QURAN inasema zimepita zama nyingi sana ulimwenguni hakukuwa na kiumbe binaadamu ,hii dunia ilikuwa na viumbe wengine wasiokuwa binaadamu inasema hii dunia ilikuwa inatawaliwa na majini baada ya kuona majini wanapigana na kuuwana ndipo Allah akaamua kumuumba kiumbe aitwae binadamu,
QURAN inaeleza namna binadamu wa mwanzo namna alivyoumbwa ni hivi ifuatavyo:
Mungu (Allah) alimtuma malaika izrail aje duniani kuchukua udongo ili aumbwe binadamu ndipo Mungu akamtengeneza binaadamu wa kwanza baada ya kumpulizia roho Mungu akawaagiza malaika kumpa heshima adam kwa kumsujudia
Baada ya kuumbwa adam ndipo Mungu(Allah)akaweza kumuumba Hawa kutoka katika ubavu wa adam as ili iwe ni kitulizo cha nafsi na kuzaa watoto ,
Ndipo Mungu akatengeneza system yake kwa wakati huo ili watu wazaliane ,hawa alikuwa anazaa kila siku asubuhi na jioni mungu amewawezesha kuzaa hivyo ,wakaruhusiwa kuoana wao kwa wao ili wawe waijaze dunia hii ndio wakaweza kuzaliwa watoto wengi sana ,ndipo baada ya watu kuwa wengi na nabii adam na hawa kuondoka duniani ndipo Allah(Mungu)akamleta nabii NUHU kuja kuwaelimisha watu kumuamini na kumuabudu Allah(MUNGU) na sio kuabudu asiyekuwa yeye ,nuhu aliwalingania watu hao kwa kipindi cha miaka 900 takribani alipta wafuasi wachache sana idadi imenipita kidogo ,ndipo dunia ikaghariki na waliopona ni waliopanda jahazi la nuhu,
Huo ndio mchakato ulivyokuwa nimetohoa ktk Qur an