Adhabu ya kifo kwa kuchinjwa mbele ya kadamnasi (Tahadhari: maelezo, picha na video za ukatili)

Adhabu ya kifo kwa kuchinjwa mbele ya kadamnasi (Tahadhari: maelezo, picha na video za ukatili)

Status
Not open for further replies.
Mkuu, unajua uislamu unachanganya dini na utawala. Ukristo na mafundisho ya biblia hauwatakiwi kuchanganya dini na utawala. Inaweza ikahojiwa kwamba nchi zisizo za kiislamu zina ustaarabu kuliko nchi za waislamu.

Huwezi kuta nchi inajiita serikali ya kikristo au nchi ambayo inahukumu kwa sheria kutoka kwenye biblia! Yesu alifundisha wafuasi wake wasiwe moja ya serikali.

Serikali nyingi za waarabu au uislamu zinahusisha Quran kama kitabu cha sheria kwa kuchanganya dini na utawala. Quran inafundisha wanadamu kuwa makatili kwa kuchukua sheria mikononi mwao, huo ni mfano wa UUNGU MTU kwa Ufalme wa Saudia!

Kwa kweli inasikitisha sana binadamu wana enjoy kuona mwanadamu mwenzao kukatwa kichwa kama mbuzi mbele ya kadamnasi! Mimi sijui ustaarabu wa waarabu huko wapi ingawa neno "ustaarabu" ni neno lenye asili ya kiarabu!!? Imagine ustaarabu gani wa kunywa mkojo wa ngamia, wakati mkojo wake usababisha magonjwa lakini waarabu wanakunywa eti ni dawa! Nini sababu? kasema Mtume Muhammad!
Kuhusu kunywa mkojo wa ngamia sio tatizo kama wanatumia kama dawa,hapa kwetu tz tunatumia pia mkojo wa punda kama dawa ya kifua.
 
Ndugu,sasa hivi tunapigania katiba mpya kwa kuwa tunaona katiba tuliyonayo ni kandamizi so utaona hata katiba zilizotungwa na watu pia ni mbaya.Kusema quran inafundisha ukatili si sawa,mbona mtu akiua anahukumiwa kunyongwa? Hapo huoni kama ni ukatili ila kukata kichwa tu!!!!!!
Ikisemwa kwamba katiba zote zilizotungwa na watu ni mbaya si sahihi, kwa sababu nchi nyingi zenye democrasia zina katiba ambazo hazijalengwa kukandamiza wananchi wao ila zimelenga kunufaisha na kulinda maslahi yao.

Kwa mfano, mimi nina ndugu zangu waishio Uingereza na Sweden, wanasifia jinsi nchi hizo zinavyojali watu wao kwamba hata kama huna kazi serikali zinawajibika kikatiba na kisheria kuwasaidia kifedha wanainchi wao ili wawaze kuishi maisha ya kawaida.

Quran inaweza kusemwa ni mbaya kwa sababu sheria zilizokuwepo humo ndizo zinazotumiwa na mamlaka kuhukumu watu in public. Swali hapa ni, kwanini mtu kunyongwa kusifanyike huko jela pasipo umati wa watu? Quran ndiyo imeruhusu mtu achinjwe hadharani?

Bora kitanzi au risasi kuliko kuchinjwa. Kuchinjwa siyo ubinadamu bali ni ukatili! Hatahivyo, nchi nyingi kwa sasa waliondoa hukumu ya kifo kutokana na makosa mengi yaliyofanyika ya kusingizia watu wasio na makosa. Pia, nchi nyingi za ulaya zina kifungo cha maisha siyo kunyonga. Na Marekani wanatumia sumu(Lethal injection) kunyonga ambayo ni more humane method of execution kuliko kuchinja.

Zaidi, ingawa TZ tuna sheria ya kunyongwa kwa kitanzi. Wengi walioua waliukumiwa kunyongwa, lakini inasemekana hajanyongwa mtu miaka mingi, badala yake unafungwa maisha mpaka kufa.
 
Kama una nia thabiti ya kuhiji kwa ajili ya kutegemea malipo kutoka kwa Allah(s.w),huwezi kukatishwa tamaa na unyama unaofanywa na viumbe dhalili.Usimuogope kiumbe bali muogope Allah tu,,InshaAllah MwenyeziMungu akujaalie nia yako iwe sahihi,,,Ami[emoji120] [emoji120] [emoji120]
Aamin Allahuma Aamin [emoji120]
 
Kuhusu kunywa mkojo wa ngamia sio tatizo kama wanatumia kama dawa,hapa kwetu tz tunatumia pia mkojo wa punda kama dawa ya kifua.
Kuhusu kunywa mkojo wa ngamia ni tatizo sababu unasababisha ugonjwa wa MERS (Middle East Respiratory Syndrome) kulingana na World Health Organisation report ya 2015. Kinyume chake, Muhammad katika Hadithi alisema ni dawa haina matatizo!

