DOKEZO Achana na kunguni, UDOM ina vyoo vichafu sijawahi kuona

DOKEZO Achana na kunguni, UDOM ina vyoo vichafu sijawahi kuona

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Daah hii kitu uisikie tu ni hatariaz sana.

Haya mambo ya usafi na yenyewe sasa wayaingize kwenye orientation course mara mtu aking'aa viwanja vya chuo apigwe msasa haya mambo uenda ikasaidia.

nasema uongo wajameni?
Suala la mtu kuwa msafi au mchafu ni la kitabia, na tabia haijengwi kwa siku moja.

Akisubiriwa mpaka aende Chuoni ndipo akafundishwe matumizi sahihi ya vyoo, itakuwa too late.

Alau ungewekwa utaratibu watu waanze kifundishwa kuanzia darasa la kwanza, na kuwepo utaratibu maalum wa ufuatiliaji kuhakikisha kuwa wanayaishi hayo mafunzo.
 
Karibia vyuo vyote wapo hivo sio udom tu,
Uongo UONGO UONGO UONGO, kuna Chuo nikikupeleka chooni unaweza ukasema hiki sio choo, kuna vyoo vya kisasa hadi unaogopa na ni Chuo cha Serekali
 
Very true,,,
Nakwambia huyo jamàa hajui kuna vyuo vina vyoo vizuri na wale watu wa usafi wanapiga kazi kuhakikisha choo kinakua safi mda wote, alafu sio tu choo ni choo cha kisasa choo bafu la kisasa sio kulenga choo cha shimo sekondari primary, choo km wanatumia maofisa kumbe wanatumia wanafunzi

Ngoja siku nikienda Chuo kimoja nyarekodi video nije kutupia hapa najua kuna watu wataulizana hiki Chuo gani?
 
Watanzania wengi hawaja fikia level ya ustaarabu.

Na hii ni my own observation...

Waafrika hasa watanzania wana Asili ya uchafu karibu kila mahali.

Unaweza weka kila miundombinu ya usafi lakini ikaharibiwa au isitumiwe kabisa.
Uko sahihi kabisa mkuu!
 
Karibia vyuo vyote wapo hivo sio udom tu, baadhi ya wanavyuo wenyewe ni wachafu,nje wanavaa vizuri ila tabia zao sasa
Sahihi kabisa, nimesoma SUA, postgraduate aisee kuna watu unawaangalia unatikisa kichwa kwa masikitiko, Yani ni wachafu wachafu ajabu, anaenda chooni bila maji hata kidogo, aibuuu, kule maji yanasumbua Ila Kuna madumu tunachotea maji lazima uwe nayo room kwako Kuna wengine uchafu ni jadi yao, Pedi wanatupa hovyo hovyo PhD huyooo! Aiseee koridoooo inanuka mikojoooooooo jaman khaaaaa

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Mnauonea uongozi bure
Shida ni wanafunzi wenyewe wachafu.

Dada wa usafi anamaliza kufanya usafi,mtu anaenda tua mzigo wake pale..utadhani mtoto mchanga asiyejitambua.
Watu wanatupa uchafu hovyo, kwanini vyoo visizibe??

Kama kila mtu angetunza hivyo vyoo Kwa kuzingatia usafi
Kila mmoja angeenda chooni na maji ya kutosha , ile hali isingekuwepo .


Wanafunzi acheni uchafu.
Matatizo mengine yanatatulika na wanafunzi wenyewe.

Maji kutokutoka bombani bado si kigezo Cha mtu kutua mzigo wake na kuuacha..
Kavute maji kisimani
Kama huwezi basi katumie vyoo vya madarasani umalize mambo yako huko,, mara nyingi huwa na maji.
 
Uko sahihi kabisa mkuu!
Hilo suala sio la watanzania, ushaelewa hilo suala ni la uongozi wa Chuo wameajiri watu wa kufanya usafi wa vyoo kwanini vyoo vinakua vichafu, unasemaje watanzania kufanyaje?
 
Suala la mtu kuwa msafi au mchafu ni la kitabia, na tabia haijengwi kwa siku moja.

Akisubiriwa mpaka aende Chuoni ndipo akafundishwe matumizi sahihi ya vyoo, itakuwa too late.

Alau ungewekwa utaratibu watu waanze kifundishwa kuanzia darasa la kwanza, na kuwepo utaratibu maalum wa ufuatiliaji kuhakikisha kuwa wanayaishi hayo mafunzo.
mkuu shule zipi izo? kayumba nyingi wanafunzi zaidi ya 700 matundu ya choo ya kuhesabu.
 
Wanafunzi acheni uchafu.
Matatizo mengine yanatatulika na wanafunzi wenyewe.
Kwanini vyuo vingine vina vyoo visafi kwani havina wanafunzi? Tembea uone sio unakaa tu sehemu moja toka tembelea vyuo tofauti utajifunza jambo kila Chuo unachoingia omba wakuelekeze choo kilipo ukaduwae chooni
 
Kwenye Orientation vijana wafundishwe,ila Watanzania wengi ustaraabu hawana.Utunzaji wa vitu F
Wanafundishwa ila watu ni wapumbavu
Mtu anatua zigo lake analiacha.

Mtu anaenda oshea chombo chake kwenye sink la kunawa, na anamwaga mabaki ya chakula.

Halafu uje ulalamikie uongozi kweli!

Udom wanafunzi wameendekeza uchafu.
 
Wanafundishwa ila watu ni wapumbavu
Mtu anatua zigo lake analiacha.

Mtu anaenda oshea chombo chake kwenye sink la kunawa, na anamwaga mabaki ya chakula.

Halafu uje ulalamikie uongozi kweli!

Udom wanafunzi wameendekeza uchafu.
Mboni vyuo vingine visafi hakuna wanafunzi? Au wanafunzi wa UDOM wanatoka Nchi gani? Msituchanganye hapa
 
Kwanini vyuo vingine vina vyoo visafi kwani havina wanafunzi? Tembea uone sio unakaa tu sehemu moja toka tembelea vyuo tofauti utajifunza jambo kila Chuo unachoingia omba wakuelekeze choo kilipo ukaduwae chooni
Nadhani ingekuwa busara muwabebe hao wanafunzi wa Udom wakatembelee vyoo vya vyuo vingine.
Na wafundishwe usafi.. na waache uvivu wa kubeba maji kisimani.



Udom Kuna shida ya maji
Hivyo maji huchotwa kisimani, mabomba ndani ya hostel hayatoi maji.
Sasa mtu hataki kujitesa kuchota maji, anaacha mzigo wake mzima mzima .. na tena anavizia muda ile usafi umemalizika .
 
Hicho chuo ni kipya intake ya kwanza ni 2008 lakin leo kinazidiwa na Sua chuo cha mwaka 1984 vyoo visafi mpaka unafua nguo
 
Back
Top Bottom