DOKEZO Achana na kunguni, UDOM ina vyoo vichafu sijawahi kuona

DOKEZO Achana na kunguni, UDOM ina vyoo vichafu sijawahi kuona

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hawa wanafunzi wengi wao ni watoto wetu sisi wakulima uku. sisi uku vyoo yetu ni vya shimo vile vya kulenga.

Hayo mambo ya choo cha mzungu wameyakuta ukouko chuo na bahati mbaya mambo aya hakuna anaekufundisha, utafanya unavoweza au ulivozoea uko kwenu.

inabidi lazma wafundishwe matumizi (wapende wasipende) vinginevo iyo shida haiwezi kuisha.

uko maofisini kwenyewe tu kuna watu kibao wanapanda na viatu juu ya masinki ya choo cha kukaa sembuse uko shuleni.

wakusanywe ao wanafunzi wafundishwe matumizi sahh na usafi wa choo.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nimehitimu chuo kikuu cha dodoma hivi punde, lakini mazingira tuliyokuwa tunaishi pale chuoni hakika yanasikitisha.

Colleges nyingi za pale UDOM kuna changamoto kubwa ya usafi chooni na ukiachilia mbali suala la usafi ila maintenance kwenye vyoo vya UDOM ni hovyo kabisa. Wanafunzi wanalipa ada na kutimiza majukumu yao mengine ila nashangaa Sana kwanini uongozi hauzingatiii maeneo nyeti Kama maliwatoni.
Ukiwa mgeni ukaanza kutembea kwenye viunga mbalimbali kwa nje utavutiwa na majengo lakini ukiingia kwenye vyoo vya hosteli hali ni mbaya Sana. Yaani hadi hosteli zinanuka mikojo na mavimavi tu. Hii sio sawa hata kidogo na ni aibu kwa chuo kikubwa kama kile kushindwa kuhimili na kukarabati vyoo mara kwa mara.
Ukienda chooni kwanza sahau kuhusu kukuta maji, yaani maji ni hadi utoke hosteli uende kuchota mita kadhaa toka umbali wa hosteli zilipo upande ngazi na ndoo yako ndio ukanye au ukafanye mengine. Nahisi dada zetu huwa wanapata kadhia sana kuhusu usafi wao binafsi wanapotumia vyoo.

UDOM mnakera aisee, mmekanusha la kunguni na hili najua mtakanusha ila chuo chenu kina vyoo VICHAFU

"We embracing knowledge" knowledge my foot wakati hata knowledge ya kukarabati vyoo hamna.
Mkuu, umeshapata ajira?
 
Hicho ni choo cha stendi ya mabasi ya Katoro mkoani Geita. Unafikiri ni kwa nini wameamua kuandika hivyo?

Inawezekana Uongozi wa UDOM una mapungufu yake, lakini kwa vyoo kuwa vichafu si la uongozi wa Chuo pekee.

Suala la usafi wa vyoo bado ni changamoto kubwa sana Tanzania. Tabia ya usafi bado haijafikia viwango sahihi.
Hakika, Pia sehemu nyingi za kula za mabasi vyoo ni vichafu sana. Watu wanajisaidia hawaflashi, sabuni za kunawa za unga wamedailuti na maji, kwingine vyakula wanauzia njia za kwenda vyooni.
 
Wewe ulipokuwa Mwanafunzi ulifanya jitihada gani za kurekebisha hali hiyo,usije kuwa unatoa malalamiko maana Watanzania kwa malalamiko hatujambo kuchukua action kirekebisha hiyo hali.
 
Hawa wanafunzi wengi wao ni watoto wetu sisi wakulima uku. sisi uku vyoo yetu ni vya shimo vile vya kulenga.

Hayo mambo ya choo cha mzungu wameyakuta ukouko chuo na bahati mbaya mambo aya hakuna anaekufundisha, utafanya unavoweza au ulivozoea uko kwenu.

inabidi lazma wafundishwe matumizi (wapende wasipende) vinginevo iyo shida haiwezi kuisha.

uko maofisini kwenyewe tu kuna watu kibao wanapanda na viatu juu ya masinki ya choo cha kukaa sembuse uko shuleni.

wakusanywe ao wanafunzi wafundishwe matumizi sahh na usafi wa choo.
Wawekwe mgambo katika vyoo kukagua kila anayetoka chooni kama amesafisha vizuri.
 
Karibia vyuo vyote wapo hivo sio udom tu, baadhi ya wanavyuo wenyewe ni wachafu,nje wanavaa vizuri ila tabia zao sasa
Mkuu, kwani hao wanavyuo wametoka wapi? Nafikiri ungesema tu "Watanzania"

Kama upo jirani na Mwanza, tembelea vyoo vya stendi mpya ya Nyegezi. Utashangaa kwamba pamoja na kwamba vimeanza kutumika miezi ya hivi karibuni, baadhi vimeshaharibiwa.