Kuhusu mkojo wa punda kutumika kama dawa TZ sijawahi kusikia. Naona itakuwa maamuzi ya watu binafsi au kuambiwa kwamba ni dawa. Mgonjwa wa ukimwi akiambiwa mavi ya panya au mkojo wa mende ni dawa atatumia kwa imani kwamba atapona, ingawa hamna ushaidi wowote!!!

Soma link hizo...

Middle East respiratory syndrome coronavirus (MERS-CoV) – United Arab Emirates

MERS-CoV | Home | Middle East Respiratory Syndrome | Coronavirus | CDC
 
Kuhusu kunywa mkojo wa ngamia ni tatizo sababu unasababisha ugonjwa wa MERS (Middle East Respiratory Syndrome) kulingana na World Health Organisation report ya 2015. Kinyume chake, Muhammad katika Hadithi alisema ni dawa haina matatizo!

Kuhusu mkojo wa punda kutumika kama dawa TZ sijawahi kusikia. Naona itakuwa maamuzi ya watu binafsi au kuambiwa kwamba ni dawa. Mgonjwa wa ukimwi akiambiwa mavi ya panya au mkojo wa mende ni dawa atatumia kwa imani kwamba atapona, ingawa hamna ushaidi wowote!!!

Soma link hizo...

Middle East respiratory syndrome coronavirus (MERS-CoV) – United Arab Emirates

MERS-CoV | Home | Middle East Respiratory Syndrome | Coronavirus | CDC
Hawawezi kukuelewa, wamelishwa sumu. Karne ya 21 kuna watu bado wako gizani kabisa, licha ya kupelekwa shuleni na wazazi wao
 
Ndiyo maana nchi hizo sio kimbilio. Hata wao wanazikimbia. Sheria hizo watawala wanazitumia kulinda viti vyao kwa mgongo wa dini. Eti kuhama dini, capital punishment!! Uzinzi , capital punishment. Execution style: public. Huyo mungu wao huyo, mmmmhhh
 
Kwakweli hii dini ni balaaa Duniani. Alaaniwe sana aliyeileta dini hii ya kikatili inayoendeleza mauaji ya kikatili na ya kinyama kila kukicha. Dini hii Mungu wake chakula chake ni damu ya mwanadamu. Mungu huyu mkatili hutuma wafuasi wake waue watu kote Duniani kila siku. Kweli, baada ya ukomunisti uislaam ndiyo umebaki kuwa tatizo la Dunia.
 
Ndiyo maana nchi hizo sio kimbilio. Hata wao wanazikimbia. Sheria hizo watawala wanazitumia kulinda viti vyao kwa mgongo wa dini. Eti kuhama dini, capital punishment!! Uzinzi , capital punishment. Execution style: public. Huyo mungu wao huyo, mmmmhhh
Umeongea point kwamba watawala wanatumia sheria za Quran kulinda viti vyao. Na mfano mkubwa ni Saudi Arabia chimbuko la uislamu! Wao wanatumia dini kukandamiza watu. Cha ajabu, waislamu wana support hizo hukumu kama ulivyosema "uzinzi, kuhama dini na mengi mengineyo ni capital punishment.

Kabisa! Hamna mtu anataka kwenda kwa waarabu maana hawachelewi kubadilikiana wenyewe na kubadilikia wageni pia! Nchi zao hazifai kabisa maana hamna uhuru wowote zaidi kwenda msikitini 24 hours kuomba kwa Allah ambaye hajibu sala za kuacha mauwaji na vita vyao visivyo kwisha.

Mpaka karne hii bado wanajiendesha na kuishi maisha ya kibedui ya kuchinjana chinjana eti Allah alisema! Tukisema ukweli kwa faida yao wanadai eti tunatukana dini na mtume wao.
Hawawezi kukuelewa, wamelishwa sumu. Karne ya 21 kuna watu bado wako gizani kabisa, licha ya kupelekwa shuleni na wazazi wao
 
Umeongea point kwamba watawala wanatumia sheria za Quran kulinda viti vyao. Na mfano mkubwa ni Saudi Arabia chimbuko la uislamu! Wao wanatumia dini kukandamiza watu. Cha ajabu, waislamu wana support kama ulivyosema "uzinzi, kuhama dini na mengi mengineyo ni capital punishment.

