Abel na Kaini (kizazi cha Adamu na Hawa); Je, wake zao ni kizazi cha nani?

Abel na Kaini (kizazi cha Adamu na Hawa); Je, wake zao ni kizazi cha nani?

mchina muafrika mzungu mwarabu mjapani walikuaje na asili tofauti na adam na hawa? na kama asili ya mwanadamu ni pale eden, wamarekani wabrazil waargentina wametokea wapi? sababu wapo bara tofauti na bara waliloumbiwa adam na hawa.
Mkuu wakati nilipojiuliza hili swali, niliona nadharia ya uumbaji ni uongo...Kama chanzo cha watu ilikuwa Eden, ni teknolojia ipi iliyotumika kusambaza watu kwenda mabara mengine? watu walifikaje Peru, Chile Madagascar na maeneo mengine ya mbali na Eden?

Kama walisafiri kutoka Eden, kwanini wasingekuwa wanawasiliana kwa safari mbali mbali? kwanini Columbus aseme aligundua Dunia mpya?....Kuna uwezekano wa binadamu kutokuwa na chanzo kimoja.
 
Abel alimuoa pacha wa Kaini na Kaini alitakiwa amuoe pacha wa Abel ndipo Kaini akakataa kwani pacha wake alikuwa mzuri sana kuliko pacha wa Abel.Baada ya mzozo Adam akapewa maelekezo na Mwenyezi Mungu waandae sadaka na yayule itakayochukuliwa atakuwa imekubaliwa.Sadaka ya Abel ilikubaliwa na Kaini alikasirishwa sana na kuahidi lazima atamwangamiza Abel.Kaini alipewa mbinu na Shetani ya kumuua Abel na akamuua.Abeli akawa ndiyo mtu wa kwanza kuuwawa na Kaini akawa mtu wa kwanza kua.
 
Mkuu wakati nilipojiuliza hili swali, niliona nadharia ya uumbaji ni uongo...Kama chanzo cha watu ilikuwa Eden, ni teknolojia ipi iliyotumika kusambaza watu kwenda mabara mengine? watu walifikaje Peru, Chile Madagascar na maeneo mengine ya mbali na Eden?

Kama walisafiri kutoka Eden, kwanini wasingekuwa wanawasiliana kwa safari mbali mbali? kwanini Columbus aseme aligundua Dunia mpya?....Kuna uwezekano wa binadamu kutokuwa na chanzo kimoja.
it doesnt make sense kabisa. na ukiuliza asili nyingine za binadamu zimetoka wapi wanakupa majibu ambayo sources zake ni unbiblical.. kama bible ni kitabu kikamilifu kwanini wasifanye reference humo humo?

inasikitisha kumuona mtanzania anajiita mwana wa israel na wale wasio wakristo kuitwa watu wa misri.. halafu yupo serius kabisa anajiita mtu wa taifa teule.
 
Nilisikia walizaa mapacha wa kike na kiume kwa hiyo wakaoana kwa kubadilishana yaani mfano amuoe pacha wa abeli na ukiziangatia zamani hawakuhesabu wanawake. Mi mwenyewe sijui ila nimejibu kutokana na kusoma huhkuhuku JF.
Ulisikia kutoka kwa nani,??
 
it doesnt make sense kabisa. na ukiuliza asili nyingine za binadamu zimetoka wapi wanakupa majibu ambayo sources zake ni unbiblical.. kama bible ni kitabu kikamilifu kwanini wasifanye reference humo humo?

inasikitisha kumuona mtanzania anajiita mwana wa israel na wale wasio wakristo kuitwa watu wa misri.. halafu yupo serius kabisa anajiita mtu wa taifa teule.
Ndio utumwa huo....wakati wa vita vya Palestine na Israel watanzania walisapoti Israel wakisema piga wana wa kambo hao kisa ni waarabu.....Sasa wale wana damu ya Abraham unawaita watoto wa kambo, wewe ambaye hata evolution hujamaliza unatumia kigezo gani kujiita mwana halali?....kiroho?...kweli watu wapo mbali na wao wenyewe.
 
aliumbaje watu wengi?
duniani kuna races 4 ambavo zinaweza kuwa divided into more 3o gorups ambazo ni caucasian, mongoloid or asian, negroid or black and australoid. na hizi races zote haziweza toka kwa wat wawili tu.
 
Inawezekana! Kama ilikuaje kuaje mpaka watu weusi tukatokea?
ndio kuna races 4 tofauti duniani kama caucasian, mongoloid or asian, negroid or black and australoid. hizi haziwezi tokana na watu wawili
 
Ndio ubaya wa story za kutunga....mara nyingi zinaishia hewani pasipo na majibu ya maswali yatakayo ibuka....kama Mungu ndiye aliyeumba watu basi angeumba wanawake na wanaume wakutosha ili wasizalishane ndugu kwa ndugu.....na kama aliruhusu ndugu kuzaliana, kwa nini akataze sasa hivi???
Una maswali marahisi ajabu.Tatizo kila kitu mnatumia mantiki.

Wale walikuwa wanazaliwa wawili,dada na kaka wa kwanza kisha dada na kaka wa pili.Yule ambaye alizaliwa na dada yake wa kwanza pamoja anaozeshwa na dada wa uzao wa pili.Kwahiyo kila kitu kina jibu na kiko wazi.

Lakini Allah anafanya mambo na kuumba atakayo na kuwekea utaratibu na sheria vile alivyoviumba.Mathalani sheria ya torati si sheria ya injili wala si sheria ya zaburi wala si sheria ya Qur'an isipokuwa iwe imewafikiana na Qur'an.

