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kililipwa Tsh. Bilioni 2.7 ikiwa ni malipo ya ruzuku ya miaka mitatu kutoka Serikalini, mchakato ambao ulifanyika wakati wa mazungumzo ya maridhiano baina ya CCM na CHADEMA.

Amesema “Ruzuku inapitia katika Bajeti ya Serikali na ikishapita haipatikani tena lakini Rais (Samia Suluhu) akaagiza Serikali kutafuta utaratibu wa kuwalipa na wakasema mkitupa hizo hela itakuwa mwanzo mzuri wa kutambuana, wakalipwa lakini hawakuwahi kusema japo madai yao yalikuwa yamepitwa na wakati.”
ccm wao wanasemaga wanakula ngapi!
 
"Wakasema mkitupa hizo hela itakuwa mwanzo mzuri wakutambuana"

😀😀😀😀😀😀😀😀🤣🤣🤣

Siasa hizi.
 
04 February 2024

Abdulrahman Kinana kuhusu maridhiano , uchaguzi wa 2019 na 2020 CCM hatutaki kutoa kauli kuwa uchaguzi ulivurugwa. Bali tumekuja na sheria pia miswada kurekebisha ya 2019 na 2020

View: https://m.youtube.com/watch?v=-FxK8p4voBI

Makamu mwenyekiti wa CCM asema chama dola kongwe kina nguvu na madaraka tunayo lakini hatuwezi kutoka hadharani kukubali uchaguzi wa 2019 na 2020 ulichafuliwa na kuporwa.

Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana anaongeza kuwa hatuna rais mfalme na ndiyo maana ameamua kutoa nafasi mabadiliko ya sheria za uchaguzi wa madiwani, mabunge na rais, pili sheria za tume ya uchaguzi na tatu katiba

Makamu mwenyekiti Abdulrahman Kinana amekishutumu chama kikuu cha upinzani CHADEMA kwa sababu ilidai rais apunguziwe madaraka, Serikali tatu, maridhiano kushirikisha vyama vikubwa tu na vile vya mfukoni kuachwa pembeni...

CCM inaonekana hata ile miswaada mibovu serikali yake ambayo waziri wa nchi masuala ya sera, uratibu na bunge aliyosoma ktk mkutano wa 14 wa bunge unaendelea Dodoma hawajakubali kiuungwana bali kwa shingo upande sana na si ajabu wakafuata njia rais wa Senegal kuifuta

04 February 2024
Dakar, Senegal

RAIS WA SENEGAL AFANYA MAPINDUZI YA 'KIKATIBA' KWA KUFUTA UCHAGUZI MKUU

Rais wa nchi tulivu iliyokwepa Mapinduzi ya kijeshi ya Africa Magharibi ya Senegal imeigia katika mtihani mkubwa toka ipate uhuru wake. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo uchaguzi mkuu kalenda ya uchaguzi kufutwa kwa muda usiojulikana.
1707076806947.png

Picha: Rais Macky Sall wa Senegal

Uchaguzi mkuu ulitegemewa kufanyika tarehe 25 February 2024, lakini kwa kutumia madaraka yake wachunguzi wa kisiasa wanasema haya ni mapinduzi ya kikatiba kwa rais Macky Sall kuahirisha uchaguzi mkuu.

Rais Macky Sall asema sababu ya hatua yake ni baada ya mahakama ya kikatiba kukata majina ya wagombea baada ya kudai majaji walikula rushwa kuondoa majina ya watia nia wa kugombea uongozi ktk uchaguzi wa baadaye February 2024

Rais Macky Sall aliingia madarakani kupitia uchaguzi mwaka 2012 na kuchaguliwa tena 2018 huku akitangaza kuwa hatagombea tena urais 2024.

Viongozi wa upinzani akiwemo kinara wa upinzani Bw. Ousmane Sonko walaani hatua hiyo ya kufutwa uchaguzi mkuu kwa kisingizio cha rais Macky Sall aliyepo madarakani kuokoa taifa toka Mahakama ya Kikatiba anayodai imekosa sifa kutokana na rushwa kusimamia uchaguzi huru na wa haki

Upinzani wanadai hatua hiyo ya rais Macky Sall ni njama zake za kuendelea kubakia madarakani kwa kufanya mapinduzi ya 'kikatiba' tofauti na nchi jirani za Afrika magharibi kutumia mapinduzi ya kijeshi kuingia mafarakani.

Wachambuzi wa siasa za Senegal wanasema rais Macky Sall amefanya mapinduzi hayo ya kikatiba kutokana na woga kuwa akiingia rais mwingine madarakani ataingia katika matatizo kutokana na ufisadi wa utawala wake toka mwaka 2012 utamuwekea mazingira ya kushitakiwa kama rais aliyemtangulia, rais Abdoulaye Wade alifunguliwa mashitaka na kubidi kukimbilia uhamishoni Ufarasa kuepuka kifungo.
1707076869600.png

Picha maktaba : Rais mstaafu Abdoulaye Wade wa Senegal
 
View attachment 2894448

View attachment 2894452
Picha maktaba : Rais mstaafu Abdoulaye Wade wa Senegal

CCM yazidi kushupaza shingo kuwa hawawezi kutoka hadharani, ingawa katika mazungumzo ya maridhiano ya faragha wakubali walifanya faulo kubwa 2019 na 2020 .... Abdulrahman Kinana azidi kufunguka jinsi walivyojitahidi kuachana na jinamizi la CCM kupora uchaguzi wote kwa kukusanya vyama mamluki vidogo dhidi ya wasema kweli wenye msimamo CHADEMA ...

View: https://m.youtube.com/watch?v=qJSMiUBM-ic
 
Back
Top Bottom