Kabisa! Hamna mtu anataka kwenda kwa waarabu maana hawachelewi kubadilikiana wenyewe na kubadilikia wageni pia! Nchi zao hazifai kabisa maana hamna uhuru wowote zaidi kwenda msikitini 24 hours kuomba kwa Allah ambaye hajibu sala za kuacha mauwaji na vita vyao visivyo kwisha.

Mpaka karne hii bado wanajiendesha na kuishi maisha ya kibedui ya kuchinjana chinjana eti Allah alisema! Tukisema ukweli kwa faida yao wanadai eti tunatukana dini na mtume wao.
Kungekuwa na haki, tusingeona mafuriko yao kule Ulaya na Marekani. Ni mabedui kweli kweli. Kukata mtu kama kitoweo as if unachinja kuku, mbuzi, ng'ombe. Ni unyama uliopitiliza, ktk historia ulipata kuwepo hata huku Africa na maeneo mengine duniani. Ni ukatili ambao ulimwengu wa giza ulitawala. Cha ajabu bado wao wako huko gizani.

Mambo ya kikatili kutendeka hadharani ili kutisha jamii yamepitwa na wakati. They need to stop this
 
Hivi mwendelezo wa hii habari tayari? Naomba kusaidiwa ni post namba ngapi ili nipitie!

cc Nifah
 
Aamin Allahuma Aamin [emoji120]
Unatishwa na maandishi ya mtu ambaye amefasiri yale yaliyoandikwa na wengine na kuongozwa na hisia? Je wajua dhamira ya bandiko lake? Mapungufu ya kiutawala ya serikali ya Saudia hayaficha ukanjanja wa mleta mada
 
Ndiyo maana nchi hizo sio kimbilio. Hata wao wanazikimbia. Sheria hizo watawala wanazitumia kulinda viti vyao kwa mgongo wa dini. Eti kuhama dini, capital punishment!! Uzinzi , capital punishment. Execution style: public. Huyo mungu wao huyo, mmmmhhh


HUYO BWANA WENU TRIUMPH MWENYE HUYO MUNGU WENU AMEKIMBILIA HUKO KUTAFUTA PESA NA HAKUZINI
 
Umeongea point kwamba watawala wanatumia sheria za Quran kulinda viti vyao. Na mfano mkubwa ni Saudi Arabia chimbuko la uislamu! Wao wanatumia dini kukandamiza watu. Cha ajabu, waislamu wana support hizo hukumu kama ulivyosema "uzinzi, kuhama dini na mengi mengineyo ni capital punishment.

Kabisa! Hamna mtu anataka kwenda kwa waarabu maana hawachelewi kubadilikiana wenyewe na kubadilikia wageni pia! Nchi zao hazifai kabisa maana hamna uhuru wowote zaidi kwenda msikitini 24 hours kuomba kwa Allah ambaye hajibu sala za kuacha mauwaji na vita vyao visivyo kwisha.

Mpaka karne hii bado wanajiendesha na kuishi maisha ya kibedui ya kuchinjana chinjana eti Allah alisema! Tukisema ukweli kwa faida yao wanadai eti tunatukana dini na mtume wao.


Ni kweli kwa watu kama wewe mliozowea kwenda sauna kufanyishana yale mambo ya kiroho , mtakimbia , kwani huko mkikamatwa ni kukatwa vichwa tu

The Vatican Buys Europe's Biggest Gay Sauna
 
ADHABU YA KIFO KWA KUCHINJWA MBELE YA KADAMNASI




SEHEMU YA PILI





Katika sehemu ya kwanza ya makala hii niliandika kwa kina sana juu ya mfumo was adhabu ya kifo inavyotekelezwa nchini Saudi Arabia. Sikuishia hapo tu bali pia nilijadili kuhusu mtelelezaji wa adhabu hiyo (mchinjaji) Muhammad al-Besh.

Katika sehemu hii ya pili ya makala hii nataka nijadili visa vichache vilivyopo nyuma ya maisha ya ya watu ambao walihukumiwa adhabu hii na hatimaye kuchinjwa hadharani. Nataka kujadili ilikuwaje hasa mpaka kupelekea kuhukumiwa visa hivyo?

Katika mjadala wangu huu nitagusia zaidi visa ambavyo viligusa hisia za watu wengi na visa vingine kusababisha hata hasira ya kimataifa dhidi ya nchi ya Saudi Arabia.


911fca0601e1e4dde262cde849f0bb13.jpg




KISA #1: RIZANA NAFEEK


Umri: Miaka 24

Uraia: Sri Lanka

Kazi: Msaidizi wa Kazi za Ndani


Tarehe ya kuchinjwa: January 9, 2013, Saa 5 dakika 40 Asubuhi.





Nini hasa kilimkuta?



