Binadamu wa kwanza kuumbwa Na Mungu ni Adam Na Hawa.Watoto waliowazaa ni Abel Na Kaini.Abeli Na Kaini walioa je Wake zao ni kizazi cha nani?
Nimesoma mjadala wa hoja yako unavyoendelea, nimebaki na mshangao na kujiuliza, hivi swali ni la kidini, kisayansi au kihistoria!
Mwuliza swali "mwembemdogo" sina uhakika wewe ni mwumini wa dini na dini ipi, ila kwa kuwa umegusa maandiko ya dini, kutoka Biblia, nakujibu kwa Biblia hiyo hiyo.
Hivyo basi waumini wa dini na watetezi wa maandiko ya Biblia wanaamini hilo. Ni wazi kwamba mke wa Kaini au Abeli walikuwa wa ukoo wa Adamu na Hawa; kitabu cha Biblia "Mwanzo 4:1-2 Adamu akamjua Hawa mkewe; akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanaume kwa BWANA. Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi.... Mwanzo 5:1 Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu akimfanya".
Kitabu cha Mwanzo 5 kinatoa orodha ya vivazi vya Adamu na Hawa - ni vizuri kusoma. Ila kabla sijajibu swali la msingi, ni vizuri kuyaeleza maandiko matakatifu ya Biblia.
1) Tunasoma Waraka 1 wa Paulo kwa Wakorintho 15:45: -Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha".
Maana yake Mungu hakuumba kundi la wanadamu bali binadamu wametokana na mwanamme na mwanamke mmoja - Adamu na Hawa.
2) Waraka wa Paulo kwa Warumi 5:12 - "Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi".
Kifungu hicho kinadhihirisha wazi kwamba ni vizazi vya Adamu na Hawa TU ndivyo vinaweza kuondolewa dhambi aliyoitenda Adamu. Dhambi ya mauti, aliyopewa Adamu kwa kuasi amri ya Mungu, pia ilirithiwa na vizazi vyake.
Soma kitabu cha Biblia Mwanzo 3 hasa 17 "Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako"; Mwanzo 3:19 - kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbuni utarudi".
3) Kwa sababu Adamu aliadhibiwa dhambi hiyo kwa mauti, uzao wote wa Adamu hulipa kwa mauti. Hata hivyo, Biblia inafundisha kwamba "kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, Waraka wa Paulo kwa Warumi 2:23". Je, jibu lake ni lipi?
4)Mtume Paulo kwenye Waraka wake 1 kwa Wakorintho 15 kwamba Mungu alimuumba Adamu mwingine kwa sura yake, Yesu mwana wa Mungu, ambaye hakuwa na dhambi yoyote, soma "1Wakorintho 15:45 - Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha".
Kwa sababu ya dhambi ya Adamu na Hawa, binadamu wamerithi adhabu walizopewa hao watu wa kwanza. Siyo kifo tu bali hata kuzaliana, soma kitabu cha Biblia cha Mwanzo 3:16 - Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto ; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala".
Tuzingatia maandiko, bila chuki yoyote binafsi, kuingiza siasa, au mawazo yoyote ya ziada ya Biblia, tukirudi mwanzo wa uumbaji, wakati kulikuwa na kizazi cha kwanza, ndugu wangeona (dada na kaka)la sivyo kusingekuwapo na vizazi zaidi. Yote haya yamesababishwa na Mtu wa kwanza, Adamu.
Watu wengi hukataa hitimisho kwamba watoto wa Adamu na Hawa walioana, kwa misingi ya sheria ya binadamu inayokataza umbu kuoana. Lakini usipoana na ndugu hutooa binadamu! Wote ni uzao wa Adamu na Hawa, wote ni wa damu moja na Hawa akiwa aneumbwa ubavuni mwa Adamu.
Sheria inayokataza ndoa kati ya ndugu wa karibu haikuwepo hadi wakati wa Nabii Musa (Mambo ya Walawi 18:20 - usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye". Maana yake awali hakukuwa na uasi wa sheria ya Mungu (Kitabu cha Nwanzo 1 na 2) kuhusu ndoa na ndugu wa karibu (hata ndugu na dada).
Lakini leo kwa sababu ya ugunduzi wa vinasaba, kuona ndugu kwa dungu kunaongeza uwezekano wa kuongezeka kwa vizazi vyenye ulemavu. Adamu na hawa waliumbwa bila chembechembe zozote zenye hitilafu. Kila alichoumba Mungu kilikuwa bora na imara (Mwanzo 1:31 - Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita".
Binadamu wa kwanza kuumbwa Na Mungu ni Adam Na Hawa.Watoto waliowazaa ni Abel Na Kaini.Abeli Na Kaini walioa je Wake zao ni kizazi cha nani?