DOKEZO Achana na kunguni, UDOM ina vyoo vichafu sijawahi kuona

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mkuu, umeshapata ajira?
 
Hakika, Pia sehemu nyingi za kula za mabasi vyoo ni vichafu sana. Watu wanajisaidia hawaflashi, sabuni za kunawa za unga wamedailuti na maji, kwingine vyakula wanauzia njia za kwenda vyooni.
 
Wewe ulipokuwa Mwanafunzi ulifanya jitihada gani za kurekebisha hali hiyo,usije kuwa unatoa malalamiko maana Watanzania kwa malalamiko hatujambo kuchukua action kirekebisha hiyo hali.
 
Wawekwe mgambo katika vyoo kukagua kila anayetoka chooni kama amesafisha vizuri.
 
Karibia vyuo vyote wapo hivo sio udom tu, baadhi ya wanavyuo wenyewe ni wachafu,nje wanavaa vizuri ila tabia zao sasa
Mkuu, kwani hao wanavyuo wametoka wapi? Nafikiri ungesema tu "Watanzania"

Kama upo jirani na Mwanza, tembelea vyoo vya stendi mpya ya Nyegezi. Utashangaa kwamba pamoja na kwamba vimeanza kutumika miezi ya hivi karibuni, baadhi vimeshaharibiwa.

Ingekuwa ni mamlaka yangu ingepitishwa sheria ya kila kaya kupewa semina maalum ya usafishaji na utumiaji vyoo kiusahihi.
 
Hilo la vyoo siyo UDOM tu ni Tanzania nzima, Mtanzania hana kabisa utamaduni wa kuweka usafi wa vyoo.

Elimu kubwa sana kwa vitendo inahitajika hapo.
Madam, upo sahihi, lakini kusema hiyo ni tabia ya "Mtanzania" utakuwa umekosea. Labda ungesema Watanzania wengi. Naamini wewe huna hiyo tabia.

Na kweli, mimi binafsi, kati ya mambo ambayo yamekuwa yakinikera, ni la vyoo kutokupewa hadhi stahiki. Inaonekana vyoo havipewi kipeumbele na Watanzania walio wengi.

Ndiyo maana unaweza ukamkuta mtu kajenga nyumba ya tofali akaezeka kwa bati na kusakafia, lakini choo akazungushia tumifuko tu, halafu mlangoni mwa choo akaweka gunia.

Kama mtu ameweza kuezeka nyumba kwa bati, angeshindwa kujenga kachoo kanakoendana na hadhi ya nyumba anayoimiliki?

Vyoo havipewi hadhi stahiki na Watanzania wengi.
 
Sio UDOM tu hata hapo UD kuna vyoo inabidi uvute pumzi ndio uingie kukojoa. Ukitoka unanuka harufu ya choo

Kuna hall 5 upande wa vyoo ilikuwa ni hatari kwa afya, maji ya mavi yalikuwa yanatiririka hovyohovyo

Sijajua miaka hii hali ikoje
 
Hizi tabia za kutojua matumizi ya vyoo wanafunzi wa vyuo wanatoka nazo shule za sekondari na msingi.
 
Kinachotakiwa na kuwekwa mgambo kusimamia matumizi sahihi ya vyoo.
Sio wawasimamie vizuri watu wa usafi mkuu

Kwa upande wa majengo ya accommodation waanze na warden na watu wake wa usafi wa jengo analosupervise

Maana warden ndio kama baba mwenye nyumba anayesimamia jengo linalitumiwa na wanafunzi
 
Kikweli vyuo vya binafsi kwa usafi wapo vzr sana mf Jordan University-Moro...Wafanyakazi wapo full time kufanya usafi kila baada ya masaa 3 au 4 kwa siku....
 
Mtu wa maombi hapaswi kusema hivyo.
 
Yule mama yenu msemaji wa UDOM atakuja kukupinga vikali na kusema unasema haya wakati vyuo vimefungwa, subiri uone suala la KUNGUNI alipinga vikali kwamba mnachafua Jina la Chuo Sasa umeibuka huu uozo kuna vyuo ukienda chooni unatamani ubakie huko huko usitoke, chooni bafu maji bwelele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…