ShyaRuwa
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 7,895
- 13,643
Kwahiyo huu ujinga ndio mnaomezeshwa?Una maswali marahisi ajabu.Tatizo kila kitu mnatumia mantiki.
Wale walikuwa wanazaliwa wawili,dada na kaka wa kwanza kisha dada na kaka wa pili.Yule ambaye alizaliwa na dada yake wa kwanza pamoja anaozeshwa na dada wa uzao wa pili.Kwahiyo kila kitu kina jibu na kiko wazi.
Lakini Allah anafanya mambo na kuumba atakayo na kuwekea utaratibu na sheria vile alivyoviumba.Mathalani sheria ya torati si sheria ya injili wala si sheria ya zaburi wala si sheria ya Qur'an isipokuwa iwe imewafikiana na Qur'an.
Unapouliza swali hilo pia uulize swali la mbona kuna viumbe wengine wameubwa bila mama wala baba na mwengine ameumbwa bila baba na sisi tumekuwa zao la baba na mama ?
Sababu Allah aliyetukuka ni mjuzi wa kupangilia mambo na mjuzi wa kuumba na kuweka taratibu ameamua kufanya vile anavyotaka.
Leo hii kuna kifo na kuna uhai na kila nafsi amesema itaonja umauti,sasa wale Mulhidi(Wakana Mungu) wakatae kufa au waseme kufa hakupo.Maana yeye aliyetuumba ameshasema na hiyo ndio sheria na angetaka angeumba uhai peke yake lakini ameamua kuumba uwili,yaani kifo na uhai,ili atupe mtihani kwamba ni wakina nani wataamini na kina nani hawataamini.
Kwahiyo muwe mnatumia akili akili zenu kuhoki kuliko tukuka sio zile zenu eti kama A ni 2 na B ni mbili basi A ni B.Upuuzi mtupu.
Ajabu iliyoje sisi tunaoamini uwepo wake na sheria zake nafsi zetu zimetulizana na majibu tunayo.
Tatizo vijana nyinyi wa leo mnafikiria kama wakubwa zenu waliofikiria wale wakina Socrates,Thalesi,Homeri,Anaksimenes,Anaksimanada,Demokretus,Zeno wa Abdela,Plato,Pythagoras na wasio kuwa wao.Wao wamekosewa na nyinyi mnakosea kama wao.
Kuna tatizo pia huwa naliona kwenu huwa mnauliza maswali ya kitoto mnajibiwa na nyinyi mkiulizwa maswali huwa hamjibu bali hamuwezi kujibu,hili ni tatizo kubwa.
Msingi wenu ni nadharia na majaribio(Experimental data),huu ujinga sisi tulitahadharishwa nao zamani.Kwanini vipimo vyenu haviendi bila nadharia na kuchukulia (Assumptions) ? Soma mkasa wenu juu ya Orbits.
Halafu huwa nakushangaa wewe bado upo katika zile zama ambazo wanasayansi walikuwa walikuwa wakana Mungu,wenzako leo hii wamekubali uwepo wake na wakasema ndio msingi wa mambo yote.
Kwahiyo Mola muumba anafanya vile anavyotaka tena kwa bora uliopea nafanowe hakuna.
Una ushahidi gan kwamba Allah ndiye aliyetuumba?
Una ushahidi gani wa kuwepo kwa Allah?
Umesema kila mtu na Dada yake wa kuzaa nae, majina yao ni yepi?
Kama Mungu anafanya atakavyo yeye bila kushirikisha wanadamu, ina maana yeye ni dictator?