Uchaguzi 2020 ACT-Wazalendo wasema watashiriki uchaguzi mdogo jimbo la Muhambwe

Itakuwa ni ujinga chama cha upinzani kuwa hakiwezi onyesha upinzani mpaka kuwepo na tume huru, nyi wabongo mmelegea sana hamukuonyesha kujikaza wakati wote tokea mumeanzisha chama chenu
@Zitto alituambia tarehe 30 November kuwa hamtashiriki chaguzi yoyote ya NEC kutokana na wizi. Okay apart from maridhiano nini kimebadilika mpaka leo mdhani mkishinda mtatangazwa huku bara?
 
Nyie ACT kushiriki ni halali maana mna maridhiano tayari but kwa CHADEMA ingekua aibu maana wamepinga chaguzi, wamekataa viti maalum afu waje kutafuta jimbo moja??

Then kuhusu kuwa CCM.... Nadhani CHADEMA kama ingekua imelainika ingeshakufa toka 2012!! Hvi madhila aliyopata Mbowe, Mnyika kufungiwa kusoma milele, Lissu kumiminiwa SMG nzima n.k unaweza kudai hao ni CCM B?
Unataka mulainike vipi tena Tundu Lissu anapigwa risasi lakini bado viongozi wenu wakuu bawacha wanaunga mkono juhudi, kwisha habari yenu chadema., anzeni upya chama chenu
 
Tangazeni basi 2025 hamtashiriki bila tume huru kama walivyotangaza CUF lipumba., kwann mna kigugumizi
Mbowe alitangaza hilo siku moja na @Zittona amesimamia hilo mpaka leo nyie ndio mmerudi nyuma kwa kigezo cha maridhiano. Mnasahau kuwa tume ni ile ile iliyompora zitto ubunge unless mna makubaliano ya kumrudisha bungeni.
 
Unataka mulainike vipi tena Tundu Lissu anapigwa risasi lakini bado viongozi wenu wakuu bawacha wanaunga mkono juhudi, kwisha habari yenu chadema., anzeni upya chama chenu
Nani kaunga juhudi? Hao mabinti tamaa ya madaraka ndio imewapeleka but chama kiliwafukuza. Nyie ACT jussa kapigwa huku makumi ya wafuasi wameuawa wakipigania ushindi wenu mmeenda kuwasaliti kisa ving'ora na wizara mbili tu
 
Mie mtazamo wangu naona wote sahihi kabisa, ACT wazalendo kushiriki ni sawa na CDM kutoshoriki haisumbui chochote. Kimsingi tatizo sugu lipo na litaendelea kuwepo hata baada ya uchaguzi mdogo kuisha na hata kuingia uchaguzi wa 2025!

In fact tatizo la sheria zetu kuwa mbovu litaendelea nadhani hadi baada ya miaka 100 mbele.Nayasema haya kwa kutazama muamko na ukakamavu wa wananchi kwa ujumla. Upinzani unasubiri wananchi wapiganie mabadiliko ya kisheria, na wananchi wanaona hayo sio mambo yenye umuhimu katika maisha yao. Wengi hususan mikoani wanadhani wapinzani sio watu wanaoitakia mema TZ au wanatumiwa na watu kutoka nje (siasa zinazotumiwa na CCM).

Zanzibar CCM huwaunganisha wapinzani na waarabu, na Tanganyika na mebeberu au wamagharibi. Hizi ni siasa za kitoto sana, inashangaza sana kuona zimefanya kazi kiasi hiki. Hasa utawala wa JPM alipigia chapuo sana eneo hili na kujijengea jina kama mkombozi wa afrika, wakati facts ziko vyengine kabisa.
 
