Makato ya KUTUMIWA Pesa kwenye mmoja wa Mitandao ya simu ilikuwa kuanzia Tsh. 50,000 hadi 99,999 unakatwa makato haya hapa:
ADA KUTUMIWA: Tsh. 720+VAT
JUMLA KUU: Tsh. 720
Na sasa KUTUMIWA hiyo hiyo 50,000 hadi 99,999 Unakatwa makato haya hapa:
ADA YA KUTUMIWA: Tsh. 720+VAT
TOZO MPYA YA SERIKALI: Tsh. 2,050
JUMLA KUU: Tsh. 2,770
Hapo ina maana kwa sasa ukitaka KUMTUMIA mtu kiasi chochote kuanzia 50,000 hadi 99,999 unapaswa kuweka Pesa ya ziada Tsh. 2,770 badala ya Tsh. 720 ya awali hivyo hapo una mzigo mpya wa makato wa Tsh. 2,050.
Makato ya zamani ya KUTOA Pesa hiyo hiyo Tsh. 50,000 hadi 99,999 kwa Wakala yalikuwa haya hapa:
ADA YA KUTOA: Tsh. 2,700+VAT
JUMLA KUU: Tsh. 2,700
Na sasa KUTOA Pesa hiyo hiyo kuanzia Tsh. 50,000 hadi 99,999 unakatwa makato haya hapa:
ADA YA KUTOLEA: Tsh. 2,700+VAT
TOZO MPYA YA SERIKALI: 2,050
JUMLA KUU: Tsh. 4,750
Hapo ina maana kwa sasa ukitaka kutoa Tsh.50,000 hadi 99,999 kwa WAKALA utapaswa kuwa na ziada ya Tsh. 4,750. Hivyo hapo una mzigo mpya wa nyongeza ya Tsh. 2,050 nyingine.
KWA KIFUPI TU MUAMALA WA TSH. 50,000 HADI 99,999 KWENYE KUTUMA NA KUTOA UTAPASWA KULIPIA TSH. 7,520 YA SASA BADALA YA TSH. 3,420 YA AWALI AMBAYO MTUMAJI ANAKATWA TSH. 720 TU NA MTOAJI ANAKATWA TSH. 2,700 IKIJUMUISHA NA VAT.
TSH. 4100 NI ZIGO JIPYA LA MAKATO KWA MTUMAJI NA MPOKEAJI PESA AMBALO NI ZAIDI YA PESA WANAYOICHUKUA MITANDAO HUSIKA.
KWA UFAFANUZI HUO KAZI NI KWAKO UMTUMIE MTU ALIYEPO KIBAHA MKOA WA PWANI UKITOKEA UBUNGO au MBEZI KIASI CHA TSH. 50,000 HADI 99,999 MKATWE NA PESA YA ZIADA YA TSH. 7,520 AU UMPELEKEE KWA DALADALA ILI UMKABIDHI MKONONI NA UTUMIE NAULI TU YA TSH. 3,000 YA KWENDA NA KURUDI NA UBAKIZE SALIO LA TSH. 4,520 NA UJIPOZE WALAU MATUNDA NA CHAKULA CHA MCHANA ILI SIKU IPITE VYEMA KWAKO.