Rizana Nafeek binti muadilifu wa kiislamu, alizaliwa February 4, 1988 na kukulia katika kijiji cha Moothoor, wilaya ya Trincomalee nchini Sri Lanka.
Kutokana na wazazi wake kuwa wacha Mungu sana ndio maana hata alipozaliwa walimchagualia jina la Rizana mtoto wao likimaanisha "kuomba" (to pray).

Rizana ndiye mtoto wa kwanza kwenye familia yao yenye watoto wanne.

Familia yao ilikuwa ni moja kati ya familia masikini zaidi hapo kijijini, waliishi katika kijumba cha "mbavu za mbwa" kilichojengwa kwa nyasi.

Umasikini wao uliokithiri ulichangiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na hali tete ya kiafya ya baba yake ambayo ilikuwa haimruhusu kufanya shughuli nzito. Enzi ambazo baba yake alikuwa timamu kiafya, alikuwa anajishughulisha na ukataji mbao msituni, na akasitisha shughuli hizo baada ya afya yake kuzidi kuzorota kadiri siku zilivyoenda.

Kitokana na afya ya mzee Nafeeq kuwa mbaya na kushindwa kufanya kazi, ili waweze kujikimu kimaisha, Rizana na wadogo zake walikuwa wakiokota kuni msituni na kwenda kuuza kijijini, wakati ambapo mama yao alikiwa anasaidia shughuli ndogo ndogo vibarua kwa wanakijiji wengine na kulipwa ujira.
Katika mtindo huu kwa miaka kadhaa ndivyo ambavyo waliweza kuendesha maisha yao.

Kama jinsi ilivyo kwa watoto wote wanaokua katika umasikini wa kupindukia, Rizana akajikuta anapata kiu ndani yake ya kuwa mkombozi wa familia yake. Akajikuta anapata kiu ya kutaka kuitoa familia yake katika aibu ya kuwa familia inayodharaurika na walau aweze kuipa familia yake maisha yenye staha na heshima mbele za wanakijiji wengine.
Ndipo hapa ambapo moja ya binamu zake aliyepo hapo hapo kijijini Moothoor akamshauri Rizana ajaribu "bahati" yake kwenda kutafuta ajira 'Uarabuni'.

Rizana akarudi na wazo hili nyumbani na kuwaeleza wazazi wake kuwa anataka ajaribu "bahati" ya kutafuta ajira Uarabuni.
Wazazi wake walilipinga suala hili mara moja baada tu ya Rizana kulitamka. Hoja yao kuu ilikuwa ni kwamba wanaogopa mtoto wao kwenda kunyanyasika Uarabuni. Walikuwa wamesikia 'stori' nyingi sana kuhusu wafanya kazi wa ndani namna ambavyo walikuwa wananyanyaswa na mabosi wao wakifika kwenye nchi za kiarabu. Hawakutana mtoto wao Rizana naye aende akanyanyaswe, waliona ni bora aendelee kuokota kuni kijijini.


Lakini Rizana alikuwa na kiu haswa ya kuindoa familia yake kwenye umasikini wa aibu, akajitahidi kwa uwezo wake wote kujieleza kwa wazazi wake na hasa hasa ni namna gani ambavyo kwenda kwake Uarabuni kutaleta 'neema' kwenye familia yao. Baada ya kujieleza sana kwa wazazi wake hatimaye wakakubaliana naye kuhusu kwenda kujaribu "bahati" yake huko Uarabuni.


Huu ulikuwa ni mwaka 2005, Rizana alikuwa ni kabinti ka miaka 17 tu.


f06cdf483dab4f266403f680a704bead.jpg

Hapa ndio nyumbani kwa kina Rizana Nafeek, kijijini Moothoor, nchini Sri Lanka

349f4f6cbd2f65d876dba0351e731e8c.jpg

Baba na mama mzazi wa Rizana Nafeek

c17fc722545ce81ec37a4207d4e428a3.jpg

Mama mzazi wa Rizana akiwa na wadogo zake Rizana



Baada ya wazazi kukubali Rizana aende kujaribu "bahati" yake Uarabuni, ikafanyika mipango ya kuwasiliana na makampuni ya uwakala wa kutafuta watumishi wa ndani ("mahausigeli") na kuwaunganisha na 'ajira' kwenye nchi za kiarabu. Kampuni hii iliitwa Badurdeen.


Lakini Rizana alikuwa na changamoto kubwa mbili.

Mosi, alikuwa hajui hata neno moja la kiarabu au kingereza. Lugha pekee aliyokuwa anaifahamu ilikuwa ni Tamil.

Pili, Rizana alikuwa hajafikisha umri wenye kumruhusu kwa mujibu wa sheria za kimataifa kupata ajira kwenye nchi ya kigeni.