Ingekuwa ni mamlaka yangu ingepitishwa sheria ya kila kaya kupewa semina maalum ya usafishaji na utumiaji vyoo kiusahihi.
 
Hilo la vyoo siyo UDOM tu ni Tanzania nzima, Mtanzania hana kabisa utamaduni wa kuweka usafi wa vyoo.

Elimu kubwa sana kwa vitendo inahitajika hapo.
Madam, upo sahihi, lakini kusema hiyo ni tabia ya "Mtanzania" utakuwa umekosea. Labda ungesema Watanzania wengi. Naamini wewe huna hiyo tabia.

Na kweli, mimi binafsi, kati ya mambo ambayo yamekuwa yakinikera, ni la vyoo kutokupewa hadhi stahiki. Inaonekana vyoo havipewi kipeumbele na Watanzania walio wengi.

Ndiyo maana unaweza ukamkuta mtu kajenga nyumba ya tofali akaezeka kwa bati na kusakafia, lakini choo akazungushia tumifuko tu, halafu mlangoni mwa choo akaweka gunia.

Kama mtu ameweza kuezeka nyumba kwa bati, angeshindwa kujenga kachoo kanakoendana na hadhi ya nyumba anayoimiliki?

Vyoo havipewi hadhi stahiki na Watanzania wengi.
 
Sio UDOM tu hata hapo UD kuna vyoo inabidi uvute pumzi ndio uingie kukojoa. Ukitoka unanuka harufu ya choo

Kuna hall 5 upande wa vyoo ilikuwa ni hatari kwa afya, maji ya mavi yalikuwa yanatiririka hovyohovyo

Sijajua miaka hii hali ikoje
 
Hizi tabia za kutojua matumizi ya vyoo wanafunzi wa vyuo wanatoka nazo shule za sekondari na msingi.
 
Kinachotakiwa na kuwekwa mgambo kusimamia matumizi sahihi ya vyoo.
Sio wawasimamie vizuri watu wa usafi mkuu

Kwa upande wa majengo ya accommodation waanze na warden na watu wake wa usafi wa jengo analosupervise

Maana warden ndio kama baba mwenye nyumba anayesimamia jengo linalitumiwa na wanafunzi
 
Kikweli vyuo vya binafsi kwa usafi wapo vzr sana mf Jordan University-Moro...Wafanyakazi wapo full time kufanya usafi kila baada ya masaa 3 au 4 kwa siku....
 
Tulikuwa hapo UDOM mwaka juzi kwenye kongamano la maombi ya kitaifa na Mwalimu Mwakasege,

Tulikuwa tunalala kwenye mabweni ya hicho chuo!
. Aisee tulkaa hapo wiki nzima ila muda wote nilishindwa kabisa kwenda kujisaidia kwenye vile vyoo humo ndani

Niliwaza sana, nikasema mtu mweusi ni laana.
Mtu wa maombi hapaswi kusema hivyo.
 
Nimehitimu chuo kikuu cha dodoma hivi punde, lakini mazingira tuliyokuwa tunaishi pale chuoni hakika yanasikitisha.

Colleges nyingi za pale UDOM kuna changamoto kubwa ya usafi chooni na ukiachilia mbali suala la usafi ila maintenance kwenye vyoo vya UDOM ni hovyo kabisa. Wanafunzi wanalipa ada na kutimiza majukumu yao mengine ila nashangaa Sana kwanini uongozi hauzingatiii maeneo nyeti Kama maliwatoni.
Ukiwa mgeni ukaanza kutembea kwenye viunga mbalimbali kwa nje utavutiwa na majengo lakini ukiingia kwenye vyoo vya hosteli hali ni mbaya Sana. Yaani hadi hosteli zinanuka mikojo na mavimavi tu. Hii sio sawa hata kidogo na ni aibu kwa chuo kikubwa kama kile kushindwa kuhimili na kukarabati vyoo mara kwa mara.
Ukienda chooni kwanza sahau kuhusu kukuta maji, yaani maji ni hadi utoke hosteli uende kuchota mita kadhaa toka umbali wa hosteli zilipo upande ngazi na ndoo yako ndio ukanye au ukafanye mengine. Nahisi dada zetu huwa wanapata kadhia sana kuhusu usafi wao binafsi wanapotumia vyoo.

UDOM mnakera aisee, mmekanusha la kunguni na hili najua mtakanusha ila chuo chenu kina vyoo VICHAFU

"We embracing knowledge" knowledge my foot wakati hata knowledge ya kukarabati vyoo hamna.
Yule mama yenu msemaji wa UDOM atakuja kukupinga vikali na kusema unasema haya wakati vyuo vimefungwa, subiri uone suala la KUNGUNI alipinga vikali kwamba mnachafua Jina la Chuo Sasa umeibuka huu uozo kuna vyuo ukienda chooni unatamani ubakie huko huko usitoke, chooni bafu maji bwelele
 
Back
Top Bottom