Acheni kupotosha alichokuwa amesema Tundu Lissu kuhusu Acacia na MIGA

Huo ulikuwa wimbo, enzi za Ukapa, kwamba tunalipa madeni, tunafunga mikanda, ikaundwa TRA tukawa tunakusanya kodi, wakaja na NIHF pilot. Na tukaambiwa tulisamehewa sehemu kubwa ya deni la taifa kupitia Oxfam na budget yetu ikawa imepunguza utegemezi kutoka kwa donor contries na ikawa inajitegemea up to 80%, sasa hapo ndio sielewi lini tumerudi nyuma mpaka 30 to 45%, and how do we fund our own mega projects at that level of dependence in our budget?! Na hili tunadanganywa?
 
Hahaha unataka white paper kwenye eneo lao la kula?!
Hawatakaa wakusanye maoni kwenye hili, waka hata usiote.
Peleka tu maoni kama unayo lakini, hawawezi kukusanya maoni ya wananchi wote.
Wao wanasema kuyazuia makinikia kumefanikisha kuondoa mbaya wao ACACIA, wewe unauliza wamefanikiwaje?!
Huo ndio mtaji wao kisiasa, na ndio msingi wa uzi huu, wali miss construe statements za lisu kuhusu MIGA politically wao na wengi tusiofahamu, wakasema alipotosha ila wao ndio wako right.
 
hata mara ya kwanza shida ilikuwa sio kusafirisha. shida ilikuwa kutojuwa kinachozalishwa huko Japan.

Tuliambiwa hakuna kinachozalishwa ila mchanga wanasafirisha tu kama uchafu. JPM akasema basi wauache uchafu wetu. Mbunge Msukuma akasema kama uchafu mbona unalindwa sana toka machimboni hadi Dar?
Nasikia katika makubaliano yao-makinikia yataruhusiwa kusafirishwa na hiyo smelter siyo issue tena. Hii ina maanisha tumerudi pale pale.
 
Nilisema nitafuatilia, na nikasema kwa kumbukumbu zangu, hadi BM anaondoka madarakani, bajeti yake ilikuwa tegemezi kwa at least 40%... nilikuwa sahihi! Nimetafuta hotuba ya bajeti ya mwaka 2005 ambayo ilisomwa na Basil Mramba! Sehemu ya hotuba hiyo inasema:-

Halafu baada ya kuipitia kwa haraka haraka hii hotuba, kuna jambo limenishangaza sana... Mzee wa Msoga sijui alikuwa na nini!! Inaonesha watu wakifanya kazi bila shuruti hata productivity inakuwa kubwa! Kilichonishangaza ni jinsi alivyokuwa ameongeza mapato ya serikali maradufu kwa kulinganisha na yale aliyokuwa ameachiwa na Mkapa!!

Sehemu ya hotuba ya mwisho ya Mkapa inasema:-

Yaani Mkapa kaacha mapato chini ya TZS 200 Billion kwa mwezi, Mzee wa Msoga kaacha takribani Sh. 900 Bilioni kwa mwezi!!

Hotuba kamili nimeambatanisha hapo chini!

Anyway, niongee kidogo kuhusu hilo la kusamehewa madeni!

Naweza kusema Mkapa aliingia na mguu mzuri... 1996 IMF walikuja na initiative iliyofahamika kama Highly Indebted Poorest Countries wakilenga kusamehe madeni kwa nchi 38 maskini zaidi duniani! Sharti lao la kwanza, walizitaka selected countries waoneshe nia ya kulipa... na Mkapa akaonesha hiyo nia, ndio maana alikuwa analipa kweli kweli ili Tz i-qualify initiative ya kusamehewa madeni!!

Baada ya ku-qualify, tukafutiwa madeni kwa sharti kwamba, zile tulizokuwa tunadaiwa badala ya kuzilipa tuzitumie kuboresha ustawi wa jamii in terms of Elimu, Afya na kuondoa umaskini wa kipato. Kufikia hilo, ndipo ikaanzishwa MKUKUTA... Mkakati wa Kupunguza na Kuondoa Umaskini Tanzania!

Kwahiyo mambo yoooote kuanzia Shule za Kata, MEM (Mpango wa Elimu ya Msingi), MES, MEMKWA, Kufuta Ada Shule za Msingi na Kupunguza Ada kwa Shule za Sekondari, na hatimae Elimu Bure pamoja na Zahanati kila kijiji bila kusahau TASAF... yote hayo chimbuko lake ndo hilo.
 

Attachments

Ndo maana kila wakati huwa nawaambiwa nyie kazi yenu ni kupiga makofi tu hata mkidanganywa!!! Yaani wanachosema wanasiasa na nyie mnakidakia kama kilivyo bila kutafuta ukweli!

Mwaka 2011, Tanzania Mineral Auditing Agency (TMAA) wakati wanatafiti commercial viability ya kujenga smelters Tanzania, walitoa viwango viwango vya madini mbalimbali vilivyomo kwenye makiniki kama ifuatavyo:-

Sasa wewe ni nani ambae alikuambia kwamba wanachosafirisha ni uchafu tu?!

Na hata ukiingia kwenye tovuti ya Acacia, walikuwa wameeleza wazi copper concentrate ina-account asilimia ngapi ya mapato yao... na kama sikosei, ni zaidi ya 30% ya mapato yao!! Sasa tangu lini uchafu ukawa unatoa mapato makubwa kiasi hicho?!!