Unapouliza swali hilo pia uulize swali la mbona kuna viumbe wengine wameubwa bila mama wala baba na mwengine ameumbwa bila baba na sisi tumekuwa zao la baba na mama ?

Sababu Allah aliyetukuka ni mjuzi wa kupangilia mambo na mjuzi wa kuumba na kuweka taratibu ameamua kufanya vile anavyotaka.

Leo hii kuna kifo na kuna uhai na kila nafsi amesema itaonja umauti,sasa wale Mulhidi(Wakana Mungu) wakatae kufa au waseme kufa hakupo.Maana yeye aliyetuumba ameshasema na hiyo ndio sheria na angetaka angeumba uhai peke yake lakini ameamua kuumba uwili,yaani kifo na uhai,ili atupe mtihani kwamba ni wakina nani wataamini na kina nani hawataamini.

Kwahiyo muwe mnatumia akili akili zenu kuhoki kuliko tukuka sio zile zenu eti kama A ni 2 na B ni mbili basi A ni B.Upuuzi mtupu.

Ajabu iliyoje sisi tunaoamini uwepo wake na sheria zake nafsi zetu zimetulizana na majibu tunayo.

Tatizo vijana nyinyi wa leo mnafikiria kama wakubwa zenu waliofikiria wale wakina Socrates,Thalesi,Homeri,Anaksimenes,Anaksimanada,Demokretus,Zeno wa Abdela,Plato,Pythagoras na wasio kuwa wao.Wao wamekosewa na nyinyi mnakosea kama wao.

Kuna tatizo pia huwa naliona kwenu huwa mnauliza maswali ya kitoto mnajibiwa na nyinyi mkiulizwa maswali huwa hamjibu bali hamuwezi kujibu,hili ni tatizo kubwa.

Msingi wenu ni nadharia na majaribio(Experimental data),huu ujinga sisi tulitahadharishwa nao zamani.Kwanini vipimo vyenu haviendi bila nadharia na kuchukulia (Assumptions) ? Soma mkasa wenu juu ya Orbits.

Halafu huwa nakushangaa wewe bado upo katika zile zama ambazo wanasayansi walikuwa walikuwa wakana Mungu,wenzako leo hii wamekubali uwepo wake na wakasema ndio msingi wa mambo yote.

Kwahiyo Mola muumba anafanya vile anavyotaka tena kwa bora uliopea nafanowe hakuna.
 
M nmesoma sehem flan inasemekana Adamu na Eva walikuwa na watoto wengine wengi zaidi so hao walioana kaka na Dada zao
 
Ndio utumwa huo....wakati wa vita vya Palestine na Israel watanzania walisapoti Israel wakisema piga wana wa kambo hao kisa ni waarabu.....Sasa wale wana damu ya Abraham unawaita watoto wa kambo, wewe ambaye hata evolution hujamaliza unatumia kigezo gani kujiita mwana halali?....kiroho?...kweli watu wapo mbali na wao wenyewe.

ukifikiria deep hata kusema sisi ni wanadamu napo tunakosea.. sababu neno binadamu linatokana na neno Bin Adam >>> mwana wa Adamu >>> mwanadamu.

mkuu, our whole life is a lie.
 
ukinipa source nyingine manake biblia haina hizi info zaidi ya story ya adam ba hawa ambayo haileti maana. unakubali kwamba biblia haijitoshelezi?
Yah haijitoshelezi na ndio maana kunakuwa na maswali mengi yanayowachanganya watu isitoshe ni historia inayowahusu taifa fulani
 
Swali jepesi sana.iko hivi
Adam na hawa hawakuwa watu halisi kama tulivyo mimi na wewe bali yalikuwa ni majina ambayo yalitumika kuwakilisha makundi ya watu.so Adam alikuwa anawakilisha wanaume na hawa alikuwa anawakilisha wanawake.lengo la kitabu cha mwanzo ni kuonyesha historia ya binadamu so isingewezekana kuzungumziwa namna kila mtu alivyopatikana so yakachaguliwa majina mawili ili yawe vielelezo au kuwakilisha makundi hayo ya watu.ukisoma vizuri kitabu chenyewe kinajieleza mfano habari ya nyoka kuongea unaona kabisa kwamba No kitu ambacho hakileti maana.so mwandishi wa kitabu kile alitumia majina ya adamu na hawa kwa maana hizo.mfano mzuri ni hadithi za sungura na fisi ambazo hutumia majina hayo kuwakilisha watu halisi.
UONGO ULIOCHUPA MIPAKA.Naona umeona haingii akilini kuambiwa nyoka aliongea basi mpaka jiwe liliongea Mzee.Hapo utauliza vipi liongee hali halina mdomo.Na mimi nitakujibu kwani kila chenye mdomo huongea na kwani kila kisicho na mdomo hakiongei?

Hapo ndipo utakapoona ujuzi wa Allah.
 
Yah haijitoshelezi na ndio maana kunakuwa na maswali mengi yanayowachanganya watu isitoshe ni historia inayowahusu taifa fulani

ni historia au hadithi zinazowahusu waisraeli..

MATAYO. 19:28
Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.

hapo unaona hio hukumu itatolewa kwa kabila kumi na mbili za israeli, cha kushangaza unamkuta mndengeleko kama mimi na ye anajihesabia ni mmoja wa makabila hayo wakati yeye ni mndengeleko na mama ni mfipa.. wapi na wapi na kabila 12 za israeli.

hatari sana.
 
Back
Top Bottom