ACT Wazalendo: Bandari ni Hoja ya Kiuchumi, Tunaunga Mkono Uwekezaji

Mnakumbuka shuka wakati kushakucha kitambo 🤣🤣🤣🤣
 
Hakuna chama hapo ni wapiga vigelegele ndio shughuli yao
Swala la Bandari sio ngoma ya kutoa au kupeleka mwali.
Watulie wasitupigie makelele
 
Hakuna anayepinga uwekezaji, sisi watanzania tunasema tunataka uwekezaji wenye tija kwa Taifa.
 
Wajuzi nisaidieni: Kama mkataba (IGA) umesharidhiwa na bunge, na tulishasikia serikali ikisema yenyewe inasonga mbele, je, mapendekezo haya ya act na ya wadau wengine yatazingatiwa je? Je hakuna njia ya kuilazimisha serikali izingatie mapendekezo ya wadau mbalimbali? Najua serikalini yamejaa majizi. Na ukiangali muwekezaji huyu alivyopatikana, na anavyotetewa, wabunge na wasanii walivyopelekwa Dubai, Kun harufu ya rushwa kubwa hapa.
 
Hata TEC wanaunga mkono uwekezaji ktk bandari zetu. Lakini wanapinga kwa nguvu zote mkataba huu mbovu wa Dpworld. Na mimi nimewaelewa. Pia nimeusoma mkataba.
 
Zitto ni mnafiki sana. Amevizia sakata limepoapoa huku wengine wakidai DP World hawaji tena ndo anajifanya kuleta maoni ya ACT. Walikuwa wapi muda wote!?, Zitto ni mnafiki na mdini sana.
Nashindwa kuelewa kwa nini baadhi ya wachangiaji hupendelea kushambulia watu binafsi badala ya hoja zinazowekwa mezani. ACT Wazalendo wameweka hoja mezani. Tuichambue badala ya kumshambulia Bw. Zito
 
Nashindwa kuelewa kwa nini baadhi ya wachangiaji hupendelea kushambulia watu binafsi badala ya hoja zinazowekwa mezani. ACT Wazalendo wameweka hoja mezani. Tuichambue badala ya kumshambulia Bw. Zito
Mkuu huu Uzi umewekwa humu asubuhi saa 1 na mapendekezo ya ACT(pdf) imekuwa uploaded saa 5 au 6 kama sijakosea. Hiyo ni moja, nimesoma mapendekezo yote ya ACT ni mazuri sana na yana nia nzuri. Swali ni kwanini hayakuletwa wakati mjadala wa DP World upo moto!??, Zitto alikuwa anakwepa nini?,kwanini wasubirie hadi tuanze kuhisi serikali imenyanyua mikono kuhusu DP World ndo walete mapendekezo!?,huoni kama wanavizia vizia, wanadai waliunda kamati July 5, leo September 4, miezi miwili mbele walikuwa wanatafiti nini ishu iliyoishajadiliwa mara kibao!?,ndo maana tunamuita Zitto mnafiki, hapendi rangi yake halisi ionekane.
 
Kama hauna shida mbona mnasema mtaurekebisha kutokana na hoja zinazotolewa na wananchi?Au mnadanganya hata kwenye hilo?

Amandla...
Mkataba hauna shida inabidi serikali ijibu hivyo make maswali yenu sijui ya ukomo yatakuwepo kwenye HGA.
 
Hakuna jipya!! Hakuna asiyeunga mkono uwekezaji. Maeneo yaliyoainishwa kuwa na utata na TEK nao wamepita humo humo!! Plagiarism at work! Laiti hili andiko wangelitoa mwanzo kabisa, wangeibuka mashujaa!! Swali je kama DP World wasipokuwa tayari kukubaliana na mapendekezo yaliyotolewa nini msimamo wa ACT Wazalendo? Hicho ndicho tunachotaka kusikia!!
 
Ulitaka CHADEMA wakubali mkataba wa kijinga vile?
Mkataba sio wa kijinga Ila chadema ni matamanio Yao serikali iharibikiwe iselete maendeleo yoyote ili wapate cha kusema Kwa wananchi then matamanio Yao ya kukamata madaraka yatimie, hayati magufuli alipata kusema ukiona adui yako ameanza kukupongeza jiulize mara mbili ni sehemu unakosea, so chadema kupinga kila kitu cha serikali sie wanaccm wala hatushangai Ila wakitaka kutumia nguvu nyingi kupotosha lazima tuwashughulikie.
 
Kila siku maswali hayo hayo?😂😂
 
ACT bwana,wameshanusa uelekeo, hivyo nao wamelalia hukohuko ili kujichukulia credit za bure.
 
Wanaunga mkono uwekezaji? Kwani Kuna anayepinga uwekezaji? Kinachopingwa ni Yale masharti ya hovyo ya mkataba, na mkataba wenyewe kusainiwa na kufanya Siri. ACT mmengoja na kupima upepo ndo mnakuja na unafiki wenu?
 
Nashindwa kuelewa kwa nini baadhi ya wachangiaji hupendelea kushambulia watu binafsi badala ya hoja zinazowekwa mezani. ACT Wazalendo wameweka hoja mezani. Tuichambue badala ya kumshambulia Bw. Zito
Hapo hakuna hoja mpya ya kuchambua toka ACT Wazalendo!! Wame-copy na ku-paste hoja ambazo tayari zilishaibuliwa na yule wakili wa mbeya na pia na waraka wa maaskofu wa katoliki TEK. ACT Wazalendo walikuwa wapi? Wameamua kudandia gari la wazalendo wa ukweli ili kuepuka kuhukumiwa na historia!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…