@Zitto alituambia tarehe 30 November kuwa hamtashiriki chaguzi yoyote ya NEC kutokana na wizi. Okay apart from maridhiano nini kimebadilika mpaka leo mdhani mkishinda mtatangazwa huku bara?
Zitto ni mtu wa hoja, akili yake haijaganda alishiriki uchaguzi mdogo kule pemba jimbo la pandani kumpima hussen mwinyi kama angedumisha demokrasia na kashinda jimbo kwa level ya uwakilishi na sasa kaweka hoja nyengine kwa mama Samia na hivi kwa mwanasiasa ndivyo anavyotakiwa awe siku zote awe na mtazamo chanya sio siku zote unajifunguia ndani kwenye kiyoyozi kule belgium au dubai na canada halafu wananchi wako ambao wameeka matumaini yao kwako hawajuwi nini cha kufanya, ni kufeli kisiasa, chadema imefeli sana kisiasa
 
Zitto hajajifunza tu kwa usaliti alioufanya kwa kujiunga na serikali ya mseto Zanzibar akasababisha Maalim Seif apoteze maisha bado anaendelea tu na usaliti wake ?
 
Nani kaunga juhudi? Hao mabinti tamaa ya madaraka ndio imewapeleka but chama kiliwafukuza. Nyie ACT jussa kapigwa huku makumi ya wafuasi wameuawa wakipigania ushindi wenu mmeenda kuwasaliti kisa ving'ora na wizara mbili tu
Sasa kama viongozi wen wakuu wana tamaa ya madaraka kama ulivyosema apo kuna nini tena, well jussa kapigwa sana lakini jussa binafsi alikuwa mtu mwanzo mwanzo kukubali wazanzibari kuungana na hata hao waliopigania ushindi waliafiki umoja wa wazanzibari ili angalau wazanzibari wapate haki zao kipindi hichi ambacho ubaguzi ulikithiri kule zanzibar, matabaka lakini na chuki na hivi ndivyo siasa, adui hupigani naye kwa siku 1 au mbili, muhimu ni kwambza zanzibar saivi watu wote wanapata haki sawa.
 
Ndio maana wamefukuzwa!! Kama nyie mlivyotimuliwa na Lipumba mlipomsaliti the principle is clear ili chama kibaki na heshima.

Sasa nyie kama kamati kuu mnakubali ku surrender kisa ving'ora? Maalim alipogomea 2016 nadhani umeona heshima na nguvu aliyoingia nayo 2020. Nyie waganga njaa ndio msahau kabisa hyo 2025 kuambulia chochote zenji maana CCM washajua mtakubali tu umakamu hta kma mmeporwa majimbo 20.
 
Zitto ni mtu wa hoja, akili yake haijaganda alishiriki uchaguzi mdogo kule pemba jimbo la pandani kumpima hussen mwinyi kama angedumisha demokrasia na kashinda jimbo kwa level ya uwakilishi na sasa kaweka hoja nyengine kwa mama Samia na hivi kwa mwanasiasa ndivyo anavyotakiwa awe siku zote awe na mtazamo chanya sio siku zote unajifunguia ndani kwenye kiyoyozi kule belgium au dubai na canada halafu wananchi wako ambao wameeka matumaini yao kwako hawajuwi nini cha kufanya, ni kufeli kisiasa, chadema imefeli sana kisiasa
Zitto akiibiwa kura hapo kibondo asije kulialia hapa akubali matokeo na ampe ushirikiano Samia!!

Huyo unayesema alikua kwenye kiyoyozi uliona alivyorudi hadi ACT mkapoteana na mgombea wenu wa kubumba haahaaa.

Yaani pale ndio nliwadharau kabisa.... Mnapokea kapi la CCM na liliwakomesha mkakosa kila kitu huku bara hamna mtaji wa wanachama kabisa.

Lissu is worth a million more ndio maana zitto alikubali kumuunga mkono maana aliona upepo wake haukamatiki.
 
Ndio maana wamefukuzwa!! Kama nyie mlivyotimuliwa na Lipumba mlipomsaliti the principle is clear ili chama kibaki na heshima.

