ACT–Wazalendo waichambua Ripoti ya CAG - Aprili 11, 2021

ACT–Wazalendo waichambua Ripoti ya CAG - Aprili 11, 2021

Ah nasubiria babu T naye aichambue

Ova
 
Media zinaanza kufunguka zama za uoga uoga zimekwisha hivi Azam wangeweza kuchambua Ripoti hii waziwazi wakati wa Mwenda
... kwa Katiba iliyopo, utashi wa kiongozi mkuu ni muhimu sana katika kuamua hatma ya taifa. Rais Samia alielekeza "hakuna kuficha kitu" na pia akaagiza "media zilizofungiwa zifunguliwe" ni maneno machache sana ya Kongozi Mkuu unaona watu wanapumua na kufunguka sasa. Japo wazito kuelewa kwa haraka akina Abbas hawakosekani ila ni suala la muda tu wataelewa!
 
Habari hii ni kwa mujibu wa tweet ya ACT-Wazalendo UDSM ambapo wamearifu uchambuzi huo utaanza saa sita kamili mchana wa leo.
Mkuu geuza huu uzi wako kuwa Live maana uchambuzi sasa unaendelea.
 
ACT Wazalendo wanafanya uchabuzi wa ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali.

Fatilia uchambuzi huo live.

 
Haya mambo enzi za mwendazake hayakuwezekana kabisa!

Sasa hata hamu ya kutazama local stations inaanza kurudi.

JIWE alikuwa Dikteta ukweli lazima usemwe.

Kwanza hata ITV na Azam wasingekubali kumrusha Zitto hata kama wangepewa dau la maana.
 
Ila naomba msinielewe vibaya.
Jana Asad aliongea na leo Zitto anaongea, mbona kama hapa kuna kaharufu flani ka Ijumaa?

Sikushangaa Maalim kujiunga na ACT pia sio jambo la ajabu Asadi nae punde au next election akawa mgombea wa ACT nafasi ya Urahis.

Naomba mnisamehe kwa mawazo yangu kwani msiba umenichanganya
 
Miaka yote Zitto huwa anachambua Report ya CAG na anabamiza kweli kweli, sehemu kubwa ya umaarufu wa Zitto imetokana na uchambuzi wake wa report hii na kama Serikal ya Jk ilichafuka basi ilitokana na uchambuzi wa Zitto kwny reports hizi wakati wa Ludovick Uttoh kama CAG na Zitto kama Mwenyekiti wa PAC

Reports za CAG wakati wa Jk zilikuwa zinapelekea Mawaziri kutemwa

Hata Mwakani tutaoneshwa madudu mengi ya Utawala wa Samia,

Tatizo sio reports za CAG, tatizo ni mstuko unaotokana na Imani tuliyokuwa tumejenga kwa Hayati kuwa katokomeza Ufisadi ndio maana kila taarifa ya Ufisadi tunaona kama imelenga kumchafua
Ila naomba msinielewe vibaya.
Jana Asad aliongea na leo Zitto anaongea, mbona kama hapa kuna kaharufu flani ka Ijumaa?

Sikushangaa Maalim kujiunga na ACT pia sio jambo la ajabu Asadi nae punde au next election akawa mgombea wa ACT nafasi ya Urahis.

Naomba mnisamehe kwa mawazo yangu kwani msiba umenichanganya
 
Back
Top Bottom