BelindaJacob
Platinum Member
- Nov 24, 2008
- 6,474
- 4,039
Sijakimbia sheikh lakini nina wakati mgumu sana hapa nilipo.
kuna wachezaji wa Milan wamenisononesha saaana.
hakika Milan ni timu kipenzi changu na najivunia hilo.
Ila narudia KUNA WACHEZAJI WA MILAN WAMENISONONESHA MNO.
Dida, cafu, maldini, stam, nesta, gatusso, pirlo, ambro, ruicosta, crespo na seedorf...
Je ktk kikosi hicho nani ambae si old men? Na unajua kuwa ktk kikosi hicho Man aliparamiwa mara ngapi?Usikurupuke.
Unachotakiwa kufahamu ni kuwa kuna wachezaji wamefungisha leo.

Ninaifahamu na kuipenda kwa moyo wangu woote klabu ya AC Milan.
milan ni timu kubwa barani ulaya na kwa namna moja ama nyingine huwezi kuifananisha na Chelsea, Liverpool, Man UTD au Arsenal.
Milan ina mafanikio makubwa ktk medani ya soka kupita klabu hizo nilizozitaja hapo juu.
Milan kama Milan pia ni timu inayothamini wachezaji wenye umri mkubwa na ndio maana huwezi kusikia kuna chembe chembe yoyote ya utovu wa nidhamu.
ktk kipindi choote tangu nimeifahamu AC Milan sijawahi kuona imezidiwa ktk nafasi ya kiungo kama ilivyozidiwa leo haswa kipindi cha pili kilivyoanza mpk kocha alipokumbushwa na washabiki wenye uchungu waliokuwa wanaimba nyimbo za kuwatukuza watu kama Seedorf na Pippo kwa rugha ya kitaliano.
majonzi niliyonayo hapa ni wazi kuwa hata yule kocha wetu ambaye tunamuheshimu na ataendelea kuheshimika muheshimiwa Carlo Ancelotti atakuwa anayo pengine zaidi yangu.
Leo hii ukimuuliza Ancelotti ni kitu gani haswa kimeifungisha AC basi atakwambia ni mfumo uliopo sasa wa kubadili tamaduni za Milan za kuamini wazoefu.
Kwa miaka ya hivi karibuni ulimwengu ulishuhudia AC ile ya Ancelotti ikiifunga na kuitoa Manchester kila kukicha.
Na ukijaribu kuangalia utagundua Ancelotti amekuwa akijaza wakongwe wa Milan anbao wanajua nini uchungu wa kufungwa ktk chmps league.
Milan hiyo ilikuwa na mtu mwenye umri mdogo na mgeni Kaka tu, lakini alikuwa anazungukwa na kundi la wazoefu ambao mara zote walikuwa wanambeba...
hakika kitu kilichoifungisha milan leo ni upangaji mbovu wa timu yetu ambayo hasilani abadani HAIJAWAHI KUSAIDIWA AU KUTENDEWA WEMA NA WAGENI AU WATOTO AMBAO WANA HADHI YA NYOTA 4 KUSHUKA CHINI.
Hivyo ni wazi kuwa kama AC wangekuwa na viungo kama seedorf, gatusso, pirlo na ambrosini huku Dinho akipewa nafasi ya kuchezea mpira kisha mbele akapewa muda wa kutosha super pippo basi ktk thread hii ningetamba peke yangu na wageni ambao wangekuwa wanaingia kunipa hongera.
Hakika Watoto na wageni wametuua Milan.
Watoto wasiojua umuhimu wa kutumia nafasi unazozipata nyumbani wametuua.
Wachezaji wasiojua misingi ya milan wametuua.
Upangaji mbovu wa timu umetuua.
Inasononesha jamani, inasononesha
All in all hands shakes hongera sana Man UTD...
but msisahau final series itakayopigwa old traford ambayo itapewa jina la the return of Gatusso....
Naomba niwaage
Adios...
Forza Milan
Mkuu hope next time utafanya 'utafiti' zaidi kabla ya kuanzisha thread itakayokusonesha tena!All in all hands shakes hongera sana Man UTD...
but msisahau final series itakayopigwa old traford ambayo itapewa jina la the return of Gatusso....
Naomba niwaage
Adios...
Forza Milan
'AC 3 MAN U 2'...........Shekhe Yahaya
utabiri mzuri....kama ilivyo kwa sheikh yahya, utabiri huwa kinyumenyume kama ngadu vile....final whistle: Milan 2: ManU 3
All in all hands shakes hongera sana Man UTD...
but msisahau final series itakayopigwa old traford ambayo itapewa jina la the return of Gatusso....
Naomba niwaage
Adios...
Forza Milan
Wazee wa AC Milan wasingeweza kukimbizana na muziki mnene wa mashetani wekundu.Wasubiri kichapo kingine Old trafford,Vidic atakuwa tayari ameshapona hakutakuwa na makosa ya kijinga yaliyofanywa na Evans,upande wa kulia atacheza Wes Brown kuondoa kitisho cha Gaucho.
Sir Alex tayari keshaguandua jinsi ya kuidhibiti timu ya wazee.