Lakini madalali hao walimtia moyo kwamba hakuna changamoto yoyote ambayo wao watashindwa kuisawazisha alimradi tu akiwa tayari kwenda kufanya kazi Uarabuni.

Kuhusu kutojua kiarabu au kingereza, walimtia moyo kwamba wako wasichana wenzake wengi tu ambao nao walikuwa kama yeye wanafahamu 'lugha ya mama' pekee na Kiarabu walikwenda kukijulia huko huko kwenye ajira zao. Suala hili lilikuja kumgharimu sana Rizana huko mbeleni.

Pia kuhusu umri, mawakala hao wa ajira walimtengenezea Rizana cheti kingine cha kuzaliwa cha kughushi ambacho kilionyesha kuwa Rizana ana umri wa miaka 23.


Baada ya mipango hii yote kukamilika, familia ya Rizana wakakopa fedha kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki na kuwalipa kampuni ya Badurdeen ada ya huduma hii ya kumuunganisha binti yao na ajira Uarabuni.

Mkopo huu waliokopa familia ya Rizana kutoka kwa ndugu, jama na marafiki walikuwa wameahidi kuulipa pindi tu ambapo Rizana akifika Uarabuni na kuanza kupokea mshahara.


*********


Siku ya tarehe 1April 2005, Rizana aliwasili kwenye mji wa *Dhawadhimi* (wengine hutamka "Dwadmi") nchini Saudi Arabia, karibu kabisa na mji mkuu wa nchi hiyo, Riyadh.

Muajiri wake ambaye alikwenda kukabidhiwa kwake alikuwa ni Bw. Naij Jiziyan Khalaf al Otaibi ambaye alikuwa ni afisa wa ngazi za juu katika wizara ya fedha ya Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa taratibu za kazi nchini Saudi Arabia, kazi ya Uyaya (Nanny) na 'uhausigeli' (house maid) huwa zinatenganishwa lakini mara nyingi binti akiajiriwa anajikuta akifanya shughuli zote hizi mbili, yaani shughuli za nyumbani kama upishi na usafi (house maid) na shughuli za uangalizi wa watoto wadogo (nanny).
Hiki pia ndicho kilichomba Rizana kwa muajiri wake Familia ya Otaibi. Alijikuta anawajibika kufanya shughuli zote za nyumbani za usafi na upishi na papo hapo akiwajibika kuwa muangalizi wa watoto wadogo waliopo kwenye familia ya Otaibi akiwemo mtoto mchanga wa miezi minne ambaye aliitwa Kayed.


Kwa wiki kadhaa Rizana alichapa kazi pasipo kuwepo na mgogoro wowote na mabosi wake wala kuwepo kwa malalamiko kutoka upande wake.

Kazi ikaendelea, huku ndoto yake kichwani ya kuitoa familia yake katika umasikini uliokithiri ikizidi kuchanua kichwani mwake.




"Siku ya hatma, kiza hakichelewi"


Miezi miwili baada ya Rizana kuwa katika ajira, yaani siku ya tarehe 22 May 2005, Bw. Otaibi na mkewe waliondoka nyumbani asubuhi kama ilivyo ada.

Rizana naye aliendelea na shughuli zake kama kawaida ya siku zote.

Mnamo majira ya kama saa 6 na nusu mchana akaanza kumpatia maziwa mtoto mchanga Kayed ambaye naye alikuwa ni jukumu lake kama siku zote. Maziwa haya alikuwa anampatia kwa kutumia chupa ya watoto ya kunyonyeshea.

Akiwa anaendelea kumpa mtoto maziwa, alipokuona ameshiba akamuachia chupa achezee na kisha kwenda jikoni kuangalia maendelea ya chakula alichokuwa anapika. Ilimchukua dakika kadhaa akiwa jikoni, takribani dakika tano nzima na aliporejea alishapigwa na butwaa kumkuta mtoto mchanga Kayed chupa ameweka mdomoni kama anainyonya lakini amefumba macho.

Rizana akamuinua Kayed na kuanza kumfungua macho. Lakini kila akimfungua macho mara moja yanafunga tena. Lakini pia akagundua kuwa Kayed alikuwa hapumui.

Baada ya kumchunguza akagundua kwamba, Kayed alikuwa amebanwa pumzi (ame-suffocate) kutokana na kunyonya vibaya chuchu ya chupa ya maziwa na kusababisha kuziba koo la kupitisha hewa.

Kutokana na utoto wake (kumbuka ni binti wa miaka 17 tu) akaanza kulia na yeye papo hapo asijue afanye nini.


