Pre GE2025 Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia

Pre GE2025 Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
View attachment 3056347
Abdulrahman Kinana

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amemwandikia barua ya kuomba kupumzika.

Katika majibu yake Mwenyekiti wa CCM amesema "Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako".

Pia Mwenyekiti wa CCM amesisitiza kuwa Chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Ndugu Kinana kila vitakapohitajika.

Chama Cha Mapinduzi kinamshukuru Ndugu Abdulrahman Kinana kwa mchango wake mkubwa kwa Chama chetu.

PIA SOMA
- Matokeo CCM: Abdul Kinana Makamu Mwenyekiti Bara, Hussein Mwinyi Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Samia Hassan Suluhu Mwenyekiti Taifa

Na Bado. Mzimu wa Magufuli utawamaliza wote walioshangilia kifo chake. Muda utajibu
 
Yaan hipo hivi, huyu mzee yupo kwenye kundi la January Makamba kumfanyia figisu mama. Kwa mujibi wa taarifa ya kigogo, wajumbe wengine kwenye kundi hilo ambalo lilitaka Kipara awe makamu wa Rais mwaka, 2025 yupo, Adams Malima,Kinana .

Ilikuwa lazima mzee huyu ajiuzulu tu kwa kuwa amegundulika kwenye uhaini huo.Na amelazimishwa kujiuzulu kwa kuwa ni msaliti.
Ila maza acha akome aliona walivyokuwa wafitini enzi za mwendazake yeye kajifanya bibi huruma
 
Hata mimi. Mtu wa muhimu kwa Samia ni Kikwete, mkwe wake sio heavyweight wala sio smart. Samia hana team mpaka sasa amekumbatia team ya Kikwete ambayo ndio hii kaanza kuivuruga.

Adui muombee njaa. Natamani wafeli vibaya mno wavurugane
point...........sawasawa.....sahihi..
 
In msoga voice "labda mambo yakiaribika sana" naona mambo ndo hayo yameshaanza kuparanganyika
Mzee wenu keshapigwa pingu tayari hamuwezi tena Mama Samia, njia nyeupe kwa Mama Samia 2025 hakika Mama kachagua fungu jema kuambatana na Paul C. Makonda.
 
Back
Top Bottom