Absalom Kibanda: Sasa sitaogopa kitu na sina cha kupoteza, nitafichua kila kitu

Kibanda kafunguka na ukweli umefichuka...magaidi wabaki uchi!

  1. Amesema yako matukio mengi yalitangulia ya kuwadhuru waandishi wa habari kabla yake yeye.
  2. Amesema wiki mbili kabla ya kutekwa aliwahi kuliona gari la taasisi moja limepaki na kuanza kumfuatilia.
  3. Aliwahi kutahadharishwa na mtu toka taasisi nyeti ya taifa hili kuhusu msimamo wake katika maswala ya taifa.
  4. Amesema viongozi wengi wa serikali wamefanya jitihada kubwa katika kukwepesha ukweli wa yaliyomkuta.
  5. Amesema vyombo vya dola vimetumika katika kupotosha ukweli wa matukio ya aina hiyo.
  6. Amesema amepata faraja kuwa wapo viongozi wa ulinzi wa usalama wastaafu wanafuatilia.
  7. Amedai kama alivyowahi kulialia Pinda kuwa nchini kuna watu wahalifu wenye nguvu zaidi ya dola, hawakamatiki!
Asante sana Absalom Kibanda, kama kawaida ya binadamu wapo wanaosubiri chakula wawekewe mezani na hata baada ya hivyo, walishwe. Wapo pia ambao baada ya kulishwa wanashindwa kutafuna na kumeza, hao kwa kweli na bila kutafuna maneno ni wagonjwa mahututi, miili na akili imepooza!
 
Kwa nchi maskini kama Tanzania kauli za "Tunamuachia Mungu" zimekuwa za kawaida, si kwa watu wa kawaida tu bali hata kwa viongozi wa kisiasa,.. na hata katika matamushi ya kiserikali. Hata raisi anapenda hiyo kauli. hii ni dalili ya kukata tama na "kufikia ukomo wa kufikiri". Hii ni dalili tosha kabisa kuwa kukuwa kwa DEMOKRASIA kutachukua muda mrefu sana! Na hicho ndicho kikwazo kikubwa kwa maendeleo katika nchi yetu!

Ni jukumu la raia wote kuiwajibisha serikali na chama tawala na siyo kuwaachia baadhi ya watu ama taasisi na asasi zisizo za kiserikali. Otherwise..tutaendelea kumwachia Mungu sana!
 
kwani baada ya kile kitu cha mlipuko kwenye mkutano wa chadema Arusha, reaction ya serikali ilikuwa ni nini? Kibanda aache kuuma maneno

Ndiyo maana mh. Mbowe hakuuma maneno. Ukianza kusema 'nitasema', basi umekwisha. Taja, tamka wazi ili wahusika wabaki kuhangaika kuijinasua, na hapo watakuogopa. Kwa sasa Kibanda anawezamalizwa na ikaishia hapo basi. Anatakiwa aonyeshe hasira!
 
Anasema alipolazwa hospitalini nchini Afrika Kusini serikali ilimtuma mtu mmoja kwenda kuona maendeleo yake. Uongozi wa hospitali uliamua kumficha ili kunusuru maisha yake.
 
jamani maumivu ya kung'olewa kucha na meno na kutobolewa jicho bila ganzi si mchezo. Anasema sasa ana ujasiri upi? Anajua fika kuwa wahusika wako juu ya sheria wakimtaka wanampata. Hii nchi jamani!!
 
Baada ya mkasa uliompata na mateso aliyoyapata,ndugu Kibanda amesema hata ogopa chochote Sasa kwasababu hana cha kupoteza ataandika mabaya yote anayoyajua.

kumbe alikuwa anaficha?????hili ndilo tatizo la wanahabari wa tanzania.wanaficha habari muhimu.BADILIKENI SASA.
 
kibanda mungu akupe afya njema uweze kuwa shushua hawa magamba na lameck wao.
 

Hapa naanza kupata kapicha kidogo
1. Mahusiano ya Mwigulu na Rudovick,
2. Mwigulu kusema anaomkanda unaoonyesha Viongozi wa CDM wakipanga mauaji,
3. Siku Kibanda anatekwa naye Rudovick kusingizia katekwa pia.
4. Mwigulu kumtumia Rudovick kumrecord Lwakatare
5. Kukamatwa kwa Lwakatare kuhusishwa na kesi ya kutaka kuteka na kumzuru Denis

Nahitimisha kwa kusema wahusika wameishaanza kuanikwa - Rudovick, Mwigulu, Usalama wa Taifa na vyombo vingine vya usalama Lengo ni kuihusisha CHADEMA na matukio yote haya lakini kwa maneno haya ya Kibanda ukweli unaanza kujulikana na ndo maana CDM wamekaa mbali sana na Rudovick.
 
Haya ... hata akisema mhusika ni Mr ABCD mtafanya nini? Kwa sababu watanzania ni mafundi sana wa maneno lakini utendaji unakuwa sifuri. Wale waliotaka kumuua Dr Ulimboka mbona wanajulikana? Wananchi walifanya nini? Kazi kuangalia kama sinema tu!

Asiwe mwongo!
 

Yaani true !!halafu yeye haogopi kama watu wanamteka akili,na amekili ni watu wakubwa ambao wanaweza hata ingilia upelelezi,my take ni kwamba huu ndo wasaa wa kibanda kumtaja vinginevyo watamuua kwa sababu hawezi na hana uwezo wa kuwatishia(kuwa threat) kwa mtandao kama huo,kwa hilo namshauri aendelee kutembea na ganzi

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Aseme aliye mteka kabla hawajammalizia
 
Washauri wa kisheria hawashauri kumuhudumia victim unless inataka kuonyesha unawajibika. Hata ukimgonga mtu na gari sio wajibu wako kumpatia matibabu. Serikali haiwajibiki kuwatibu waliotekwa unless makosa yalikuwa ya askari wake.
Inasikitisha' serikali hawakugharimikia matibabu,, kazi waliyoifanya ni uchunguzi...je, angepoteza maisha kwa kukosa huduma ya matibabu uchunguzi ungesaidia nini??
 

Mungu mwenyewe anakuambia jisaidie nami nitakusaidia, sasa wanamwachiaje angali hawajajisaidia kwa njia yoyote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…