BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mtoto, Ashura Makelebe (4) amekufa kwa kuteketea kwa moto ndani ya nyumba baada ya mtu anayedhaniwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mama yake mzazi kudaiwa kuchoma moto nyumba aliyokuwa amelala.
Mtuhumiwa huyo ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai hayo, anadaiwa kufikia uamuzi wa kuteketeza nyumba hiyo baada ya kumkosa, Acyprian Charles (24) ambaye ni mama mzazi wa Ashura alipoenda kumtembelea usiku wa kuamkia leo Juni 23, 2023.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Gideon Msuya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akisema jeshi hilo linamshikilia, Magesa Mkama (29) kwa tuhuma za kuchoma nyumba hiyo kwa lengo la kumkomoa hawara yake na kupelekea kifo cha mtoto huyo.