ACT-Wazalendo yaridhia kushiriki kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na Vyombo vya Uwakilishi

ACT-Wazalendo yaridhia kushiriki kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na Vyombo vya Uwakilishi

Ameongea vizuri. Lakini swali la msingi ni kuwa yale yote waliyosema kuhusu uchunguzi wa mambo yaliyotokea, fidia kwa walio athirika, wahusika kuadhibiwa na marekebisho katika vyombo vya dola na usimamizi wa uchaguzi yatafanyika kabla ya wao kuingia rasmi katika GNU au wanategemea kuyafanya wakiwa ndani ya serikali kwa kutegemea nguvu za wawakilishi wao wanne na wabunge wanne?

Amandla...
 
Nikapewa zile karatasi....
Nikajongea katika KITUTURU..kalamu mkononi....

Kwa mara nyingine nikajiuliza..je kumchagua MAGUFULI ninapoteza kwangu?wanangu?nchi yangu?!!

Jibu likawa HAPANA....

Je nimchague Tundu Lissu ama Membe?!!

Kwa haraka ikanijia ile picha Mh.Mbowe anaibadili gia angani na kumchukua mh.Lowassa....
Kwa mbali ikanijia ile picha Tundu Lissu anaongea ule mkutano wa kumpokea Mh.Membe ACT....

Nikasunya msunyo wa NGUVU...

Nikamtilia tiki JPM
Nikamtilia tiki Mbunge wa CCM
Nikamtilia tiki Diwani wa CCM...

Nilipogeuka NIKACHOVESHWA wino kidole changu cha MWISHO nikajisepea FASTAAAA....



BILA CCM IMARA NCHI ITALEGALEGA.
 
Chadema nao wakae na JPM kisha wakubali kumsaidia kurudisha uhusiano wa kimataifa, TL ampe maelekezo Wakili asitishe mambo ya AICC na kumtakia kila la heri JPM, JPM atumie nafasi hii kurudisha umoja wa kitaifa na ushirikiano baina yake na wapinzani.

TL awe wakala wa kuwaleta wafadhili, watalii, wawekezaji nchini akiwa huko nje, JPM aboreshe Sera ya uwekezaji na awasaidie sekta binafsi kukuza mitaji na kuinuka tena. Baada ya miaka 5 TL arudi kugombea nafasi ya uraisi. Hata Akishindwa, Tanzania itaheshimika sana.

PESA ZA WAZUNGU NA MISAADA YAO BADO TUNAITAKA SANA TU. ILA ILI WASITUUMIZE INATUPASA KUSHIKAMANA NA TUSINYANYASANE.
 
"Ni bora kukaa meza moja na CCM (kufanya maridhiano) kuliko kukaa na Msaliti Lipumba."

Huyo ndo Maalim Seif, mwanasiasa jembe na mpinzani wa kweli.
 
Ismail Jussa ameumizwa, Mazrui alitekwa mara mbili, baadhi ya viongozi na wananchi wamekufa na kujeruhiwa kutokana na huu uchaguzi haramu halafu eti mnaungana na watesi wenu kwa ajili ya maslai ya watu wachache! Maalim Seif, wewe mwenyewe ulisimamishwa kufanya kampeni kwa siku 5. ACT mmeshakuwa mamluki hampo kwa ajili ya wazanzibari na watanzania bara.

mbna kama unatufokea, si kikao chao ndo kimeamua kwan tumemuita?
 
Nikapewa zile karatasi....
Nikajongea katika KITUTURU..kalamu mkononi...



BILA CCM IMARA NCHI ITALEGALEGA.
Maandiko yako hayana maana, hayajengi yanabomoa. Mshindi wa kweli ni yule anayerudisha mshikamano baada ya ushindi, si yule anayejitapa kwa ushindi huku akimnanga mpinzani.

CCM NA UPINZANI NI MUDA WA KUUNGANA NA KUIPIGANIA NCHI ILI HALI YA UCHUMI IRUDI NA PESA ZITAWALE MTAANI. CORONA IMETUUMIZA SANA.
 
We jamaa bwana
Sasa wasingeshiriki ndio zile maiti zingefufuka?

Bakini wenyewe chadema na siasa zenu za kwenye mitandao tu

Coz kwa miaka mitano yote hamtakuwa hata na mkutano wa udiwani

jamaa anajipaga kazi msemji wa chadema sasa mebaki solemba
 
Back
Top Bottom