Watoto wengine wadogo wa familia ya Otaibi waliokuwa wanacheza chumba kinachofuata waliposikia kilio cha Rizana walikimbilia chumba hicho alichomo na kumkuta analia huku anampindua pindua mtoto na kujaribu kumuamsha Kayed.

Watoto hao nao wakabaki wamepigwa butwaa tu wasijue nini kinaendelea au wamsaidieje Rizana au Kayed.


Ghafla muda huo huo Mke wa Otaibi akarejea nyumbani na moja kwa moja akaelekea chumba ambacho alisikia kilio kinatoka huko tangu yuko getini.

Alipofika alimkuta Rizana amembeba Kayed mikononi huku analia. Mara moja mke wa Otaibi akamchukua Kayed kutoka mikononi mwa Rizana na mara tu baada ya kumgusa ndani ya sekunde chache aligundua kuwa mtoto mchanga Kayed ameshafariki.

Kama vile mbogo aliyejeruhiwa, Mke wa Otaibi alimrukia Rizana kwa hasira na kuanza kumshambulia huku akipiga yowe la kilio, akirudia neno moja tena na tena….

"KWANINI UMEMUUA MWANANGU..!!"




Itaendelea post inayofuata hapo chini...
 
ADHABU YA KIFO KWA KUCHINJWA MBELE YA KADAMNASI



SEHEMU YA TATU


Inaendelea kutoka ilipoishia sehemu ya pili….


Yapata kama saa 7 na nusu hivi, polisi walipogiwa simu na kufika nyumbani kwa familia ya Otaibi.

Walipofika mama mwenye nyumba akawaeleza kwamba Rizana amemuua mtoto wake kwa kumnyonga shingo.
Mama mwenye nyumba alieleza maelezo haya mara baada ya watoto wake kumwambia kuwa walisikia Rizana analia chumba cha pili na walipoenda wakamkuta anamgeuza geuza mgeuza mtoto mikononi mwake. Kwa maelezo haya ya watoto, mama huyu akahitimisha kuwa Rizana amemuua mtoto wake kwa kumnyonga shingo.

Pamoja na maelezo hayo, mama mwenye nyumba aliwaeleza polisi kuwa asubuhi ya siku hiyo alikuwa amemfokea Rizana kutokana na kutofanya usafi vizuri, kwa hiyo aliamini kuwa Rizana alimuua mtoto wake ili kulipa kisasi kwa hasira za kufokewa.

Moja kwa moja Rizana akachukuliwa mpaka kituo cha Polisi. Alipofikishwa na kituoni na kuanza kuhojiwa ndipo ambapo alijua ni namna gani kutokujua kuunga hata sentesi moja ya kiarabu kuna mgharimu.

Ilikuwa ni ngumu hata kumafanyia mhojiano… Rizana alikuwa hajui kuongea kiarabu, lugha pekee aliyokuwa anaifahamu ni Tami na hakukuwa na polisi yeyote yule ambaye alikuwa anajua kuongea Tamil.

Kwa hiyo alipokuwa anaulizwa ajieleze ni nini kimetokea alibakia kuduwaa tu asijue aseme nini na ukijumlisha kipigo alichopewa na mwenye nyumba pamoja na mtoto kumfia mikononi mwake, Rizana alikuwa katika mshituko kana kwamba amechanganyikiwa.


Baadae polisi wakapewa taarifa ya daktari kwamba mtoto amefariki kwa sababu ya "suffocation" (kukosa hewa) na si kunyongwa shingo kama mama yake alivyoeleza. Lakini hii haikutosha kuwafanya polisi wamuone Rizana labda hana hatia.


Kuna suala moja kubwa lenye ukakasi mwingi kuhusu adhabu ya kifo nchini Saudi Arabia.
Watu wote ambao huwa wanahukumiwa adhabu hii na hatimaye kuchinjwa hadharani huwa wanakili kufanya kitendo hicho na huwa wanakiri kwa maandishi na kuweka sahihi zao.


Hili ni suala la kushangazo mno, ni vipi kila anayechinjwa lazima akiri kwa maandishi juu ya kitendo anachoshutumiwa nacho.

Kupitia mkasa huu wa Rizana, kuna masuala nyeti mengi yaligundulika kuhusu utesaji ambao polisi huwa wanawafanyia washtakiwa ambao kesi zao zina adhabu ya kifo ili waweze kukiri na kusaini nyaraka za kuthibitisha kujutia kwao walichokifanya.

Hiki ndicho ambacho pia kilimkuta Rizana alihojiwa kwa wiki kadhaa pamoja na kuteswa na polisi ili akiri kumuua mtoto wa muajiri wake.

