‘Acha kazi nitakutunza’ imeliza wengi

‘Acha kazi nitakutunza’ imeliza wengi

Yaani wazazi wanajipinda kumpa binti yao elimu bora toka shule ya msingi mpaka chuo kikuu, tena unakuta wazazi wengine wanalipa ada mpaka ya chuo ili binti yao asisumbuke na mkopo, binti kapata kazi na uko kazini anatokea msela anamuahidi ndoa alafu eti anamwambia aache kazi amfungulie MPESA. Aise hii inauma sana sio kwa binti tu bali wazazi waliogharamia elimu ya huyo binti. Wakati huo huo kama mzazi hana kipato na binti kapata mchumba wakati bado anahitaji elimu utasikia wanasema mchumba hasomeshwi. Mabinti kiukweli wananyanyasika.
 
Ndio maana dunia ya sasa ndoa za kweli hakuna , mke anaishi huko na mume huko kisa kazi bora muachane .
 
Yaani usomeshe mtoto toka Chekechea Hadi chuo.
Ufanye juhudi hadi apate kazi, alaf atokee jamaa falani huko anaye sema anampenda kupita watu wote duniani.
Amwachishe hiyo kazi na kuwa mama wa nyumbani na amtegemee yeye.
Halafu akubaliwe, Binti aache kazi.
Hapa inamaanisha shule yake yote inarudi kuwa sifuri.
Binti anarudi kuwa omba omba tena.
Vipi huyo mwenye kutegemewa akipatwa na umauti
Vipi wakiachana
Vipi akianza kuteswa na kunyanyaswa.
Ukisikia mtu kuwa Mpumbavu basi wamojawapo ni aina ya hao mabinti.
 
Back
Top Bottom