Adaiwa kuchoma nyumba ya hawara baada ya kutomkuta usiku, mtoto afia ndani

Mtoto, Ashura Makelebe (4) amekufa kwa kuteketea kwa moto ndani ya nyumba baada ya mtu anayedhaniwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mama yake mzazi kudaiwa kuchoma moto nyumba aliyokuwa amelala.

Mtuhumiwa huyo ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai hayo, anadaiwa kufikia uamuzi wa kuteketeza nyumba hiyo baada ya kumkosa, Acyprian Charles (24) ambaye ni mama mzazi wa Ashura alipoenda kumtembelea usiku wa kuamkia leo Juni 23, 2023.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Gideon Msuya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akisema jeshi hilo linamshikilia, Magesa Mkama (29) kwa tuhuma za kuchoma nyumba hiyo kwa lengo la kumkomoa hawara yake na kupelekea kifo cha mtoto huyo.
View attachment 2667028
Kanda ya ziwa again
 
Haya mambo ya mapenzi wakati mwingine hugeuka uadui na uhasama wa kuuana na kutiana hasara wakati yalianza kwa upendo na mahaba makubwa. Kuna mwanamke mmoja yeye alikichoma moto chumba cha mpenzi wake cha kupanga akimtuhumu anaye wapenzi wengi. Majamaa mengine nayo yaliumizana vibaya na mmoja kufa yakigombania mpenzi huku yakiwa yana wake zao nyumbani. Ni vizuri wapenzi kusomana tabia mapema, ukiona mpenzi wako ana wivu kimbia hiyo hatari achana naye haraka sana atakuja kuleta madhara
Kuna mtu hana wivu mkuu??
Bora huyo mwenye wivu na anaounesha ukaujua. Vipi wale wakugumia ndani kwa ndani ndo hao unakuta kakuchomea ndani bila sababu za msingi.
 
Haya mambo ya mapenzi wakati mwingine hugeuka uadui na uhasama wa kuuana na kutiana hasara wakati yalianza kwa upendo na mahaba makubwa. Kuna mwanamke mmoja yeye alikichoma moto chumba cha mpenzi wake cha kupanga akimtuhumu anaye wapenzi wengi. Majamaa mengine nayo yaliumizana vibaya na mmoja kufa yakigombania mpenzi huku yakiwa yana wake zao nyumbani. Ni vizuri wapenzi kusomana tabia mapema, ukiona mpenzi wako ana wivu kimbia hiyo hatari achana naye haraka sana atakuja kuleta madhara
Wivu ndo mapenzi yenyewe
 
Mtoto, Ashura Makelebe (4) amekufa kwa kuteketea kwa moto ndani ya nyumba baada ya mtu anayedhaniwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mama yake mzazi kudaiwa kuchoma moto nyumba aliyokuwa amelala.

Mtuhumiwa huyo ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai hayo, anadaiwa kufikia uamuzi wa kuteketeza nyumba hiyo baada ya kumkosa, Acyprian Charles (24) ambaye ni mama mzazi wa Ashura alipoenda kumtembelea usiku wa kuamkia leo Juni 23, 2023.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Gideon Msuya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akisema jeshi hilo linamshikilia, Magesa Mkama (29) kwa tuhuma za kuchoma nyumba hiyo kwa lengo la kumkomoa hawara yake na kupelekea kifo cha mtoto huyo.
View attachment 2667028
Kosa la mauaji
Kosa la kuchoma nyumba/ jengo ( arson)
Hivi huyu jamaa anatoka kweli?
 
Back
Top Bottom