Shida kubwa ilikuwa na lugha kutofautiana. Kila ambavyo Rizana alijitahidi kueleza upande wake wa nini kilitokea hakuna mtu ambaye alimuelewa hapo polisi alipokuwa anashikiliwa kwa kuwa hakukuwa na mtu ambaye alikuwa anazungumza lugha ya Tamil.


Baada ya wiki kadhaa alipatikana mtu ambaye alidai kuwa anaifahamu lugha ya Tamil. Kijana huyu alikuwa ni raia kutoka Malaysia ambaye alikiwa hapo Saudi Arabia akifanya kazi ya kuchunga kondoo.

Kupitia kijana huyu mahojiano yakaendelea kwa kasi ya ajabu.

Lakini alichokuja kuongea Rizana huko mbeleni ni kwamba kijana huyo hakuwa anajua Tamil kwa ufasaha na hakuamini kuwa alikuwa anatafsiri kwa usahihi kile alichokuwa anakiongea.


Baada ya mateso ya miezi kadhaa hatimaye Rizana alifikishwa mahakamani.

Kama ambavyo nilieleza katika sehemu ya kwanza ya mfululizo wa makala hii, kwamba nchi ya Saudi Arabia wanatumia mfumo wa Sharia ya Kiislamu (kwa tafsiri yao) katika kuendesha mashataka.
Kwa hiyo mambo mengi ya kisheria yaliyomo katika mfumo wa sheria wa kawaida huwa hayatekelezwi nchini Saudi Arabia.

Kwa mfano Rizana akishatakiwa na kesi kuendeshwa pasipo kupewa mwanasheria wa kumtetea.

12ebc30b030c098bf789b112a7be9354.jpg

fb3b59df53931b90288d8e593405d498.jpg

Maandamano kudai haki itendeke na kuachiwa kwa Rizana

95489d661258ec86dbee72f64f000175.jpg

Familia ya Rizana[



Kesi ya Rizana ilizua mjadala mzito wa kimataifa.

Wanaharakati wengi walihoji ni kwa namna gani Saudi Arabia walifanya uzembe mpaka binti wa miaka 17 akaingia ndani ya nchi yao na kupewa kibali cha kufanya kazi.

Lakini pia watu walihoji namna ambavyo kesi ilikuwa inaendeshwa pasipo Rizana kupewa msaada wa kisheria.

Kesi ya Rizana ilivuta hisia za wengi sana huku watu wengi wakiamini kuwa Rizana hakuwa na hatia na kwa kuwa Rizana hakuwa raia wa Saudi Arabia na wala hatoki kwenye familia yenye ushawishi ilikuwa ni dhahili kwamba kesi hiyo lazima itaisha kwa Rizana kuhukumiwa kifo kwa kuchinjwa mbele ya kadamanasi.

Maandamano yalifanyika katika nchi nyingi za Asia na Ulaya kuishinikiza serikali ya Saudi Arabia kutenda haki katika kesi ya Rizana.


Hatimaye mwaka 2006 upande wa mashataka wakawasilisha mahakamani "confession" ya Rizana ambayo iliandikwa na polisi kwa kiarabu na Rizana kutia sahihi ya dole gumba.

Nyaraka hiyi ilisomwa mahakamani na kuonyesha kwamba Rizana alikuwa amekiri kumuua mtoto Kayed wa boss wake.

Lakini January 30, 2007 Rizana alisainu Affidavit kujieleza upande wake wa nini kilitokea.

Alisema hivi, nanukuu;


"..madam alirudi nyumbani saa 7:30 mchana na baada ya kumuona mtoto alianza kunishambulia na kunipiga mpaka damu zikaanza kunitika mdomoni na puani.
Baada ya hapo nilichukuliwa mpaka kituo cha polisi ambako nako nilidhalilishwa na kuendelea kupigwa kwa mikanda ya polisi na kulazimishwa kukiri kuwa nimemuua mtoto.
Walinipiga na kunitisha kuwa nisipokiri wataendelea kunipiga mpaka nife. Ili kujiepusha na maumivu haya na kutokana na kuchanganyikiwa kwa kipigo, nilitia sahihi yangu katika karatasi ya maelezo yalikuwa yakionyesha kuwa nimuua mtoto wa muajiri wangu. Lakini nasema ukweli na naapa kwa Allah, sikumuua yule mtoto."



Mwisho wa nukuu.


Licha ya hoja hizi za Rizana, lakini siku ya tarehe 16 June 2007, mahakama ikamuhukumu Rizana Nafeek adhabu ya kifo kwa kukatwa kichwani mbele ya umma.


Hukumu hii iliibua hasira zaidi za wanaharakati za haki za binadamu duniani kote.

