Pre GE2025 Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia

Pre GE2025 Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hii si bure bali kuna jambo.

Huenda ule utenguzi wa wale jamaa unahusika.

CCM kimwili wako pamoja, ila kiroho wana makundi tena yanayotafunana kuelekea 2025.
Yaweza kuwa laana ya wanung'ung'unikao kwa matendo yao,waombwe radhi maisha yaendelee.
 
images - 2024-07-29T200954.804.jpeg
 
View attachment 3056347
Abdulrahman Kinana

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amemwandikia barua ya kuomba kupumzika.

Katika majibu yake Mwenyekiti wa CCM amesema "Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako".

Pia Mwenyekiti wa CCM amesisitiza kuwa Chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Ndugu Kinana kila vitakapohitajika.

Chama Cha Mapinduzi kinamshukuru Ndugu Abdulrahman Kinana kwa mchango wake mkubwa kwa Chama chetu.

PIA SOMA
- Matokeo CCM: Abdul Kinana Makamu Mwenyekiti Bara, Hussein Mwinyi Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Samia Hassan Suluhu Mwenyekiti Taifa

Nakumbuka mwaka 2017 baada ya Nape vuvuzela bumunda kufukuzwa uwaziri zilianza tetesi kwamba Kinana amesusa kufanya kazi ya ukatibu mkuu. Na kweli baada ya hapo alikuwa haudhurii vikao vingi vya kamati kuu na halmashauri kuu kwa taarifa kwamba anamuuguza mtoto wake India au yeye mwenyewe kuugua,ziliendelea kuwa tetesi mpaka siku alipojuzulu rasmi.
Coincidentally? Baada ya vijana wake aliofanya nao kazi kwa karibu 2015 kung'olewa kwenye uwaziri chini ya wiki moja naye anajiuzulu.
Je,inavyodaiwa kwamba waliondolewa kwa sababu ya mipango na yeye alikuwa sehemu ya mipango?
Je ni kweli ameamua kustaafu na kwa nini sasa sio jana au kesho?
Je kasusa baada ya kuona vijana wake wametemwa?
 
Back
Top Bottom