Sasa nyie kama kamati kuu mnakubali ku surrender kisa ving'ora? Maalim alipogomea 2016 nadhani umeona heshima na nguvu aliyoingia nayo 2020. Nyie waganga njaa ndio msahau kabisa hyo 2025 kuambulia chochote zenji maana CCM washajua mtakubali tu umakamu hta kma mmeporwa majimbo 20.
Mtafukuza wangapi? mbona mumeshindwa kumfukuza Makamo mwenyekiti wenu kule Zanzibar akipigia kampeni wagombea wa ccm 2020 mchana kweupe na kina mbowe wanajua fika., ndio mana tunasema hamna taasisi imara mumesheheni mapandikizi kwenye chama chenu
 
CHADEMA ni chama cha upinzani ACT na wajinga wenzao ni matawi ya CCM.

Hivyo ukome kuilinganisha CDM na hao waganga njaa wenzenu
Waganga njaa kina nani? Hawa wanaopokea ruzuku kutoka kwa wabunge ambao uchaguzi wao na ushindi wao wanalisema hawautambui? Hata kama kupenda ni upofu hii sasa ni kupenda ni umau.ti
 
Harufu ya Udini inaanza, ZZK akiwepo Rais Muislam uwa wanayumba sana kimsimamo. Wengine tunamfahamu vizuri tangu enzi za JK, na Ustaadhi Ilunga aliwahi kumsifu kwa hilo. Tusubiri
Hapana nakataa. Mh Zito huwa anasimamia kile anachoona kina faida kwa taifa na chama chake. Aliwahi hata kumpongeza raisi Magufuli enzi za uhai wake kwa kazi yake nzuri aliyokuwa anaifanya kwa nchi hii mpk kupelekea wapinzani wenzake kumuita "msaliti". Huyu Magufuli aliekuwa anasifiwa na mh Zito kwa utendaji wake uliotukuka alikuwa ni mkristo halisi wa baba na mama. Pia raisi Magufuli alivyokuja mkoani Kilimanjaro kufuatilia maendeleo ya mkoa wetu mh Mbowe alimsifu sana raisi lkn hakuna alieunganisha sifa hizo za Mbowe na udini au usaliti.

images (3).jpeg
 
Mtafukuza wangapi? mbona mumeshindwa kumfukuza Makamo mwenyekiti wenu kule Zanzibar akipigia kampeni wagombea wa ccm 2020 mchana kweupe na kina mbowe wanajua fika., ndio mana tunasema hamna taasisi imara mumesheheni mapandikizi kwenye chama chenu
Tutafukuza wote tu ndio discipline inajengwa... Ona kina Zitto walitimuliwa ili heshima ya chama iwepo na toka hapo hamna anayeogopwa kwenye chama otherwise yangetukuta ya Lipumba and the late Seif!!

About Issa Mohammed hana madhara.... Yupo pale ceremonial kwa sababu ya muungano tu so abaki atoke hana impact. Zeni ni kina Mwalimu ndio wapo kwenye inner circle.
 
Waganga njaa kina nani? Hawa wanaopokea ruzuku kutoka kwa wabunge ambao uchaguzi wao na ushindi wao wanalisema hawautambui? Hata kama kupenda ni upofu hii sasa ni kupenda ni umau.ti
Cdm haijawahi na haitafanya matendo ya kijambazi kama mfanyavyo nyinyi majambazi wa uchaguzi
 
Tutafukuza wote tu ndio discipline inajengwa... Ona kina Zitto walitimuliwa ili heshima ya chama iwepo na toka hapo hamna anayeogopwa kwenye chama otherwise yangetukuta ya Lipumba and the late Seif!!

About Issa Mohammed hana madhara.... Yupo pale ceremonial kwa sababu ya muungano tu so abaki atoke hana impact. Zeni ni kina Mwalimu ndio wapo kwenye inner circle.
Ubarikiwe sana kiongozi kwa kumpa elimu ya bure huyo binti asiyezijua siasa
 
Back
Top Bottom