Acha kupoteza muda wako kuandika nyuzi zifuatazo, utakuwa maskini milele!

Acha kupoteza muda wako kuandika nyuzi zifuatazo, utakuwa maskini milele!

Kama wewe ni mtoto wa Elon Musk, usisome uzi huu, haukufai!

Kila siku, vijana wengi wanatumia muda mwingi kuandika nyuzi mitandaoni kuhusu mambo yasiyo na faida kwa maisha yao ya baadaye. Kwa mfano mtu anaandika uzi wenye kichwa: “Bibi yako alikuwa na vidole vingapi?” Wengine wanazungumzia drama za mastaa, utani wa kisiasa, na mijadala isiyowasaidia kupata maarifa au fursa za kiuchumi. Matokeo yake? Miaka inasonga mbele, wao wanabaki pale pale—bila maendeleo yoyote!

Una muda wa kuandika threads, lakini huna muda wa kujifunza? Utajuta!
Watu wanaofanikiwa hutumia muda wao kujifunza ujuzi mpya, kusoma vitabu, au kutafuta maarifa yanayoweza kubadili maisha yao. Kama wewe unatumia masaa matatu kuandika threads za utani, lakini huna hata dakika 30 za kusoma kuhusu biashara, uwekezaji, au ujuzi unaoweza kukuletea kipato, basi jiandae kwa maisha ya majuto baadaye!

Ukweli ni kwamba, muda unaotumia mtandaoni unaweza kuwa mtaji wa kukuongezea maarifa au chanzo cha kufeli kimaisha. Jiulize: miaka mitano kutoka sasa, utaweza kuangalia nyuma na kusema, "Nilijifunza kitu JF kilichoniletea kipato?" au utajilaumu ulipoteza muda kwenye mijadala isiyo na tija?

Badala ya kupiga kelele mitandaoni, tumia muda mwingi kujifunza pesa inapatikana vipi!
Leo hii, kuna vijana wadogo huko China wanaojifunza ujuzi wa digital marketing, coding, graphic design, forex, na mbinu za ujasiriamali. Wengine wanajifunza kutengeneza bidhaa au kuuza huduma mtandaoni. Hawa ndio watakaokuongoza kesho! Ukiendelea kuandika threads zenye vichwa kama hivi: “Bibi yako na babu yako walikuwa na macho mangapi?” jiandae kuwa mteja wa Wachina!

Usinielewe vibaya—kuandika mitandaoni sio vibaya, lakini jiulize: je, unachoandika kitakusaidia kwa namna yoyote kifedha au kielimu? Kama jibu ni hapana, basi unajidanganya! Badala ya kuandika threads zinazokukaushia MBs zako tu, afadhali uandike mada yenye maswali yatakayokusaidia kupata majibu ya kukuletea mafanikio ya kiuchumi. Badala ya kufuatilia skendo za watu maarufu, fuatilia mbinu za uwekezaji.

Kijana amka! Fanya bidii kutafuta maarifa yatakayokusaidia kujenga nyumba yako au kununua gari lako. Au unataka tu “likes” nyingi? Kama “likes” zitakusaidia kununua chips mayai, sawa, endelea kuzitafuta!

Muda ni mali. Acha kupoteza muda wako kuandika threads zisizo na maana, utakuwa maskini milele! Utakuwa maskini milele, sio tu kwa sababu unapoteza muda wako kufanya vitu visivyo na faida, bali pia kwa sababu hutaki hata kutumia muda wako kujifunza Biblia—kitabu kinachoweza kukuongoza na kukupa hekima ya kweli. Maisha haya yana mwisho, unachokifanya leo kitaamua hatima yako, sio tu duniani bali hata milele!

“Time is a coin you can spend only once. Make sure you spend it wisely." – Carl Sandburg
Kufanya kazi sana siyo kufanikiwa sana
Haya maisha hayahitaji userious sana
 
Vifungu mkuu hawa watu wanatoa Sana ushauri kwa wengine ni wale walioshindwa lakini wanaigiza wako perfect, htumskia tajiri kama Mo , GSM , Bakhresa anatoa ushauri
Sio kweli. Trump anamcha Mungu na hajashindwa. Huoni alivyoshauri misaada ikatwe ili watu waamke waanze kujitegemea

Soma vifungu hivi utaona umuhimu wa kuwasaidia wengine hata tu kwa kuwapa ushauri
Methali 3:27
Usimnyime mtu anayehitaji msaada, ikiwa unao uwezo wa kufanya hivyo.

Methali 19:17
Anayemsaidia maskini anamkopesha Mwenyezi-Mungu; Mwenyezi-Mungu atamlipa kwa tendo lake jema.

Mungu anahesabu msaada anaoutoa mtu kwa maskini kama mkopo kwake, na Mungu atamlipa mtoa msaada.
 
Huu ushauri wa leo huoni nimejitoa kwa ajili yako, mkuu.
Kuandika maneno yote hayo kwa mpangilio unaoeleweka ni nini kama sio kujitoa.
Ongeza bidii kujitoa bado sijona...
 
wamesema upunguze ushauri jishauri mwenyewe
Kina nani hao waliokutuma useme uongo

Waefeso 4:25 ​

Kwa hiyo, acheni uongo. Kila mmoja anapaswa kumwambia mwenzake ukweli
 
Ignorance is Bliss...
Ukweli ni kuwa self transformation ni swala binafsi. Watanzania na waafrika kwa ujumla ndivyo tulivyo. Tamaduni zetu zinatufunga
 
Acha kutupangia maisha .
Acha kuwasemea wengine,kuna watu huu Uzi unaenda kutubadilisha sana,huyu muandishi wa huu Uzi asipingwe kabisa,wewe kama unajuwa kuupangilia mda wako basi ni vyema ila ukae ukijua kuna watu ni wahanga wa mitandao ya simu huu Uzi unawafaa sana.
 
Back
Top Bottom