Rais wa Sri Lank yeye binafsi alituma maombi maalumu mara mbili kwa mfae wa Saudi Arabia ili aweze kumpa msamaha Rizana lakini mara mbili zote hizo ombi lake lili kataliwa na King Abdullah

Juhudi za kumuokoa Rizana hazikuishia hapo tu, hata Prince Charles aliingilia na kutoa ombi lake kwa King Abdullah ampe msamaha Rizana lakini bado Mfalme alikataa.

Kuna wengine walienda mbali zaidi hata kuanzisha kampeni ya kumtaka malkia katika maadhimisho yake ya "Diamond Jubilee" apaze sauti kuungana na wanaharakati wote kutaka Rizana asikatwe kichwa hadharani.


Serikali ya Saudi Arabia ilikuwa inapewa presha kutoka kila kona ya dunia. Hii iliwafanya wahahirishe utekelezaji wa adhabu ya Rizana mara kwa mara.


Lakini kama nilivyosema jana kuwa, "Siku ya hatma, kiza hakichelewi", hatimaye ukafika mwaka 2013. Na ulipofika mwezi January siku ya tarehe 9, Rizana alipelekwa katika uwanja wa "machinjio" kukutanishwa na binadamu ambaye kukata vuchwa vya binadamu wengine ndio amefanya kuwa wito wake wa Maisha, Rizana akakabidhiwa mikononi mwa Muhammad al-Beshi, mchinjaji rasmi wa binadamu wa serikali ya Saudi Arabia.


Zoezi la kumchinja Rizana ilikuwa ni moja ya changamoto kubwa ambayo Al-Beshi kiwahi kukutana nayo katika wito wake huu "mtakatifu". Kwa sababu kama ambavyo mwenyewe al-beshi huwa anaeleza kuwa watu wanaotakiwa kuchinjwa wakifikishwa mbele yake wanakuwa wanyonge na hawana nguvu kabisa na wamekata tamaa kabisa na hivyo wanafanya kila kitu ambacho anawaeleza. Akiwaambia inamisha kichwa, wanainamisha na anawakata kichwa kwa kasi ya ajabu kama umeme.

Lakini haikuwa hivyo kwa Rizana… Rizana alikuwa anapaparika na kupiga mayowe ya kila namna akilia kwa uchungu akirudia maneno yale yale tena na tena…

"..Sijamuua yule mtoto, sijaua mtoto, sijamuua yule mtoto, hii hadhabu ni Haramuuu, haramuuuuu..!"


Kumsikia Rizana alivyokuwa analia na jinsi walivyokuwa wanahangaika kumshika ili wamchinje ilikuwa inaweza kukufanya utokwe na mchozi shavuni.

Baada ya purukushani nyingi, hatimaye ilipotimia saa 5 na dakika 40 siku hiyo ya tarehe 9, Januaru 2013… Al-Beshi alipitisha sime shingoni kwa Rizana na kutenganisha kichwa na kiwili wili cha Rizana Nafeek.
Na huu ndio ulikuwa mwisho wa maisha na Rizana juu ya uso wa dunia.


Tazama video hapo chini…

Tahadhari: Maudhui ya ukatili mkubwa





Kuchinjwa kwa Rizana kuligusa ulimwengu kwa namna ya tofauti sana.

Serikali ya Sri Lanka walilaani vikali kitendo hicho cha raia wao kuchinjwa hadharani huku wakiamiani kuwa hakuwa na hatia.
Kabla ya kuanza kwa shughuli za Bunge, wabunge wote wasimama kwa ukimya wa dakika moja kumkumbuka Rizana.

Pia katibukuu wa Umoja wa Mataifa wa kipindi hicho alilaani vikali kitendo kilichofanyika.

Taasisi ya Asian Human Rights Commission nao walitoa tamko kali kulaani kitendo hicho.

Serikali ya uingereza nao walilaani kitendo kilichofanywa na serikali ya Saudi Arabia.


Si hao tu bali pia Ufaransa na Umoja wa Ulaya walitoa matamko kulaani kitendo cha kuchinjwa na Rizana.



Serikali ya Saudi Arabia katika juhudi ya kujisafisha kwenye Jamii ya kimataifa, wakapeleka "rambi rambi" ya dola 16,000 kwa familia ya Rizana iliyoko kijiji Moothoor, nchini Sri Lanka.
Licha ya umasikini wao wa kutupwa, lakini Familia ya Rizana ilikataa kupokea rambi rambi hiyo.





Hiki ni kisa #1…. Usikose kisa #2 nitakachoweka siku chache zijazo



The Bold
 
SEHEMU YA PILI


Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij adden



bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel ngushi Donald stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom