Pre GE2025 Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia

Pre GE2025 Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
View attachment 3056347
Abdulrahman Kinana

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amemwandikia barua ya kuomba kupumzika.

Katika majibu yake Mwenyekiti wa CCM amesema "Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako".

Pia Mwenyekiti wa CCM amesisitiza kuwa Chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Ndugu Kinana kila vitakapohitajika.

Chama Cha Mapinduzi kinamshukuru Ndugu Abdulrahman Kinana kwa mchango wake mkubwa kwa Chama chetu.
View attachment 3056339
Amemaliza kazi aliyotumwa.
Kazi kwao watekelezaji.
 
Yusuf Makamba
January Makamba
Nape Nnauye
Kinana Abdulrahman

Hawa wanajuana sana ni kundi moja kwenye kupeana chapuo za uongozi

Kama ni mpasuko umetokea CCM kwetu ni habari njema ila kama wamewekwa pembeni kwa kazi maalumu kuelekea uchaguzi kwisha habari yetu
 
Back
Top Bottom