Acha kupoteza muda wako kuandika nyuzi zifuatazo, utakuwa maskini milele!

Acha kupoteza muda wako kuandika nyuzi zifuatazo, utakuwa maskini milele!

Thibitisha utafiti wako, vinginevyo Andiko hili linakuhusu:
Ufunuo 21:8
Lakini watu waoga, wasioamini, wapotovu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, na waongo wote, mahali pao patakuwa ndani ya lile ziwa linalowaka moto na madini ya kiberiti; hicho ndicho kifo cha pili.
Umeolewa mrembo?
 
Wengine huja mitandao ku refresh mind baada ya kazi ngumu za kusaka fedha,sio kila mtu kipato chake kinategemea social platforms moja kwa moja so kumpangia mtu huyo kitu cha kuandika ni kama kumpigia kelele.
 
True kama kuna mtu anategemea kitu cha maana kwenye mitandao atakua hajitambui , huku ni porojo Tu real life kila mmoja atajijua anafanyaje
 
Waefeso 5:15-16
"Jihadharini, basi, jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima, bali kama wenye hekima; mkiukomboa wakati, kwa maana zamani hizi ni za uovu."
Ulikuwa umesahau
 
Nimeishaona, mkuu. Nimegusa kwenye mshono. Wamenivamia kama nyuki kwa hasira. Ingekuwa tunaonana "live" habari ya mjini ingekuwa "Setfree abondwa kwa mawe na wananchi wenye hasira"
Nawasamehe bure kwa kuwa hawajui walitendalo

Luka 23:34
"...Baba, wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo!”
Ngoja waje bado huyu Tlaatlaah
 
Umeolewa mrembo?
Mimi ni bibi Arusi wa Yesu
Ufunuo 19:7-8
Tufurahi na kushangilia; tumtukuze, kwani wakati wa harusi ya Mwanakondoo umefika, na bibi arusi yuko tayari. Amepewa uwezo wa kujivalia nguo ya kitani safi, iliyotakata na yenye kung'aa!” (Nguo hiyo ya kitani safi ni matendo mema ya watakatifu).
 
kuna nini gentleman, mbona weo? :pedroP:
Hujaona, mkuu? Watu wamekasirika kama mbogo. Nisaidie kuwasomea:
Mhubiri 7:9
Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.
 
Wengine huja mitandao ku refresh mind baada ya kazi ngumu za kusaka fedha,sio kila mtu kipato chake kinategemea social platforms moja kwa moja so kumpangia mtu huyo kitu cha kuandika ni kama kumpigia kelele.
No, please. Sikubaliani na wewe. Kuna vijana wanatafuta "nondo" humu zitakazowakwamua kiuchumi. Sasa kama mtu amepiga pesa mchana kutwa halafu anakuja humu ku-refresh kwa kuandika hekaya za Abunuwas, si anawapunguzia maskini hata kidogo walicho nacho?
Si ni bora kuandika hata vifungu vya Biblia kama hiki 👇 kinachotoa faraja kwa maskini
Zaburi 34:6
Maskini huyu alimwita Mwenyezi Mungu, naye akamsikia, akamwokoa katika taabu zake zote.

Maskini wanaomuomba Mungu kwa imani, Mungu anawasikia na kuwatoa katika taabu zao.
 
Back
Top Bottom