Ndo maana kila wakati hapa nimekuwa nikisema, ningekuwa JPM, kuwa na mashabiki aina yenu ningejisikia aibu sana kwa sababu ingeonesha wazi kwmaba hawa watu wananishabikia kwa sababu ama hawapo well informed au wapo tayari kushabikia hata wasichokijua!!!
 
walikuwa wanakwepa kodi..
kwa kisingizio cha mchanga hauna kitu.

Unawatetea Acacia ama?

wingi wa data sio always ni uwezo wa kuelewa.
 
kwa kukusaidia zaidi walikuwa wanapata zaidi ya ulivyotaja ikiwamo madini mengine mengi

Kodi waliyokuwa wanalipa kwa kinachotokana na mchanga hakikufanana na uhalisia wa walichokuwa wanapata Japan.

Hakukuwa na ukweli na uwazi... walikuwa wanatuibia... wakionesha they are not getting much from mchanga...

Google tena data uoneshe kuwa Acacia walikuwa wanalipa vizuri kodi. Na walikuwa wanatoa report sahihi ya wanachovuna toka kwenye mchanga.

 
walikuwa wanakwepa kodi..
kwa kisingizio cha mchanga hauna kitu.

Unawatetea Acacia ama?

wingi wa data sio always ni uwezo wa kuelewa.
Duh! Yaani nyie jamaa ni janga sana kwa taifa!!! Kwa kisingizio cha mchanga hauna kitu wakati unaona hapo wameorodhesha viwango vya madini ya aina mbalimbali?!

Kwa akili yako unadhani hizo takwimu zinatoka wapi kama sio kwa hao hao Acacia?! Sasa watasemaje mchanga hauna kitu na wakati huo huo wanatoa viwango vya madini vilivyopo?! Au watasemaje kwamba mchanga hauna kitu na wakati huo huo wanasema mapato yanayotokana na makinikia yana-account 30% ya mapato yao yote?!

Kwa mtindo huo, it's matter of time Magufuli aseme yeye ndie kafanikisha ujenzi wa hospitali ya Muhimbili, na hapo mtaanza tena kushangilia!!
 
Walikuwa wanapata zaidi kwa kiwango kipi?! Kile alichotaja Profesa Mruma sio?! Kama ndivyo, mbona hamjadai basi matrilioni yanayotokana na viwango vikubwa zaidi kama ambavyo mliambiwa na akina Profesa Mruma?1

Kwamba walikuwa wakionesha they're not getting much kwenye mchanga, nimeshakuambia hata ripoti zao zinaonesha mapato yanayotokana na copper concentrates ni 30% of total revenue!!! Sasa how come useme 30% "...not much?"
 
Acacia hawakuwa wanakwepa kodi?
Lissu nawewe mmeshinda [emoji16][emoji16]

Toa data ya kodi waliyokuwa wakilipa kwenye huyo mchanga..

kulikuwa na mazingira ya rushwa... walihonga wachache kukwepa kodi ya wanachopata kwenye mchanga.

Lissu alikuwa mteja wao.. Alifaidika sana.
Nawewe ulifaidika na dhulma ya mchanga?
 
compared to walichokuwa wanapata Japan sir....

Nn ngumu kuelewa?
Ama unataka Acacia wakuone waanze kukutumia kama Lissu?
 

..Duh!!

..Lissu alikuwa mteja wa acacia?!

..hebu tueleze alikuwa akinunua nini.

..alikuwa akinunua dhahabu, au makinikia?

..vijana wa uv-ccm hamna hoja mmebaki kuleta vioja.
 
kumbe alikuwa anawatetea bure?[emoji16]
..Duh!!

..Lissu alikuwa mteja wa acacia?!

..hebu tueleze alikuwa akinunua nini.

..alikuwa akinunua dhahabu, au makinikia?

..vijana wa uv-ccm hamna hoja mmebaki kuleta vioja.
 
Asante, kwa hili nadhani zile taarifa zilikuwa za kwenye majukwaa ya siasa.

Nadhani wakati wa kikwete walipa kodi walikuwa wengi, ukilinganisha na kipindi hiki cha sasa.
 
kumbe alikuwa anawatetea bure?[emoji16]

..mtetezi wa accacia ni yule aliyewasamehe deni la 191 billion na kukubali kishika uchumba cha 300 million.

..na aliyeingia makubaliano mapya yatakayoruhusu makinikia kusafirishwa nje ya nchi badala ya kuchenjuliwa hapa Tz.
 
Mzee ukiwa kiongoz ndo unakuwa mtanzania halali wa kuzijua tzs moneys ni hela ya nani
 
Mkuu chige naomba maoni yako kuhusu hizi initiative zote za serikali ya JPM,
1:Je kuna positive outcome yoyote iliyopatikana au itakayopatikana au serikali ingekaa tu kimya na kuendelea as usual na Accacia?
2:Je ushauri wa TL alioutoa ungefuatwa je kungekuwa na matokeo bora zaidi ya haya yaliyofikiwa?
3:Je report za Ossoro na Mruma ni kweli zilikuwa proffessional rubbish kama alivyosema TL? Kwa maoni yangu mimi zile report hasa ya Ossoro(economical ) ndiyo ili-trigger haya majadiliano na for sure i can say it was the good move by our government.
Nawasilisha mkuu
 
kuna namba 16% hujaiona
kuna 50/50 hujaelewa.
Ntakusaidiaje kuanzia hapo mkuu?
[emoji16][emoji16]
..mtetezi wa accacia ni yule aliyewasamehe deni la 191 billion na kukubali kishika uchumba cha 300 million.

..na aliyeingia makubaliano mapya yatakayoruhusu makinikia kusafirishwa nje ya nchi badala ya kuchenjuliwa hapa Tz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…